Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,998
- 135,207
Wakuu, hii mada imekuwa inspired na
Kuna sababu nyingi za wamama walioko ndani ya ndoa zao, kujiiba nje na kuleta mtoto wa nje ndani ya ndoa, kunakuitwa kubambikiwa, au hata kubambikiwa tuu mimba ni kisha kusingiziwa mtoto.
Kwa hiyo mke kupta mimba ya nje akiwa ndani ya ndoa, sio lazima iwe ni majanga, sometimes ni blessings!. Ila pia jamii zetu zimegubikwa sana na mfumo dume!. Sisi wanaume kila siku tunazaa nje ya ndoa and its usually not a big deal!.
Lets be fair kwa wake zetu!.
Thanks.
Pasco
Mkuu The Boss, kwanza asante kwa hili la "sixth sense". Hapa siizungumzii bali naanza na mazingira ya mke kupata mtoto nje ya ndoa!.Ndo maana nikasema sio kila mwanaume
wapo wanaoibiwa hawajui but wengine huwa wana kama sixth sense hivi
au strong connection.....labda Pasco aje atusaidie.....
Kuna sababu nyingi za wamama walioko ndani ya ndoa zao, kujiiba nje na kuleta mtoto wa nje ndani ya ndoa, kunakuitwa kubambikiwa, au hata kubambikiwa tuu mimba ni kisha kusingiziwa mtoto.
- Sababu kuu ya kwanza ambayo ndio maarufu zaidi ni kwa Wachagga wa zamani, wana kitu kinaitwa "curse" laana!. Ikitokea mkalaaniwa kizazi chote cha mfano cha Mkuu The Boss, ikitokea mkakorofishana na mtu (people with powers) akakulaani, then uko wako wote mnakuwa wiped out, one after the other within a specific period of time, mwisho wa siku, wore mtakwisha and there will be no trace ya jina la The Boss,at a survive!, kwa kulijua hili, wamama wa Kichagga wa enzi hizo, walikuwa wanafundishwa jinsi ya kuiba, na huyo unae iba nae unamchagua mtu anae fanania fanania na mmeo, ili dili isistukiwe!. Mwenye mtoto kamwe haambiwi, and no one will know zaidi ya mama, mara nyingi hutokea huyo mtoto aliyeibiwa kuja kuwa odd man out, au very bright, au kuwa na tabia za ajabu tofauti na wengine wote!. This was usually done in good faith!.
- Wizi wa pili ni pale Baba ana tatizo, hawezi kutengeneza watoto!, zamani ikiamini ugumba ni tatizo la mwanamke tuu, na kikawaida wanaume huwa hawapimi!. Mke kaolewa miaka inapita hashiki ujauzoto, anayelaumiwa, kunyooshewa vidole, kunyanyaswa na kusimangwa na mke! huku akitukanwa "mgumba" kazi yake ni kujaza tuu choo!. Mke anapimwa anaambiwa yuko normal, kumshauri mume akapime anaogopa kwa vile ugumba ni tatizo la mwanamke tuu!. Kitakachotokea kwenye familia hii, mume ataanza kuwa rude na kucheza rafu za wazi kusaka mtoto nje!. Hivyo anakuwa mipiga nje mzuri huku mke akivumilia kusubiria kuletewa watoto wa nje kulea!. Hili lisipotokea, mke au kwa kushauri na watu wa upande wake, au kwa her own initiatives, naye ataanza majaribio ya nje kwa siri, akinasa tuu, ataonyesha mapenzi ya ajabu kwa mumewe hata kama mume hataki tena game, atalazimishwa kisha mke atampa taarifa mume kuwa ameshika!. Itakuwa ni furaha kuu nyumbani, mume atafurahi na ndoa itashine!. In this case the "dume la mbegu huwa lina taarifa ni nini kilikuwa kinatafutwa", na usually ataendelea kutoa mbegu kwa watoto wengine wote wa huyo mhusika!. Kuna familia nyingine mume anapina na kujikuta hawezi kutengeneza watoto, ili kuepuka aibu ya hawezi, anamuweka mkewe kwenye very compromised situations za kupigwa nje ili siri isifichuke!, au koo serious wadogo mtu au kaka mtu wanashauriwa kumsaidia ndugu yao ili kumfichia siri na kuepuka aibu ya ukoo. Hapa mume atajua watoto sio wake ila atawapenda tuu kiunyonge unyonge!.
- Mimba za tatu za nje ya ndoa ni zile za michepuko tuu, usually hizi ni au za bahati mbaya au za makusudi!. Hapa ni pale kiukweli wanaume wengi wa kibongo, ni very insensitive kwa mahitaji ya wake zao, hivyo mnamkuta mke tangu ameolewa hajawahi kufikishwa ndani ya ndoa yake!. Mume akishafika tuu ndio mwisho wa shughuli!. Siku ke akichepuka na kukutana na mafundi akafikishwa!, then frrom time to time, bingwa atapelekewa!, "secret lover concept!". Ni katika kuridhishana huko, mtoto wa nje atatengenezeka na baba wa nyumbani kubambikiwa, au kuna wanawake wengine as a sight ya appreciation kufikishwa, anadhamiria kabisa, kumzawadia mtoto huyo lover wake ili ku intensify the bond!, ambao in this case lover anaelezwa ila mume ndio anafanywa zoba!.
- Aina ya nne, ni mke anapobakwa nje na kushika ujauzito, hawezo kusema.
- Koo za wake wengi kama za Kisukuma wa zamani, mtu wake 20!, hawezi kuwa service wote, hivyo wake wengine kujikuta wanalazimika kwenda nje kukidhi haja na huko ndiko watoto wa nje hupatikana na kuwaleta ndani, na kikawaida Wasukuma ndio kabila linaloongoza kwa upendo kwa wanawake na watoto!, hata kama unajua fika huyu sii damu yako, sisi tunapenda tuu!. Mimi mwenyewe hapa nilipo nina watoto 7!, miongoni mwao mimi mweusi, wife (1) mweusi, miongoni mwa watoto wetu kuna "cheupe!" ni kibinti, kizuri na ndio kipenzi cha baba!.
- Kwa familia za wafugaji, waume wanapokuwa malishoni kipindi cha ukame, huweza kukaa hukohata miaka miwili na kuwaacha wake zao nyumbani, wakirudi, wanakuta watoto na ni "watoto wao!".
Kwa hiyo mke kupta mimba ya nje akiwa ndani ya ndoa, sio lazima iwe ni majanga, sometimes ni blessings!. Ila pia jamii zetu zimegubikwa sana na mfumo dume!. Sisi wanaume kila siku tunazaa nje ya ndoa and its usually not a big deal!.
Lets be fair kwa wake zetu!.
Thanks.
Pasco