dizzle kiraka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2012
- 416
- 118
Peleka bongo movie hiyo story
Mama amechanganyikiwa anataka atoe hii siri kwa watu wa jirani na mumewe, shoga yake ambaye ni mke wangu akaniomba ushauri, nami nawaomba wana JF ushauri wenu ili tuiokoe hii ndoa maana akisema tu lazima talaka itanuka tu.
Nilishaisoma hii kule kwenye jukwaa la utani. Sitoi ushauri wowote.
Mke wa boss mmoja bahili amejikuta akiliwa uroda na kijana mahili wa mipango (Mtoto wa mjini) bila kulipwa hata senti moja. Hii imetokea karibu na sikukuu ya X-Mass ya 2012.
Kijana huyo alikuwa akimtokea huyo mke wa bosi siku nyingi lakini alikuwa akipigwa chini kwa sababu mwanamke huyo alikuwa na dharau sana na kumuona kijana huyo kama takataka fulani. Kijana wa mujini aliumiza akili akaja na mpango mkali wa kumng'oa mama huyo kama ifuatavyo:
- Kwanza alitumia mbinu ya kumzoa yule boss na akafanikiwa kuwa naye jirani sana.
- Akaomba mkopo kwa yule boss mpenda misifa, bila ajizi akapewa Sh. 3Million.
Katika kipindi cha urafiki wake na yule boss, aligundua kuwa boss na mkewe hawakuwa vizuri kutokana na tabia ya bosi kutothamini ndugu wa mke wake. Kwa kuwa X-Mass ilikuwa inakaribia, na ofisi ya mke wa bosi haikuwa na uwezo wa kulipa mshahara kabla ya sikukuu, mama alichanganyikiwa, alikosa jinsi ya kukidhi mahitaji ya ndugu zake hasa wakati ule wa sikukuu.
Mtoto wa mujini kwa kulijua hilo, alianza kumtokea tena yule mama, msimamo wake ulikuwa kama kawaida akagoma. Yule kijana akamwambia mama nikubalie mimi nina Sh.3M, nitakupa kwa kazi ya leo tu. Yule mama akakumbuka hitajio la pesa alilonalo, akaamua kukubali shingo upande.
Kijana akala ule mzigo na akampatia ile Sh.3m. Wakati mama akiwa njiani, mtoto wa mujini akampigia yule boss na kumshukuru kwa mkopo wa ile Sh.3M, akamwambia kuwa leo amelipa na amempatia mkewe amletee nyumbani.
Mama alipofika nyumbani tu, mzee akamwambia nipe ile sh.3M tatu uliyopewa na yule kijana, mama alichanganyikiwa alijuaje yule mzee, siri ime leak, yule mama akajiuliza akakosa jibu. Ilibidi atoe zile pesa ampatie mumewe na deni la msela likaisha huku akiwa amekula mzigo bureee.
Mama amechanganyikiwa anataka atoe hii siri kwa watu wa jirani na mumewe, shoga yake ambaye ni mke wangu akaniomba ushauri, nami nawaomba wana JF ushauri wenu ili tuiokoe hii ndoa maana akisema tu lazima talaka itanuka tu.