TANZIA Mke wa msanii Mrisho Mpoto afariki dunia

Kifo ni kifo tu
 
Kifo huongea.. Hutoa taarifa ya mapema❗

"Mke wangu alinipigia simu akaniambia mume wangu naona kama hali sio nzuri presha imepanda, tukamchukua tukampeleka Temeke [Hospitali] akatibiwa vizuri saa nane usiku tukarudi nyumbani...

...akaniambia hivi mume wangu mara ya mwisho mimi na wewe kuoga pamoja ni lini yani tukawa tunataniana utani utani, akaniambia bwana nataka leo uniogeshe, si unajua mke wako mgonjwa bwana siwezi kuoga mwenyewe nipeleke ukaniogeshe...

...basi nikaenda kwenye jakuzi nikajaza maji nikamwambia twende nikamuogesha vizuri saa nane usiku hiyo tukalala, akaniambia nikumbatie tukakumbatiana tukashikana mikono tukapitiwa na usingizi wote." Mrisho Mpoto akizungumzia kifo cha mkewe kilichotokea Julai 15, 2025.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…