Mke kazidi mizaha

Mke kazidi mizaha

Shida inaanzia hapo wewe kutompiga japovibao kadhaa. Kuna watu mpaka nguvu itumike ndio wanaelewa. Mwanamke kuna muda mwenyewe anamiss kupigwa, usimnyime kibao mke wako
Sasa hapo apigwe kisa nini?
Acheni udikteta kama wa Samia.
 
Mbona kawaida tu mkuu hyo shida nini sasa.
 
Nawasalimu.

Mnisamehe kwa kutokuwa mwandishi mzuri.

Moja kwa moja kwenye hoja ya msingi.

Nimeishi kwenye ndoa na huyu mke wangu kwa miaka 10 na kujaliwa watoto wawili.

Kilichonifanya nije hapa kuomba msaada wa mawazo ni hili tatizo la midhaha ya huyu mke wangu, amekuwa mtu wa kujibu au kuongea bila ya kuweka mipaka ( kutenganisha kipi Cha kuongea na mpenzi na kipi Cha kuzungumza na mume ambaye ni mkuu wa kaya).

Ni kili ya kuwa katika maisha yetu yote nilishawahi mchapa makofi mara 3 kitu ambacho sitaki kukikumbuka na sitaki kitokee tena, ila nilifanya vile Ili tuu aweze kutambua kuwa sipendezwi na tabia zake.

Tabia hiyo ya kutokuwa na mipaka hasa ya kuzungumza haijawahi kwisha zaidi ya kupungua kwa muda na baadae kuanza tena.

Nimewahi kutumia kanuni ya kumtoa out na kwenda naye sehemu ya faragha na kumuambia kuhusu kutopendezwa na tabia zake huwa anaomba msamaha lakini baada ya muda hurudia tena.

Kiukweri ninampenda sana mke wangu, na mahusiano yetu yalianza tangu tukiwa secondary na baadae kuja kuoana.

Nje ya kumkanya mara kwa mara, niliona ni busara kufikisha jambo hili kwao, Ili waweze kumkanya binti yao, ila sikuona mabadariko yoyote yale.

Yote yaliyotendeka niliweza kuvumilia ila hili nililolipata wiki hii, limenizidi uwezo. Baada ya chakula Cha jioni tukaingia chumbani, alikuwa anapanga nguo Mimi nikatangulia kuoga, baada ya muda nikatoka yeye akiwa Bado busy, kama kawaida kabla ya kulala ni kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake wa siku, nikasikia akiseme acha kusali uongo.

Niliumia sana, nikamaaliza sala na kumuuliza ulikuwa unamaana gani, nikaona anacheka, nikamuuliza hii midhaha yako itaisha lini lakini akawa anaendelea kucheka, kwa kweri nilipatwa na hasira sana ila niliishia kutoka kwenda barazani ningeendelea kuwa pale ningeweza kumpiga kitu ambacho sitaki kitokee tena.

Mimi nimemzidi miaka 4 huyu mke wangu , hata kielimu nimemzidi, kisalary nimemzidi zaidi ya mara 4. Nimeandika hivi Ili kutoa Ile dhana ya kuwa huenda nalelewa, nafanya majukumu yangu kama baba vizuri kabisa( ada, matibu, mavazi, afya, makazi) kwake na kwa watoto wetu.

Kutokana na hili huwa nakuwa na mawazo sana, kitu ambacho natamani kufanya maamuzi magumu ya kumwacha ila moyo unasita.

Ushauri wenu utaniponya.
Mbona ni Kama siku hio alikuwa "mhitaji", kwa ufupi siku hiyo alihitaji "fimbo ya Musa"
hio elimu unayosema unamzidi itumie zaidi kufanya upembuzi wa Mambo mkuu!

Samahani lkn Kama nimekukwaza!
 
Kama nimekuelewa vizur huyo mwanamke ana changamoto zake kadhaa...pamoja na kumtoa out kiume na kuongelea changamoto zenu faragha ...umesema anaomba msamaha kisha baadae anarudia tena.....umesema ameshaitwa kwao na kusemwa lkn bado Tu....naona chukulia huo ni kama udhaifu wake Tu.... Na hio wala sio sababu ya kumwacha huyo mkeo.

