dustless
JF-Expert Member
- Oct 21, 2016
- 796
- 714
Nimekupata sasa. Sasa alitafanwa na mwl ni mdogo mtu, si ndo hivo....Mdogo wa mke wa mwalimu alikaa sehemu nyingine, alikutana na dada kwenye biashara tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekupata sasa. Sasa alitafanwa na mwl ni mdogo mtu, si ndo hivo....Mdogo wa mke wa mwalimu alikaa sehemu nyingine, alikutana na dada kwenye biashara tu.
Jamaa alikuwa mwalimu wa high school mkoani, alipata nafasi ya kuja kusoma shahada ya uzamili USDM. Rafiki yake aliyesoma nae first degree alimwambia bwana usihangaike kutafuta nyumba tutakaa wote kwangu.
Baada ya muda mke wa mwalimu alifika mjini, mdogo wake ana biashara ya catering, sasa aliona muda ambao mume wake anasoma ni kheri amsaidie mdogo wake wakati anampa hubby company. Kwakweli mke wa mwalimu kwenye biashara alilipwa vizuri tu, mdogo wake hakumchukulia kama kibarua ila alikuwa anamsaidia dada.
Sasa kule nyumbani wanawake wawili kukaa nyumba moja ilikuwa ngumu, mwenyeji wao alikuwa ameoa na alichoka malalamiko kutoka kwa mkewe kila siku. Mwenyeji alijipanga jinsi ya kuwatowa lakini anashindwa pa kuanzia. Siku moja alimkuta mke wa mwalimu peke yake, akamwambia shemeji nina mazungumzo na wewe, una jua mume wako anatembea na mke wangu.
Mke wa mwalimu alimjibu, hivi unajua mume wangu anafundisha wasichana wa form 5-6 na ni wazuri kweli, wala hajawahi kuwatongoza, huyu mkeo ana nini cha zaidi? Hembu jipange uje na story nyingine.
Baada ya hapo mwalimu na mkewe ilibidi watafute nyumba, lakini nilipopewa hii story nilimsifu sana mke wa mwalimu.
Kwanza kwa kupanick jamaa angepata mgao, alafu unajuta baadae.