Mke wa mchuchu yuko busy kunitafutia mume - imekaaje hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wa mchuchu yuko busy kunitafutia mume - imekaaje hii

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sal, Mar 23, 2012.

 1. Sal

  Sal JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  hanijui, simjui. tumekutana bahati mbaya kwenye salon ya mke wa boss wa mume wake. ndio salon niendayo na mchuchu alishaniambia kua kuna siku nitakutana na mkewe maana ndio salon yake nae.
  siku isokua na jina ikafika. mama mwenye salon nimemzoea na tunaongea sana maana mimi ni mteja wake mzuri. nimekwenda kama kawaida yetu saa nyingine unaweza kushinda salon maana mambo mengi, kuanzia makucha, nyuso, nywele, vyote hivi mpaka uvimalize ni siku nzima. mke wa mchuchu kaingia. mimi simfahamu nae hanifahamu, mama mwenye salon kampokea, karibu mama mhina (sio jina lake) nikashtuka maana jina mhina jina la mchuchu wangu.
  vile tumezoeana, mama mwenye salon katoa intro. kutana na mteja wangu mzuri sana Ms. Baltazar (not my real name), tukashikana mikono, michapo ikaanza. wote tuko around the same age. wao wameoelewa, ila mimi niko single lakini niko na Mr. Mhina kama mfadhili wangu mjini. maongezi ya masaa, tuko salon na vi wine tukaanza kunywa. kidogo Mrs. Mhina "jamani Ms Baltazar nimekuona leo tu lakini nimependa sana company yako. unaonaje tukionana tena siku nyingine for a drink. Naomba namba yako ya simu" nikataka kukataa nimpe ya uongo lakini nikahisi asije akasema ngoja nikubipu u-save yangu, kama tulivyo waswahili. ikabidi nimpe namba. miezi kadhaa ikapita, hakunipigia. muwewe wala sikumwambia, niliuchuna maana asije akadhani nilijishaua nijulikane japo ananijua sina hizo. siku nyingine tutakutana tena. ni salon yake na mimi pia ni yangu. "shoga jamani za siku nyingi, hujanitafuta?" nikamwambia nilidhani utanitafuta wewe. basi tukaongea michapo ya kimama maana wote matured ladies.
  Katika maongezi mama mhina akachomekea, "jamani tuna family friend wetu, very matured guy, aliachana na mkewe some years back, anatafuta mke, jamani naomba nikuunganishe. yaani anataka mtu kama wewe"
  Toba!, nikapigwa na butwaa. mama mwenye salon nae anaongezea, si kwa ajili ya Petro? anamjibu ndio. kwa kweli wata match. wana supotiana wenyewe, mie nacheka usoni lakini moyoni niko hoi.
  hiyo sasa ilibidi mchuchu nimwambie kua mkeo nimekutana nae na yuko mbioni kuniunganisha na Petro. Huyo Petro nishamsikia sana mdomoni mwa mchuchu lakini simfahamu. mchuchu ananijibu, "mke wangu kaniambia amekutana na mwanamke mwema sana salon angependa tumkutanishe na Petro, ila sikujua kama ni wewe la azizi wangu"
  Sasa wana JF naomba mnipe ushauri, Mr & Mrs Mhina wameandaa lunch siku ya pasaka maana pia wana kitu cha kifamilia kinakumbukwa, na ndio siku pia Mrs. Mhina anasema lazima niende nikakutane na Petro.
  Petro keshanisikia sana jina langu kwa mchuchu, according to him, lakini hatujuani. Mimi sitaki hata kupeleka uso wangu huko kwao, ila mchuchu anadai eti inabidi anitambulishe kwa Petro mapema ili tujuane kabisa kua mashemeji hata kwenye easter tukionana iwe danganya toto. hapa ninapoandika Mrs. Mhina, ni kila siku napigiwa simu, ili mradi sina pa kukwepea. Natamani niumwe.
  Mimi na mchuchu hatutaki kuachana. tuna miaka mitano pamoja sasa. mahusiano ya ki utu uzima.
  (Imemkuta rafiki, naomba tumshauri) Akale pasaka, au aitolee nje? kama nikutoa nje, mpeni ushauri how?
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  mwambie mrs mhina kamshtukia kuwa anatembea na mume wake, na anampeleka kwa peter makusudi ili ajitulize na wakwake badala ya kung'ang'ania vya wenzake..........

