EXTERMINATOR
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 343
- 90
Habari wanajf. Mimi nimeoa na tuna watoto wawili ila mke wangu ni mkorofi sana mpaka nafikia hali ya kuwaza ameingiwa na nini. Yaani yeye anataka awe ndio muamuzi wa kila jambo ndani ya nyumba na ukiweka idea yako anaona eti una mdharau mnataka kwenda out basi time yake ndio ifuatwe na sio yako. Na Ikitokea mabishano ya hoja na kuona anashindwa basi atavunja kila kitu km TV, pasi, deck au hata simu anairusha ukutani na kuvunjika kwa hasira. Baada ya siku anasema tununue vitu vilivyoharibika. Sasa mm naona kama ni ukichaa huu, jamani wenye mawazo au maoni naombeni kwani nafikilia mambo mengi sana ya hii ndoa
Asante Kwa Uzi mkuu tuko wengi tunafuatilia maushauri..Habari wanajf. Mimi nimeoa na tuna watoto wawili ila mke wangu ni mkorofi sana mpaka nafikia hali ya kuwaza ameingiwa na nini. Yaani yeye anataka awe ndio muamuzi wa kila jambo ndani ya nyumba na ukiweka idea yako anaona eti una mdharau mnataka kwenda out basi time yake ndio ifuatwe na sio yako. Na Ikitokea mabishano ya hoja na kuona anashindwa basi atavunja kila kitu km TV, pasi, deck au hata simu anairusha ukutani na kuvunjika kwa hasira. Baada ya siku anasema tununue vitu vilivyoharibika. Sasa mm naona kama ni ukichaa huu, jamani wenye mawazo au maoni naombeni kwani nafikilia mambo mengi sana ya hii ndoa
Kuna siku atavunjia pasi usoni kwako. Weka mguu chini, hasa kwenye kuvunja vitu. Ukimfuga na hiyo tabia utajuta maisha yote. Kha! Na umpeleke.muhimbili kwanza akatibiwe wazimu, mkitoka hapo pitiliza church.
unaishije na mwanamke anatukana matusi? Na watoto wenu bado hawajaanza kutukana? Na ujue wanajifunza na kuvunja vitu. Siku utasema hakuna kwenda school trip mikumi, watasema na tv!
akishavunja vitu na wewe unanunua? Khaaa
Asante Kwa Uzi mkuu tuko wengi tunafuatilia maushauri..
Binafsi napenda mwanamke kama huyo, yaani wanakua na feelings ambazo ni very intense. Pole lakini kwa kukereka/
Wewe pamoja na mkeo mtakuwa mna ukichaa wa aina tofauti
Na kanisani anaenda sana kusali..na tunaenda wote pia..ila anatukana sana matusi utafikili nn sijui.
watoto wanasense kubwa sana. Na tv anaendaga kuvunjia chumbani? Kwanza hamruhusiwi kugombana wala kurushiana maneno mbele hata ya hausigelo, achia mbali watoto! Hamna ushauri hapo, tough love inahusika. Mkalishe chini, fikia makubaliano hakuna moja mbili tatu, na ikitokea nitafanya moja mbili tatu. Na hakikisha akifanya na wewe unatimiza kweli. Dawa ya jeuri ni kiburi banaa, ebo! Kuwa mwanaume basi!Najitahidi sana wasione yanayotokea ila km huyu mdogo akikasirika na yy anarusha toys zake au kujirusha chini. Sasa nasema sijui karithi tu tabia au ni kitu ambacho amewahi kuona.
Niko na wewe hapo mkwaruzano kwenye ndoa lazima uwepo.Unajua kuishi na mtu lazima kutakua na mikwaruzano ya hapa na pale lkn kusema mm ndio nimesababisha hivyo hapana. Ila kuna wakati naona inakua km vicious
cycle kwani akifanya hivyo na mm naweza ku-react vyovyote vile. Ila nakumbuka ili kupunguza hayo ma-stress naweza kuanza chatting na beer..
Na kanisani anaenda sana kusali..na tunaenda wote pia..ila anatukana sana matusi utafikili nn sijui.