Mwanaume anaweza kuona hamna masimango kumbe mwanamke anayaona masimango na dharau za kutosha ila anavumilia tu vile hana hela. Sasa akizikosa mwanamke anaona hana cha kuvumilia tena ndio dharau zinaanza.
Unajua masimango sio lazima amsimangie zile hela anazompa. Bali kufanya vitu vinavyomkera mwenzako kisa unajua hana cha kufanya na hata akitaka kuondoka hana pa kuanzia kwa hiyo lazima avumilie.
Ishini na wake zenu vizuri. Sisi tunavumilia sana na kuonesha kila kitu kipo sana na kumbe hamna kilicho sawa. Na tupo vizuri sana kwenye kutunza kumbukumbu zetu.