Nawasalimu.
Mnisamehe kwa kutokuwa mwandishi mzuri.
Moja kwa moja kwenye hoja ya msingi.
Nimeishi kwenye ndoa na huyu mke wangu kwa miaka 10 na kujaliwa watoto wawili.
Kilichonifanya nije hapa kuomba msaada wa mawazo ni hili tatizo la midhaha ya huyu mke wangu, amekuwa mtu wa kujibu au kuongea bila ya kuweka mipaka ( kutenganisha kipi Cha kuongea na mpenzi na kipi Cha kuzungumza na mume ambaye ni mkuu wa kaya).
Ni kili ya kuwa katika maisha yetu yote nilishawahi mchapa makofi mara 3 kitu ambacho sitaki kukikumbuka na sitaki kitokee tena, ila nilifanya vile Ili tuu aweze kutambua kuwa sipendezwi na tabia zake.
Tabia hiyo ya kutokuwa na mipaka hasa ya kuzungumza haijawahi kwisha zaidi ya kupungua kwa muda na baadae kuanza tena.
Nimewahi kutumia kanuni ya kumtoa out na kwenda naye sehemu ya faragha na kumuambia kuhusu kutopendezwa na tabia zake huwa anaomba msamaha lakini baada ya muda hurudia tena.
Kiukweri ninampenda sana mke wangu, na mahusiano yetu yalianza tangu tukiwa secondary na baadae kuja kuoana.
Nje ya kumkanya mara kwa mara, niliona ni busara kufikisha jambo hili kwao, Ili waweze kumkanya binti yao, ila sikuona mabadariko yoyote yale.
Yote yaliyotendeka niliweza kuvumilia ila hili nililolipata wiki hii, limenizidi uwezo. Baada ya chakula Cha jioni tukaingia chumbani, alikuwa anapanga nguo Mimi nikatangulia kuoga, baada ya muda nikatoka yeye akiwa Bado busy, kama kawaida kabla ya kulala ni kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake wa siku, nikasikia akiseme acha kusali uongo.
Niliumia sana, nikamaaliza sala na kumuuliza ulikuwa unamaana gani, nikaona anacheka, nikamuuliza hii midhaha yako itaisha lini lakini akawa anaendelea kucheka, kwa kweri nilipatwa na hasira sana ila niliishia kutoka kwenda barazani ningeendelea kuwa pale ningeweza kumpiga kitu ambacho sitaki kitokee tena.
Mimi nimemzidi miaka 4 huyu mke wangu , hata kielimu nimemzidi, kisalary nimemzidi zaidi ya mara 4. Nimeandika hivi Ili kutoa Ile dhana ya kuwa huenda nalelewa, nafanya majukumu yangu kama baba vizuri kabisa( ada, matibu, mavazi, afya, makazi) kwake na kwa watoto wetu.
Kutokana na hili huwa nakuwa na mawazo sana, kitu ambacho natamani kufanya maamuzi magumu ya kumwacha ila moyo unasita.
Ushauri wenu utaniponya.