Mke wa mchuchu yuko busy kunitafutia mume - imekaaje hii

Hayo ya Mr Mhina ni ya mpito na hakuna litakaloongeza, 5 years you're kimada na u will continue to be one...Nenda kamwone Pedro kama anafaa mbwage Mhina, kama alikupenda kweli ataziba mdogo maana yeye pia anahusika coz amecheat kwa mkewe.

Zungumza na Mr Mhina kiutuuzima zaidi kama inabidi ustaafu kwenye chama hichi cha Kimada Forever.
 
Kuhusu mume wa mtu wasikutishe hao kuna wanawake wenzio wanakubali kuolewa na mwanaume mwenye wake wa tatu na yeye anakuwa wa 4 itakuwa na wewe unajilia kisiri na unaheshimu ndoa yake?
 
  • Thanks
Reactions: Sal
hanijui, simjui. tumekutana bahati mbaya kwenye salon ya mke wa boss wa mume wake. ndio salon niendayo na mchuchu alishaniambia kua kuna siku nitakutana na mkewe maana ndio salon yake nae.
siku isokua na jina ikafika. mama mwenye salon nimemzoea na tunaongea sana maana mimi ni mteja wake mzuri. nimekwenda kama kawaida yetu saa nyingine unaweza kushinda salon maana mambo mengi, kuanzia makucha, nyuso, nywele, vyote hivi mpaka uvimalize ni siku nzima. mke wa mchuchu kaingia. mimi simfahamu nae hanifahamu, mama mwenye salon kampokea, karibu mama mhina (sio jina lake) nikashtuka maana jina mhina jina la mchuchu wangu.
vile tumezoeana, mama mwenye salon katoa intro. kutana na mteja wangu mzuri sana Ms. Baltazar (not my real name), tukashikana mikono, michapo ikaanza. wote tuko around the same age. wao wameoelewa, ila mimi niko single lakini niko na Mr. Mhina kama mfadhili wangu mjini. maongezi ya masaa, tuko salon na vi wine tukaanza kunywa. kidogo Mrs. Mhina "jamani Ms Baltazar nimekuona leo tu lakini nimependa sana company yako. unaonaje tukionana tena siku nyingine for a drink. Naomba namba yako ya simu" nikataka kukataa nimpe ya uongo lakini nikahisi asije akasema ngoja nikubipu u-save yangu, kama tulivyo waswahili. ikabidi nimpe namba. miezi kadhaa ikapita, hakunipigia. muwewe wala sikumwambia, niliuchuna maana asije akadhani nilijishaua nijulikane japo ananijua sina hizo. siku nyingine tutakutana tena. ni salon yake na mimi pia ni yangu. "shoga jamani za siku nyingi, hujanitafuta?" nikamwambia nilidhani utanitafuta wewe. basi tukaongea michapo ya kimama maana wote matured ladies.
Katika maongezi mama mhina akachomekea, "jamani tuna family friend wetu, very matured guy, aliachana na mkewe some years back, anatafuta mke, jamani naomba nikuunganishe. yaani anataka mtu kama wewe"
Toba!, nikapigwa na butwaa. mama mwenye salon nae anaongezea, si kwa ajili ya Petro? anamjibu ndio. kwa kweli wata match. wana supotiana wenyewe, mie nacheka usoni lakini moyoni niko hoi.
hiyo sasa ilibidi mchuchu nimwambie kua mkeo nimekutana nae na yuko mbioni kuniunganisha na Petro. Huyo Petro nishamsikia sana mdomoni mwa mchuchu lakini simfahamu. mchuchu ananijibu, "mke wangu kaniambia amekutana na mwanamke mwema sana salon angependa tumkutanishe na Petro, ila sikujua kama ni wewe la azizi wangu"
Sasa wana JF naomba mnipe ushauri, Mr & Mrs Mhina wameandaa lunch siku ya pasaka maana pia wana kitu cha kifamilia kinakumbukwa, na ndio siku pia Mrs. Mhina anasema lazima niende nikakutane na Petro.
Petro keshanisikia sana jina langu kwa mchuchu, according to him, lakini hatujuani. Mimi sitaki hata kupeleka uso wangu huko kwao, ila mchuchu anadai eti inabidi anitambulishe kwa Petro mapema ili tujuane kabisa kua mashemeji hata kwenye easter tukionana iwe danganya toto. hapa ninapoandika Mrs. Mhina, ni kila siku napigiwa simu, ili mradi sina pa kukwepea. Natamani niumwe.
Mimi na mchuchu hatutaki kuachana. tuna miaka mitano pamoja sasa. mahusiano ya ki utu uzima.
(Imemkuta rafiki, naomba tumshauri) Akale pasaka, au aitolee nje? kama nikutoa nje, mpeni ushauri how?

Ni mchuchu wa haja nini? Ukikubali ushaengeza watu wa kukuchunga katika hizo nyendo zako na mchumchu wako. Sasa unamwibia mmoja ukiunganishwa na Petro utakuwa unawaibia wawili, hiyo kazi sasa, wenye mali wawili kuwapiga chenga ni kazi kweli!
 
99.9% ya wanaume wa bongo wana nyumba ndogo na 85% ya wanawake ni nyumba ndogo za wanaume, you are among them. toa ushauri acha kujifanya mtakatifu wakati sio.


Kwa nilivyokuanalyse inaonesha we age imekwenda kidogo(si sana usiogope)..

Haya faida unazopata:
company ya 'mchuchu'(what is mchuchu anyway?),
pesa(yani mke mtu angejua mumewe ndo anagharamikia uwepo wenu wawili hapo saloon!),
usafiri(labda)

Hasara:
-Only a matter of time before tindikali meets your reception
-You will grow old lonely
-Your dignity kwa jamii inagaragara kwenye vumbi as we speak
-God hates your, parents hates you, rafiki zako wanaspeak behind your back(kwa kifupi u have a whole bunch of people hating you. Rafiki zako wenyewe wanakuogopa manake ww mtaalamu wa kuruka na visivyo vyako).
-Wewe ni adui wa jamii coz pesa jamaa angetakiwa awape gud education watoto wake ili waikomboe nchi hii unakula wewe bila aibu..(We are Jamii forum by the way so to us Jamii comes first)

Question:
How do you go to sleep at night?
 
mi nakushauri piga chini Mr. mhina! .... anza life na petro!
 
Kumbe small house kibabu unaweza kuiita mchuchu eh? Asante kwa kuniongezea maujuzi.
Mjini kugumu sana,kha!
 
Kuhusu mume wa mtu wasikutishe hao kuna wanawake wenzio wanakubali kuolewa na mwanaume mwenye wake wa tatu na yeye anakuwa wa 4 itakuwa na wewe unajilia kisiri na unaheshimu ndoa yake?

Ushauri wako ni sawa na nguvu za giza, rudi kuzimu chini ya bahari iwe agent wa shetani.
 
nenda kutana na petro,kama he is your type then mkubalie.mr mchuchu anawaste your tyme for a matter of passing lust.mh
 
99.9% ya wanaume wa bongo wana nyumba ndogo na 85% ya wanawake ni nyumba ndogo za wanaume, you are among them. toa ushauri acha kujifanya mtakatifu wakati sio.

Pengine ni kati ya hao wachache waadilifu. Lakini hata asipokuwa muadilifu - si vibaya kutoa ushauri mzuri.
 
naamini unaelewa utendalo japo katika hali ya kawaida ni vyema ukawa a chako kuliko kutegemea cha mwingine japo inaonyesha msimamo wako ni kula cha mtu
 
heee ni wewe bana acha kutuzuga, mi naona mchukue huyo petro, sababu kila kitu mungu kampangia mtu daraja la kufikia palipokusudiwa,hao wote kina mchuchu na mkewe ndio walipangwa na Mungu labda ili ukutane na mumeo, chukua hiyo nafasi bwana mengine yatajiseti yenyewe
 
Kumbe ndio MABUZI yanavoitwa siku hizi i.e. MCHUCHU. Mwambie huyo rafiki yako kuwa huyo mke wa BUZI lake keshamshtukia. Tena inaonekana kamshtukia siku nyingi na hata huyo bibiye mwingine wa salon ana habari zote. Mwambie hata ile introduction aliyofanyiwa kwa mwenye BUZI haikuwa coincedence bali ilipangwa na mwenye BUZI na mwajiriwa wao. Kwa leo yangu ndiyo hayo tu.
 
99.9% ya wanaume wa bongo wana nyumba ndogo na 85% ya wanawake ni nyumba ndogo za wanaume, you are among them. toa ushauri acha kujifanya mtakatifu wakati sio.

Kumbe tusiokuwa na nyumba ndogo tupo wachache hivyo yaani asilimia 0.1 sikujua kabisa.
 
yaelekea ulizaliwa ili uwe nyumba ndogo (kidampa). Kwa hiyo endelea na profesheni yako. Usijidanganye kwamba utaweza kuwa mke wa ndoa wa mtu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom