Jpinduzi
Senior Member
- Feb 26, 2011
- 136
- 68
Kwa nini unakosa akili juu ya jambo hili. Ni kitu gani kimekupofusha macho usione ya kuwa uzinifu ni mbaya? Biblia inasema; Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomangamiza nafsi yake. (Mithali 6:32)Mimi ni kijana mwenye umri fulani tatizo linalo nisumbua ni kwamba sehemu tunapoishi kuna jamaa ameamia yeye pamoja na mke wake. Wakati wanaamia sehemu ambayo mimi naishi mara ya kwanza huyo mwanamke nilijua anakaa na kaka yake kutokana na jamaa kuonekana kuwa mkubwa kiumri kushinda huyo mwanamke ambaye mimi nilikuwa najua kuwa ni kaka yake. Huyo jamaa amepata ajali na anatembelea machuma yale ya kusukuma halafu na yeye anasogea kumbe nivyokuwa nadhani sivyo huyo jamaa alikuwa ni mmewe. Huyo mwanamke tumezoeana sana mpaka kufikia hatua ya kuchukua namba yangu ya simu. Sasa tatizo ambalo linanisumbua ni kwamba huyo mwanamke ananitaka mimi kimapenzi na anaongea maneno mabaya juu ya mmewe. Huyo mwanamke ana pesa ameniahidi kunipa kila kitu nitakacho kihitaji tatizo mimi namwonea huruma mmewe kwa hali aliyo kuwa nayo nahisi nikimkubalia huyo mwanamke itakuwa ni dhambi kumwa ambayo sijawai kuifanya tangia nizaliwe. Kwa sasa mmewe yupo kama mlemavu kwa kuwa hatembei nishaurini jamani nifanyeje nimkubali au nimkatae...!! Pesa nahitaji tatizo namuonea huruma mmewe NIFANYAJE....?
Ni dhahiri ya kwamba palipo na zinaa pana uharibufu, na wengi wanaangamia. Na nataka nikuambie ya kuwa Roho Mtakatifu alishakushuhudia wewe mwenyewe kuwa hujawahi kufanya dhambi kama hiyo sasa unataka uteketeze nafsi yako kwa ajili ya pesa?Hapana tena nakemea kwa nguvu zote,shetani aliyekukamata na ashindwe