Mke kaniweka njia panda, naombeni ushauri

Mke kaniweka njia panda, naombeni ushauri

Mimi ni mwanaume wa miaka 35, nilioa mwaka 2009. Kabla ya kuoana tulipima na wote tulionekana tupo salama.

Tukazaa watoto Wawili, mwaka 2013 mke alianza kuumwa, alikuwa anatibiwa homa inarudia rudia, baada ya hali kuzidi akashauriwa kupima ukimwi mwaka 2015 na ndipo akagundulika kuwa ameathirika, na mme nikapima zaidi ya mara tatu nikaonekana ni negative.

Kwa muda wote huo tumekuwa tukitumia mipira katika tendo la ndoa. Kimsingi tangu nilivyooa sikuwahi kuchepuka. Shida niliyonayo mimi kwa sasa najawa na msongo wa mawazo kwa Muda mrefu hadi nimepungua kiukweli, sioni radha yoyote kwenye tendo, sipati msisimko wowote kwake. Moyo umekufa kabisa.

Nikiwa nae karibu ndio najawa na mawazo, sioni mapenzi yoyote kwake,,, kibaya zaidi hajawahi kuniambia alipataje na nikimuuliza anaanza kulia hadi kuchukua sumu kutishia kujiua. Ninashindwa nifanyaje nikijiangalia na umri wangu bado mdogo.

Naomba ushauri wenu wadau nifanyaje kwa sababu yeye anaonekana ana njaa kubwa ya tendo la ndoa na mimi hali ndio hivo.
Ndoa ni neno pana sana, mke kuchepuka linakuwa jambo kubwa sana but mme kuchepuka kawaida kabisa.

Kama lengo ni kukuambukiza ukimwi hata bila ngono akiamua ayakuambukiza kilaini tu.

Chamsingi ni wewe mwenyewe kuangalia moyo wako unakwambia nini? Kabla hajagundua hofu yako na namna unavyomchukulia kwasasa.

Kama moyo wako hauwezi kuwa nae achana nae for once. Akigundua unalengo la kumuacha sababu ya ukimwi atakuambukiza kiulaini tu na si lazima ngono.

Amuaka asubuhi moja mwambie basi na uwe umemaanisha usiangalie nyuma tena utakuwa nguzo ya chumvi.
 
Mke wako alichepuka..
Kama unapenda mfe wote mapema na kuacha watoto bila wazazi.. basi kuwa mjinga

Mnunulie matoi umsaidie muyachezee.. kumfikisha bila wewe kupata hayo..

Pole na kila la kheri, anatishia kujiua labda aliyempatia ni mtu wako wa karibu.. ndio maisha jipende..

Jua hawezi kujiua bali anatumia kama njia ya kutokukuambia ukweli.. huku yeye na wake wanajua. Au labda alikuwa analala na wengi wampe maraha na pesa na hajui yupi alimpa
So mchezo, huku upo vizuri balaa!
 
Mimi ni mwanaume wa miaka 35, nilioa mwaka 2009 kabla ya kuoana tulipima na wote tulionekana tupo salama.

Tukazaa watoto wawili, mwaka 2013 mke alianza kuumwa, alikuwa anatibiwa homa inarudia rudia, baada ya hali kuzidi akashauriwa kupima ukimwi mwaka 2015 na ndipo akagundulika kuwa ameathirika, na mimi nikapima zaidi ya mara tatu nikaonekana ni negative.

Kwa muda wote huo tumekuwa tukitumia mipira katika tendo la ndoa kimsingi tangu nilivyooa sikuwahi kuchepuka shida niliyonayo mimi kwa sasa najawa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu hadi nimepungua kiukweli, sioni radha yoyote kwenye tendo, sipati msisimko wowote kwake moyo umekufa kabisa.

Nikiwa nae karibu ndio najawa na mawazo, sioni mapenzi yoyote kwake kibaya zaidi hajawahi kuniambia alipataje na nikimuuliza anaanza kulia hadi kuchukua sumu kutishia kujiua ninashindwa nifanyaje nikijiangalia na umri wangu bado mdogo.

Naomba ushauri wenu wadau nifanyaje kwa sababu yeye anaonekana ana njaa kubwa ya tendo la ndoa na mimi hali ndio hivo.
1. Mna watoto(Wanakutegemea)
2. Ww huna yy anao(outcomes ni ww kuupata kwa makusudi)why?
3.Still young
4. Ukiupata umejipangaje au kujindangaya na mapendo ya kiSamson na Korean drama
5. Anataka kukuua kwa makusudi why yy kufa unaona kesi.
6. mtafuteni mshauri au doctor awapange maana wote ni viraza(sorry not sorry)
7. God first
 
Daaahh kuna watu mna roho ngumu " Yaani bado Una mto...... wakati umehakikisha mwenyewe kuwa Ameungua".... wallahi unastahiki tuzo"... Yaani mimi hata nguvu za kuvaa hizo condoms nisingekuwa nazo
 
Nimesoma kwa makini sana mada yako na ushauri wa watu wengine. Wengi wamekushauri wakiwa na mhemko mkubwa bila kuchambua kwa kina.

Kwanza mshukuru na umtukuze Mwenyezi MUNGU kwa neema na fadhila kubwa alizokufadhili katika maisha yako. Usidhani ya kwamba ugonjwa huo hujapata kwasababu wewe ni mjanja sana au upo makini sana, laaa! Ila hujapata ni kwasababu tu ya neema za Mwenyezi MUNGU juu yako. Hiyo ni zawadi ya uaminifu wako kutoka kwa Mola wako.

KUHUSU UGONJWA alionao mkeo, kuna dhana mbili za kuupata kwa kuzingatia kuwa kabla ya kuoana mlipima na wote mlikuwa negative. Dhana ya kwanza ni, Mkeo kaupata kwa njia ya kuuguza mgonjwa wa HIV au kwa njia ya vifaa vyenye ncha kali. Dhana ya pili ni kwamba mkeo kaupata kwa kuzini nje ya ndoa. Kwa kuzingatia maelezo yako, naona dhana ya kuwa amepata kwa zinaa inakuwa na nguvu zaidi. Naipa nguvu dhana hii kwasababu kila akiulizwa alikoupata baadala ya kukujibu anatishia kujiua kwasababu hana alternative yoyote ya kueleza au hata kujitetea. Sisemi kwamba alizini bali nimeipa tu nguvu dhana hiyo. Ukweli halisi anaujua yeye mwenyewe na Mwenyezi MUNGU. Na kwakuwa ww ndio unamjua mke vyema unaweza ukaderive ukawa na dhana yako mwenyewe, hata hivyo kumbuka huwezi kuchukua hatua kwa dhana, dhana inatakiwa ikusaidie tu kudodosa zaidi.

KUHUSU HUKUMU: Kwa imani yangu ya dini ambayo ndio inaniongoza maishani mwangu ni kuwa mwanandoa anayezini na akathibitika beyond reasonable dought kuwa amezini either kwa kukiri mwwenyewe au kwa watu kushudia akizini basi mwanandoa huyo (mwanamke au mwanaume) adhabu yake ni kuuawa kwa kupigwa mawe hadi mauti yake. Sasa kwasababu sheria hiyo haiwezi kutekelezeka kwa mazingira ambayo sheria za nchi zina nguvu kuliko sheria za dini, njia pekee ni kutalikiana na huyo mwenza mzinzi. Ningelikuwa mimi nikathibitisha kuwa kazini basi ningemuacha kwa wema tu. Kama sina uthibitisho basi ningesamehe na kumuachia Mwenyezi MUNGU ambaye amenikinga nisiambukizwe yeye ndio atatoa hukmu ya haki. Katika kipindi ambacho nimesamehe binafsi confidence ya kufanya tendo la ndoa bila kinga siwezi kuwa nayo zaidi nitafanya kwa kutumia kinga tu. Na kwa kuwa imani yangu inanipa ruksa ya kuoa mke wa pili binafsi kama bado nahitaji kuzaa ningeoa mke wa pili ili apate kunizalia watoto.

USHAURI WANGU nimeamua kuutoa kwa kuvaa tukio lako na kulifanaya kama langu ndio maana nimesema kama ningekuwa mimi. Kwa maoni yangu, kama hutathibitisha chanzo cha UKIMWI wa mkeo basi endelea kuishi naye kwa wemalkn uwe unamchunguza maana kama kweli ni mzinzi basi hataacha na ipo siku utamkamata na ndio utakuwa umepta sababu isiyo na shaka ya kutoa talaka.

Vilevile kuwa makini sana kuhusu mwenendo wa mkeo, wapo watu ambao wana hulka ya kutamani tatizo lake limpate mwingine. Angalia sana mkeo asijekuwa katika kundi hilo maana akiwa katika kundi hilo anaweza kufanya juu chini ili akuambukize! Kuna watu anapenda "tufe wote" au "kifo cha wengi sherehe".

MWISHO: Endeea kuwa mwaminifu, Mche Mwenyezi MUNGU aliyekuokoa na janga hilo. Usiingie kwenye kundi la wanaomuhukumu mtu halafu kumbe nao wanafanya hayohayo. Siku zote tambua kuwa huwezi kumchunga mtu, cha msingi ni ww kuwa mwaminifu, mwenyezi MUNGU atakuwa mlinzi wako na atakudhihirishia yaliyosirini mwao akitaka.

SOMO KUTOKA KWA WENGINE. Kuna kisa kimoja hivi nimewahi kukisoma mahali kitakutia nguvu: Kuna mwanamke mmoja huko njombe. Alikuwa ameolewa, ikafika kipindi akawa anaumwa umwa homa za mara kwa mara. Baadaye kuja kupima akagundulika ana HIV positive. Mumewe alipopima alikutwa yupo negative.

Mumewe alikuwa mtu muungwana sana, akakaa na mkewe kuhojiana naye kwamba wewe nimekuoa ukiwa bikra, hebu nieleze ukimwi umeupata wapi?. Mke alimwambia mume kuwa hata yeye hajui amaupata wapi kwasababu yeye hajawahi kuzini hata mara moja na amekuwa muadilifu maisha yake yote. Mume hakuwa na shaka juu ya uadilifu wa mkewe na akikumbuka alimkuta mkewe akiwa bikra wakati wanafunga ndoa.

Baadaye wakakumbuka kuwa kuna kipindi mkewe alimuuguza ndugu yake ambaye alikuwa HIV +VE na kwa kumbukumbu zake hakuwahi kutake any protection measures wakati wa kumuuguza. Basi wakawa wamepata jibu la chanzo cha ugonjwa.

Mume aliendelea kuishi na mkewe kwa wema na kwa upendo mkubwa sana. Alipokea ugonjwa wa mkewe kama ni mtihani kwake anaopaswa kuushinda. Mkewe alifarijika sana siku moja mume alienda akambusu mkewe wakati mke akiwa katika hali ya kukonda akumwa pale kitandani. Mke aliondoka duniani akiumia kumuacha mumewe lkn mume nae alitimiza mapenzi yake kwa mkewe na walitenganishwa na mauti kwa huzuni kubwa.
 
Ushauri ni rahisi tu mkeo anataka kukuambukiza ugonjwa sasa ni wewe na akili yako kufanya maamuzi magumu
yaani huyu jamaa nimemshangaa Ana moyo wa agape" mnoo " Amesahau kuwa UKIMWI hauambukizwi kwa kumtia tu pekee"... anaweza kuupata hata kwa kumla mate au kumnawa papuchi" endapo akiwa na michubuko".... kwenye dushe anavaa protection " sasa sijui kwenye mdomo na mikono atavaa gloves
 
Ushauri ni rahisi tu mkeo anataka kukuambukiza ugonjwa sasa ni wewe na akili yako kufanya maamuzi magumu
dah umeandika maneno mengi mpaka umenzidi mtoa mada kwakweli umechafukwa San na hichi kitendo kumywa maji kwanza
 
Pole sanamungu akupe wepesi ktk hili ili maisha yenu yaendelee kwa amani,waoneni watalamu wa afya watawashauri juu ya hili.MUNGU AKUBARIKI NA FAMILIA YAKO
 
Kijana maisha ya ndoa inapo fikia suara la ukimwi kwenye ndoa huwa ni kufanya maamuzi magumu bora mkutwe wote mnao mtavumiliana hivyohivyo tatizo mmoja awe nao mwingine hana ndo shida iko hapo
 
Najariibu kuvaa kiatu chako ila ni kikubwa mnoo naona kinanipwaya, so sorry
 
yaani huyu jamaa nimemshangaa Ana moyo wa agape" mnoo " Amesahau kuwa UKIMWI hauambukizwi kwa kumtia tu pekee"... anaweza kuupata hata kwa kumla mate au kumnawa papuchi" endapo akiwa na michubuko".... kwenye dushe anavaa protection " sasa sijui kwenye mdomo na mikono atavaa gloves
Kama ni wa kuupata UKIMWI angeliupata mapema sana. Kumbuka amekuwa kaikutana na mkewe kwa zaidi ya miaka mitatu bila kinga yoyote na hakupata. Amekuwa akikutana na mkewe kwa miaka mitatu mingine na hajapata. Nuru ya Mwenyezi MUNGU ipo naye. Lkn kwa kuwa ameshingia hofu, ni lazima atumie kinga.
 
Mkuu pole sana na una moyo wa pekee yako mpaka sasa bado upo na mkeo
 
Huyo dada alikutana na jamaa likamsugua kweli kweli. Inaonekana wewe jamaa yangu unaishia bao moja tu tena la dk moja na nusu yaani ukienda ukirudi ukienda tena wazungu haooo na hiko labda ndio kimekusaidia.

35 miaka bado kijana mdogo sana mjukuu wangu, huyo mkeo achana naye uhangaike na maisha mengine.
 
Kama ni wa kuupata UKIMWI angeliupata mapema sana. Kumbuka amekuwa kaikutana na mkewe kwa zaidi ya miaka mitatu bila kinga yoyote na hakupata. Amekuwa akikutana na mkewe kwa miaka mitatu mingine na hajapata. Nuru ya Mwenyezi MUNGU ipo naye. Lkn kwa kuwa ameshingia hofu, ni lazima atumie kinga.
hakuna mahali popote aliposema kuwa alishakwenda kupima tena" baada ya hiyo miaka " 3 ...so mimi nawewe hatuna uhakika kama jamaa bado nimzima". kama awali
 
Back
Top Bottom