Mke wangu amekutwa HIV+

Ndoa kama NDOA.

Mmmh ndoa NGUMU nyie.

Nikiwaambia msioe utasikia ""UNA MATATIZO YA SAIKOLOJIA""

Mmmh haya bana ENDELEENI TU KULA MIJEREDI.

MUNGU awaongoze...

#YNWA
 
Jamaaa inabidi amshauri mke wake arudi hosp

Yaan mpaka ngozi inaanza kua ya njano, kuna uwezekano INI lake limeanza pata shida.
Ndio inawezakana hata hiyo HIV positive hana kwa kielimu changu kidogo inaonesha Kama Mke wa jamaa ana hepatitis ndomana ya hiyo yelow ini limeanza kuleta shida
 
Cha kushangaza baada ya Kama miezi 6 msichana akaolewa na jamaa mwingine ,hiyo kidogo ilitushtua kwamba imekwaje gafla hivo ,inawezekana maruweruwe au daktari katoa vipimo feki
yeah, kuna uwezekano dokta alipangwa jamaa ateme mzigo.
 
Mimi siamini uwepo wa ukimwi kwasababu maeneo niliyopita na nikipima naambiwa sina naamini kabisa hili gonjwa ni kamchezo flani tu
Wanasema virusi vikikaa mwilini mwa mtu kwa muda mrefu chance ya kuambukiza inapungua tofauti na yule ambaye ndio kaupata. Kwa hiyo yawezekana hayo maeneo uliyopita hadi unashtuka ni kwa sababu tayari wamekaa navyo au tayari wanatumia dawa.

Mwalimu wangu aliyenifundisha semina kuhusu VVU alikuwa anasema yeye anajiamini akitembea na Malaya kuliko mtu wa kawaida. Huwa ananishangaza sana.
 
Ndio inawezakana hata hiyo HIV positive hana kwa kielimu changu kidogo inaonesha Kama Mke wa jamaa ana hepatitis ndomana ya hiyo yelow ini limeanza kuleta shida
Hepatitis vipimo vyake vinapatikana katika hospitali za zote? Kama za wilaya au rufaa au kuna hospital maalum?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Basi kama kweli ngwengwe ipo itabidi niokokee kwasababu kwa miaka 10 yangu toka 2008 mpaka 2018 haikua ya kawaida...sikuwahi kupoa kabisaaa na nimechomokaa si jambo dogo.
 
Basi kama kweli ngwengwe ipo itabidi niokokee kwasababu kwa miaka 10 yangu toka 2008 mpaka 2018 haikua ya kawaida...sikuwahi kupoa kabisaaa na nimechokaa si jambo dogo.
Okoka tu na utoe sadaka ya shukurani na uoe kabisa.
 
Thanks mkuu hapa nimepata kitu hii ndo JF tunayoitaka
 
Mkuu, check message box yako
 
Pole sana mkuu! Issue ya namna hiyo ilitokea hata kwa jamaa yetu wa hapa job.
Lakin yeye alioa tu mtu ambaye alimuamini kwa macho kulingana na mwonekano wa afya na umbile lake!
Kwa vile alikuwa pisi kali , chapchap jamaa akampiga mimba , wakati mtoto kazaliwa ndipo jamaa akagundua hilo siku mkewe alipotuma aletewe mikoba akiwa kwa mama mkwe ndipo katika kusearch jamaa akaziona hizo ARAV katika moja ya mabegi.
Ndo kwenda kumchukua wife, walipopima akakutwa ni HIV+ , lakini yeye jamaa hakuwa ameathirika!
Jamaa alipotafuta taarifa zaid akagundua kuwa bidada alishaanza kumeza hivo vidonge hata kabla hawajajuana, lakini ilikuwa siri yake!
Kilichofanyika walitengana lakini walikubaliana kuendelea kulea mtoto. Hadi sasa dogo ana miaka 4.
Kwa hiyo suala lako ni kama la huyo bwana. Hivyo chakufanya mchukuwe wife wako nendeni mkapate ushauri kutoka kwa Daktari, ili kama atashauri mtengane nae basi demu asione kama ni maamuzi yako binafsi bali ni kutekeleza ushauri wa kitaalam!
Mtoto kama Mungu kamjalia afya njema, anatakiwa anyonye ziwa la mama kwa kipindi cha miezi 6 tu, kisha mnamuachisha. Hicho ni kipindi ambacho maumbile ya mdomoni mwake huwa ni laini, yaani anakuwa hajaota meno!
Meno ya mtoto ndio husababisha vidonda kwenye nyonyo za matiti ya mama na hivyo kumuweka mtoto katika hatari ya kuambua ugonjwa!
 
Naomba kufahamu iyo yellowish inayotokea mapajan pindi anelala alaf akiamka inapotea, inakuwa ni nin wajuzi
 
Kwanza nikupe pole kwa maswaibu yaliyokukuta lakini pia nikupe big up kwa kuupata uhakika kuwa mwenza wako ni muathirika wa HIV na bado ukawa na ujasiri wa kuvumilia na kukabili changamoto kwanza kwa kwenda kanisani lakini pia kuja hapa JF kuomba ushauri hakika hiyo ndi sifa ya mwanaume KUKABILI CHANGAMOTO ZINAZOKUJA NA KUTOTETELEKA.Najua hivi sasa una mawazo mengi na ndio maana umekuja kupumua hapa JF na wengi wamekupa pole,kuuliza maswali kukushauri ama kwa uzoefu wao ama kitaalamu lakini wengine wamepondea au kukudharau kwa kadri ya kila mmoja alivyolipokea mimi upande wangu nataka nikushauri yafuatayo.

  • Maisha lazima yaendelee huwezi kuyabadilisha yaliyokwisha tokea songa mbele achana kabisa na kutaka kujua ukweli wa mwenza wako alipataje,na nani, lini ukiyajua yatakuumiza moyo na utakuwa mwanzo wa kupata stress ,mfadahaiko na magonjwa mbalimbali mfano shinikizo la moyo n,k.Wanawake ndivyo walivyo kukuambia ukweli ni 1 kwa kumi.
  • Wasiliana na wataalamu wa Hospitali kujua hali ya mtoto kama ameambukizwa au hapana kwa sababu nijuavyo mimi mama anapoanza clinic kipindi anapokwa mjamzito anapimwa afya na mojawapo ni kujua kama ana maambukizi basi wakati wa kujifungua kuna namna huyu mjamzito ataambiwa ili kumkinga mtoto asipate maambukizi kutoka kwa mama siku hizi kuna njia nyingi
  • Mnapofunga ndoa mlikula kiapo Kanisani kuwa mtakuwa pamoja katika shdia na raha,afya na ugonjwa ndiyo hapa sasa unatkaiwa kudhihilsha hicho kiapo.Tena Biblia inasema mke atamtii mume bali mume atampeda na kumlinda mke wake.Mshukuru Mungu umzima ni wakati wa ku kaa na mwenza kwa hekima na busara japoa haitakuwa rahisi atakuwa defensive ,mkali ili kuficha uongo wake ila muda ni mwalimu mzuri mtakuja pata suluhisho zuri baadaye hata miaka 2,3,5 ijayo
  • Utapata ushauri mbali mbali kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki na hapa JF ila sikiliza sauti yako ya ndani kutoka kwa Mungu sisi ni wasaauri tu lakini joto la jiwe anayelijua ni mjusi(wewe).
  • Wewe si kwanza kupata tatizo kama hili na sio wa mwisho ..wengi wanaugua na wamekubali hali hiyo maisha yanaendelea hivyo jpe moyo,,sasa ni wakati wa kupambana maradufu kutafuta maisha na wewe kujitunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…