Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,195
- 10,709
Msanii maarufu Mrisho Mpoto amepoteza mke wake kipenzi — msiba unaogusa moyo wa kila mwenye utu. Lakini mitandaoni, baadhi ya watu wameonekana wakifurahia, wakitoa maneno ya kejeli badala ya pole. Hili linaonesha kuwa jamii yetu inazidi kupoteza huruma, haiba na utu wa kawaida.
Tumefika wapi kama taifa hadi kufurahia maumivu ya wengine? Huruma na utu ndivyo vilivyotufanya tuwe jamii yenye mshikamano, si chuki.
Ni wakati wa kujitazama upya. Kama hatuwezi kusema pole, basi ni bora tukae kimya. Maumivu ya msiba hayawezi kufutwa, lakini moyo wa faraja huweza kuponya. Lakini pia hii iww fursa ya Mrisho Mpoto kujitazama upya na kufikiria haswa kwanini watanzania wamekuwa hivi?
Pole sana Mrisho Mpoto. Tanzania yenye utu bado ipo na ukubali kuungana na watanzania wa hali ya chini — Bi Mariamu apumzike mahala pema.