Ila hili la kuleta mdhaha ktk sala linasikitisha Sana na ulikuwa na haki ya kukasirika....huo sio utani Bali upumbavu ambao ameuonyesha mkeo.

Watu wamekusema Sana labda hujui utani na mambo kama hayo....lkn najua wewe ni mwanaume na sio mvulana....Kwa maana unajua huu sasa ni utani na huu ni mdhaha...siamini kama wewe ni mpumbavu kiasi kwamba ushindwe kujua utani na mdhaha....tatizo la mkeo ni kwamba Hana Busara hiyo ndio shida yake ndio maana analeta utani mpaka kwenye sala! Na Busara ni kuliweka jambo ktk mahala pake.....mkeo Hana Hilo.

Jitahidi kumuweka Sawa Kwa hekima Sana....Kwa mfano ukipita Mda Fulani Bila kukuletea mdhaha ebu mnunulie zawadi au mpe hela akajinunulie zawadi na mwambie kipenz huwa nafurahi Sana pale unapoacha mdhaha unanifanya nizidi kukupenda ebu kajinunulie chochote unachopenda.....jaribu kuangalia kama mbinu hii itafanya kazi.

Kuna utani na mdhaha....mdhaha sio utani unakera na ni kama dharau Fulani hivi.

Ila usifikirie kumuacha hata kidogo....hayo ni ya kawaida tofauti na usaliti
 
Kwenye mapenzi Amani na furaha viwepo. Utani na mizaha iwepo, tatizo lako unatumika elimu Yako mpaka nyumbani kwako kwahiyo mwenzako akiongea kitu unakipima kutokana na elimu yake ya makaratasi.

Happy mwenyeshida ni wewe mke Hana tatizo Tena anaonekana mtu peace Sana na anapenda kufanya uwe na furaha ila wewe Kila akifanya vituko ufurahi wewe unamuona kituko tu kisa diploma.

Kunaujinga jinga unafanya mtaani au nyumbani ambao mkeo hapendi na anaona kabisa kufumba macho kwako na kusali Kila ulalapo na uamkapo ni unafiki tu, badili mienendo Yako na jitahidi kuwa flexible.

Akizidi mtandike makofi kadhaa Ili kurestore memory na atambue nafasi Yako Kama mume na si mkuu wa kaya Kama ulivojitanabaisha, maana mkuu wa kaya anaweza kuwa mwanamke au hata mtoto.
Duuuh kwani we jamaa ni psychologist!
Umemaliza Kila kitu kaka
 
Utani wote sawa ila kwenye maombi/sala hapana hilo nakuunga mkono.
 
Mzaha hadi kwenye sala..hapana nakataaa.
Jamani tuwe wakweli
Hiyo ni mbaya zaidi.
Ila pia watu hawafanani
Kuna watu wako hivyo yaani ndobyo walivyo
Wewe hapo unatamani ungekua na mwanamke siriaz flan hivi
Ila mpaka mnaoana hukuona hayo yote?au alikua anaficha?
Sawa ushamuoa na hilo jambo unaona linakukera mpaka mwisho
Ongea nae tu kila mara maana ndo mshaoana tena.hamna namna.
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Mzibue vibao vi tatu akizinduka hapo badae atajua mda WA matani na muda WA seriously
 
nadikitika kwamba hujielewi na ukijidanganya kumuacha wajuba tunaruka nae kama mwanaume umefika umri wa miaka kumi kw ndoa unataka nn kama sio mkeo kua peace na mwenye masihara unataka akuwekee gubu utaweza kuish nae acha ufakeni mleta mada
 
Miaka kumi hujamwelewa tu mwenzio, au labda kama neno mzaha limetumika vibaya!! Labda kama ana majibu mabaya mrekebishane au pia mkuu huenda uko serious sana !! Kila muda unawaza pesa na kazi !! Wakati mwenzako hiyo ndo njia ya kukusemesha ! Pengine pia akikutania ukanuna kidogo ndo anapenda. Na vipi yeye ukimfanyia mzaha anachukuliaje ?

Mimi pia napenda za utani (usio na madhara) , hata ikitokea sijamtania mwenzangu anaona kama siko sawa !! Atauliza mara mbili mbili kuna shida gani ?
Utani napenda sana, ila mizaha ndio tatizo lilop.

Unaweza ukamwambia jambo afu yeye akafanga mizaha hadi ukaona uache tuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom