Kumbe kuna jambo ambalo watu wengi hawalijui katika maisha yao ya kila siku. Baba na mama ni kweli wana umuhimu kuwepo katika maisha yaani kuwa hai na kuendelea kuwaona na hata kuwatumia kwa ushauri wakati mwingine pale utakapohitaji kulingana na kula kwao chumvi nyingi katika maisha. Lakini ukija katika umuhimu wa mke au mume kwa mwenzie katika AGANO au ndoa ni mkubwa na aufananishwi na chochote.
Narudia umuhimu wa mke kwa mume ni mkubwa na umuhimu wa mume kwa mke ni mkubwa, na ndiyo maana imeandikwa katika vitabu vya neno la MUNGU kuwa mke atamuacha baba yake na mama yake na kuambatana na mumewe vivyo hivyo na mume ataachana na mama yake na baba yake na kuambatana na mkewe , Mwanzo 1:26-29, na Efeso 5:21-32 na 1Korinto 7:1mpaka mwisho na Zaburi 45 :10-12-imeandikwa, sikia, binti , utazame, utege sijui lako, uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako.
Naye mfalme(mume)atautamani uzuri wako, maana ndiye bwana wako,nawe umsujudie.
Sasa basi ufahamu kuwa hata wazazi wako walikuwa na wazazi nao waliachwa wawe na maisha yao ya ndoa na ndiyo ukamilifu wa hilo agano, na siyo tena una mume alafu eti mama ndiyo muhimu kuliko mume au mke hata hiyo ndoa haitadumu hata siku moja, na haitakuwa na maana ya kuoa au kuolewa kwa mujibu wa MUNGU anayeishi.
Pia kibinadamu itakuwa haina maana ya kufanya hata hiyo send off kwa mwanamke!
Turudi kwenye neno tusitumie akili zetu tu!