Mke wa mtu kuomba pesa kwa EX wake...

Mke wa mtu kuomba pesa kwa EX wake...

Ha ha kazi sana hawa watu..
Huyo mke wa mtu wala hana shida ya hio hela anayokuomba, lengo lake alitegemea wewe utamuomba lakini anakuona hauna hata mpango wa kumuomba, hivyo yeye ameamua kukufikishia ujumbe kwa kukuomba pesa, maana hua wanajua kabisa pesa ya mwanaume hua haitoki hivihivi ni lazima tu ilipiwe fadhila.
 
Kama pesa ipo mpatie, kuachana si uadui. Kuna mahali kakwama na mume wake naye labda ndo hivyo tena mambo yake yapo kwenye mawe. Kumbuka pia pesa kwasasa ina macho hivyo si kila mtu atakayeombwa msaada atapewa, yawezekana kahangaika sehemu nyingi kakosa kaona akimbilie kwako utamfaa maana uliwahi kumfaa kipindi mko pamoja.
 
Yaani wewe ungekuwa nayo hiyo pesa ya kumpa Tusingefika kote huku,mbona hukuuliza mke wa mtu kutoa papuchi kwa ex- wake?
 
Amen
Kama pesa ipo mpatie, kuachana si uadui. Kuna mahali kakwama na mume wake naye labda ndo hivyo tena mambo yake yapo kwenye mawe. Kumbuka pia pesa kwasasa ina macho hivyo si kila mtu atakayeombwa msaada atapewa, yawezekana kahangaika sehemu nyingi kakosa kaona akimbilie kwako utamfaa maana uliwahi kumfaa kipindi mko pamoja.
 
Mkuu, Kama mliachana kiroho Safi, huyo anakuwa rafiki mzuri tu, msaidie kwa kadri ya uwezo wako. Maisha Ni mduara huwezi jua kesho yake. Japo si kwa kufikiri kesho, msaidie tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli hujui la kufanya? Kuna karaha flani hivi ukifahamu unatakwa, hako ndo kanakupitia. Ushauri ni usiwe vuguvugu, we fanya au mblock.
 
Mkuu fikiria Mara mbili. Vp kama mkeo anafanya hvyo je we ungejisikiaje?
Ushauri wangu mpotezee kabisa mwambie abaki Na ndoa yake kwa sababu kuna siku atakuja kukuletea matatizo makubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom