Mkuu naona umeamua kuchukua tahadhari kuogopa mchango wa matusi na kejeli mapema, hongera.
Kwa upande wangu hata kama nitakuwa nafanya uzinifu na mwanamke yeyote yule yaani a single lady or married one hakika nitakuwa wa mwisho kumshauri mtu yeyote kutenda kama ninavyofanya, zinaa ni dhambi kubwa na mbaya zaidi na mke wa mtu jamani haikubaliki hata kidogo.
Matatizo kwenye ndoa yapo mengi kama uliyoyataja ya huyo dada na mume wake, lakini bado sio sababu ya msingi kwa mmoja wa wanandoa kumsaliti mwenzake. Jamani maadamu tatizo limetokea wakati ndoa ilikwisha fungwa tena yenye watoto wawili, kumbe jambo la msingi kwa huyo mama ilikuwa kumsaidia huyu mwenzake aondokane na matatizo yanayomkabili kwa sasa ili apate tiba na kurudi katika hari yake ya kawaida na waendelee kutenda kadri ya Mapenzi ya Mungu (tendo la ndoa ndani ya ndoa ambalo kwao ni takatifu). Huyu mama (maharage ya mbeya) amefanya kosa kuisailiti ndoa yake ambayo aliapa kuilinda katika shida na raha, arudi nyuma na kumsaidia mwenzake.
Na huyu kijana hakika amepotea pakubwa, anapoteza muda kwa kuwa na mahusiano na mke wa mtu, zinaa yoyote ni dhambi lakini angelikuwa anafanya na binti (single) tungesema ipo siku watatubu hiyo dhambi na kuingia kwenye ndoa takatifu na kuanza maisha yao yenye kumpendeza Mungu na jamii kwa ujumla. Mwambie aache, anapoteza muda wake, anakuza familia ya mtu mwingine, atakumbuka shuka kumekucha, atasahau hata kuoa aliye wake, ipo siku ataazibiwa vibaya sana hapa hapa duniani.
Na kwa huyu kiunganishi wao sio mzuri hata kidogo, anafanya biashara haramu ya kuuza mke wa mtu, anachangia kuvunja ndoa ya mtu ilihari yeye anaendelea na ndoa yake, haikubaliki hata kidogo. Ndoa na iheshiwe na watu wote jamani, na kwenye ndoa sio tendo la ndoa tu (ngono).
Pole, ila mwambie aache kwa manufaa yake binafsi na familia yake