  Aende tu kwenye mlo pasaka akutane na peter ......
   
 3. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wewe au rafiki. Acha mume wa mtu. Mtafute wako, tulia kwanza kama petro ni wako atakuja muda muafaka. Kama mumeo akiibiwa utapenda?
   
 4. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  ONYO: MME/MKE wa mwenzio ni sumu....
  here we go now,aende akaonane na petro kama atampenda aachane na mme wa mtu awe wa petro.....over.
   
 5. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mume wa mtu ni sumu dada tafuta wako
   
 6. Sal

  Sal JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Petro ni best friend wa mhina, haiwezekani hiyo. mume wa mtu ni sumu kwa watu kuongea tu lakini vitendo huwa hakuna.

   
 7. Sal

  Sal JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  waume zetu wanaibiwa kutwa lakini bado tupo nao. huyo shoga sio wa kwanza na sio wa mwisho kuiba mume wa mtu anaendeleza walio anza

   
 8. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  achana nao wote,subiri wa kwako mkuu,vya watu ni hatari atii....
   
 9. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mke wa mchuchu wako ameshagundua uhusiano wako na mumewe. Anachokifanya ni ustaarabu wa kuvunja uhusiano wenu sasa wewe ukiwa mbishi kinachofuatia ni kuharibu hiyo reception yako kwa tindikali then tuone kama mchuchu ataendelea nawe! you have been warned, chukua tahadhari!!!
   
 10. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  jf ni zaidi ya uijuavyo......ngoja niendelee kupiga chabo....
   
 11. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Jaribu kujiweka upande wa mwenzio..kwamba wewe ndio ungekuwa unafanyiwa hivyo ungejisikiaje? Ukipata jibu lake then tafakari alafu chukua hatua...
   
 12. effector

  effector New Member

  #12
  Mar 23, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mwaego vizuri kula na wenzio. Mbona wao wanakula wake za wenzao na wake zao wanaliwa na waume wenzao. Hayo maneno tu. Pasaka kaile ikiwezekana na petro kama atakufaa fresh wajoin tu.
   
 13. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Watu wabayana waume zawatu, kwani hamtafuti wenuuu?
   
 14. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  chuchu sound .
   
 15. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  wee Sal wewe....hapa umenimaliza kabisa.....
   
 16. vanmedy

  vanmedy JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 2,245
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Umeng'ang'ania "mchuchu mchuchu"
  DEFINE MCHUCHU?_____________
   
 17. m

  mzawahalisi JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  hureee!watch the reality show.
   
 18. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Kwa nilivyokuanalyse inaonesha we age imekwenda kidogo(si sana usiogope)..

  Haya faida unazopata:
  company ya 'mchuchu'(what is mchuchu anyway?),
  pesa(yani mke mtu angejua mumewe ndo anagharamikia uwepo wenu wawili hapo saloon!),
  usafiri(labda)

  Hasara:
  -Only a matter of time before tindikali meets your reception
  -You will grow old lonely
  -Your dignity kwa jamii inagaragara kwenye vumbi as we speak
  -God hates your, parents hates you, rafiki zako wanaspeak behind your back(kwa kifupi u have a whole bunch of people hating you. Rafiki zako wenyewe wanakuogopa manake ww mtaalamu wa kuruka na visivyo vyako).
  -Wewe ni adui wa jamii coz pesa jamaa angetakiwa awape gud education watoto wake ili waikomboe nchi hii unakula wewe bila aibu..(We are Jamii forum by the way so to us Jamii comes first)

  Question:
  How do you go to sleep at night?
   
 19. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  kumbe mume wa mtu mtamu eeh.. but sal kasema rafiki yake ndiyo mwenye hilo tatizo, mbona mnamkomalia yeye sasa?
   
 20. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Mi ningekushauri kwanza jitahidi kupunguza mawasiliano na huyo mke wa hawara yako, potezea kabisa. Na pili fanya kila mbinu usiende nyumbani kwake, usiende kabisa.

  Ku-intertain mawasiliano na huyo dada wakati unanijua wewe ni nyoka kwake ni ufedhuli uliopitiliza kabisa.

  Na mwisho achana na mume wa mtu ili Mungu akupe wa kwako.
   
Loading...