Mke kazidi mizaha

Mke kazidi mizaha

Hapana hichi alichokisema jamaa nasapoti kabisa. Kwakweli mizaha hata matani yasizidi. Mfano, mimi ninatakiwa kusafiri kuna kazi Dar nahitaji kuimaliza hivyo bibie akasema anakuja leo kutoka Arusha kuja Mwanza ila asubuhi namuuliza ushapanda gari ananiambia imeshindikana kupitia text. Mimi nikasema acha niwahi safari yangu Dar, chakushangaza anafika jioni ananiambia ujue nafikia kwako ila hutaki kujibu text zangu. Sasa kuongea naye anasema asubuhi alikuwa anatania tu. Mimi nikamwambia utakuja na kuondoka lasivyo nikuachie nyumba ukae mwenyewe. Anaanza kulalamika na kunilaumu, wakati kuna vitu utani utakucost. Mimi nikimwambia siwezi geuza msimamo wangu, na hajui kuwa mimi nimekereka kuliko yeye ila anataka abembelezwe, huo ujinga sifanyi. Hivyo kwamtu aliyekutana nayo, mizaha inakera na ni maudhi.
 
Acha kuwa serious sana na maisha utajinyonga Bure , so mbona hapo sijaona kosa kubwa la mkeo mpaka
Kukufanya u- react to that extent
 
Mkuu nadhani wewe ndo mwenye matatizo! Sasa kwa mfano hapo ulichokasirika mpaka kwenda kukaa barazani ni nini?
Mbona unacomplicate sana maisha? Kwa kweli kama mambo kama haya ndo ulienda kushtaki ukweni hakika walikushangaa sana!
Yaaani Nimeshangaa jamaa ni mkoloni Ile mbaya
 
Mimi ni mwanaume ninayependa masihara mengi. Nahisi mimi na mkeo tungeendana sana. Maisha yangekuwa ya furaha muda wote, kama mimi na mke wangu.
Kwa kuwa mimi nina kanuni mbili.

Nafanya jambo la seriously kwa njia ya masihara. Na nipo seriously kufanya masihara.
nimekuja dm mkuu naomba unijibu kuna jambo nimekuuliza
 
Nawasalimu.

Mnisamehe kwa kutokuwa mwandishi mzuri.

Moja kwa moja kwenye hoja ya msingi.

Nimeishi kwenye ndoa na huyu mke wangu kwa miaka 10 na kujaliwa watoto wawili.

Kilichonifanya nije hapa kuomba msaada wa mawazo ni hili tatizo la mizaha ya huyu mke wangu, amekuwa mtu wa kujibu au kuongea bila ya kuweka mipaka (kutenganisha kipi Cha kuongea na mpenzi na kipi Cha kuzungumza na mume ambaye ni mkuu wa kaya).

Nikiri ya kuwa katika maisha yetu yote nilishawahi mchapa makofi mara 3 kitu ambacho sitaki kukikumbuka na sitaki kitokee tena, ila nilifanya vile Ili tuu aweze kutambua kuwa sipendezwi na tabia zake.

Tabia hiyo ya kutokuwa na mipaka hasa ya kuzungumza haijawahi kwisha zaidi ya kupungua kwa muda na baadae kuanza tena.

Nimewahi kutumia kanuni ya kumtoa out na kwenda naye sehemu ya faragha na kumuambia kuhusu kutopendezwa na tabia zake huwa anaomba msamaha lakini baada ya muda hurudia tena.

Kiukweli ninampenda sana mke wangu, na mahusiano yetu yalianza tangu tukiwa secondary na baadae kuja kuoana.

Nje ya kumkanya mara kwa mara, niliona ni busara kufikisha jambo hili kwao, Ili waweze kumkanya binti yao, ila sikuona mabadaliko yoyote yale.

Yote yaliyotendeka niliweza kuvumilia ila hili nililolipata wiki hii, limenizidi uwezo. Baada ya chakula Cha jioni tukaingia chumbani, alikuwa anapanga nguo Mimi nikatangulia kuoga, baada ya muda nikatoka yeye akiwa Bado busy, kama kawaida kabla ya kulala ni kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake wa siku, nikasikia akiseme acha kusali uongo.

Niliumia sana, nikamaaliza sala na kumuuliza ulikuwa unamaana gani, nikaona anacheka, nikamuuliza hii midhaha yako itaisha lini lakini akawa anaendelea kucheka, kwa kweri nilipatwa na hasira sana ila niliishia kutoka kwenda barazani ningeendelea kuwa pale ningeweza kumpiga kitu ambacho sitaki kitokee tena.

Mimi nimemzidi miaka 4 huyu mke wangu, hata kielimu nimemzidi, kisalary nimemzidi zaidi ya mara 4.

Nimeandika hivi Ili kutoa Ile dhana ya kuwa huenda nalelewa, nafanya majukumu yangu kama baba vizuri kabisa(ada, matibu, mavazi, afya, makazi) kwake na kwa watoto wetu.

Kutokana na hili huwa nakuwa na mawazo sana, kitu ambacho natamani kufanya maamuzi magumu ya kumwacha ila moyo unasita.

Ushauri wenu utaniponya.
Jomba hapo mwenye shida ni wewe, humpendi tena ndio maana jokes za kawaida unafura kwa hasira, angekuwa mwenzio hapo kwa jokes hizo wangeishia kucheka na kugonga mikono na siku zingeendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom