Mke wa mtu ataka kuwa dereva Bodaboda

Mke wa mtu ataka kuwa dereva Bodaboda

Kamwe siwezi kupanda bodaboda inayoendeshwa na mwanamke kwani kifo ni nje nje, alafu mi kama ni mke wangu ndo katoa propasal ya kuwa dereva bodaboda basi taraka lazima imuhusu sana.

Mkuu jaribu kuchunguza katika udereva mwanamke saiv kashika chart ! Kwanza no wapole wanaendesha kiustaraabu sio ukibebwa na goswe anakukimbiza mpaka machozi yaungane kisogoni*
 
Utani bwana na wewe hutaki kutabasamu ukiwa jf mkuu?
 
Mke wng siwezi kumruhusu kuwa dereva wa bodaboda hata siku moja... Kazi nyingine matatizo tu bora hawe muuza vitumbua na maandazi lakini bodaboda noooo

Mkuu inategemea na tabia ya huyo mkeo,kama tabia yake ni mzuri itaendelea kuwa mzuri na kama tabia ni ziro hata akae nyumbani ataharibu tu.
 
Kila kitu kinawezekana kama hatashawishika kutumia viroba

Niliwahi kumuona dada mmoja hapa kahama anaendesha boda boda na anaonekana kujiheshimu,ingawa sijui mambo ya kwenye familia
 
Hata kama maisha magumu my wife hawi dereva wa bodaboda.

Bora nipambane mimi yeye anipikie nyumbani na kuwatizama wanetu.

Mkuu kutokana na ugumu wa maisha unajikuta unamruhusu
 
Ni wazo zuri ila kiusalama kidogo inakuwa ni shida japo usalama hata kwa man's ni muhimu, ikiwa ataweza kumudu vishawishi na kufanya kazi kwa kutwa basi itasaidia familia

Nafikiri kwa suala la usalama ni jepesi kwa huyo mama kukataa tripu za mbali sana na mji pia kuwa na muda muafaka wa kufunga kazi.
 
Kamwe siwezi kupanda bodaboda inayoendeshwa na mwanamke kwani kifo ni nje nje, alafu mi kama ni mke wangu ndo katoa propasal ya kuwa dereva bodaboda basi taraka lazima imuhusu sana.

Mkuu unatisha sana
 
kama ni mkeo utakubali aendeshe boda boda au kwa vile ni wa mwenzio....majukumu ya mke nyumbani atamwachia nani kwa mfano...

Atamwacha msichana wa kazi,ili yeye apambane kuongeza kipato ndani ya familia kwani 1+1 unapata 2.
 
Atamwacha msichana wa kazi,ili yeye apambane kuongeza kipato ndani ya familia kwani 1+1 unapata 2.

hujanishawishi...kama ni kuongeza kipata wanunue hiyo boda boda apewe kijana atakaye kuwa analeta hesabu jioni na mama ataisimamia kwa karibu!
 
Back
Top Bottom