Mke kaendelea kuhama chumba na kulala na watoto. Nimfanyaje mtu kama huyu?

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Mar 8, 2019
366
1,377
Wakuu salaam kwenu,

Nipo nawaza na kuwazua juu ya huyu mke wangu.

Miezi michache nyuma tulipishana kidogo, sasa tangu wakati huo hadi sasa kila akija hapa home hataki kulala na mimi chumba kimoja, yeye analala na watoto.

Kimsingi hatuishi pamoja, tunakutana zaidi kipindi cha likizo, sasa baada ya kuhitilafiana siku kadhaa nyuma na yeye kuanza kulala na watoto nikajua awamu hii akija home atabadilika.

Ila cha ajabu bado ameonesha msimamo wa kutotaka kulala na mimi chumba na kitanda kimoja na ukiangalia tulihitilafiana kwa masuala madogo sana. Sasa nashangaa mwenzangu hadi sasa bado ana bifu, sijui ndo anatafuta sababu ya kuvunja ndoa, sijui anatafuta nini, sielewi nimebaki njia panda?!

Wadau nimfanyaje huyu mtu, maana kama kuzungumza nae kipindi tumegombana tulishazungumza ila naona kama bado mwenzangu ana kitu moyoni mwake? Nifanyaje??

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Mwanaume hatakiwi kuja kulia lia hapa kisa mkewe hataki kulala nae. Ifike wakati wanaume tuwe na kitchen part Kama wanawake kujadili maswala ya masculinity . Haya yote yanatokea baada ya kwapa haki sawa mnaita 50/50.

Kuna muda mwanaume unatakiwa uwe dikteta ili mambo yanyooke na heshima ifate mkondo ndani ya nyumba.Moe suspension akajifunze jinsi ya kuwa mke.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Hamna funguka mkuu, hamja talafiana kwa jambo dogo, mwanamke akisusa chumbani mwake ni jambo kubwa kwake either uliingiza demu kwenye mashuka yake anayo fua kitantandani kwa ke au una mahusiana na mwanamke mgine ila hutaki kusema, kwa navo jua wanawake wanakua na hamu ya mahusiano kuliko wanaumme kama ni jambo dogo angekuja tu. Ila kuoa pia watumishi wa mbali kuna changamoto japo ulitaka mchangie matumizi ya pesa.
 
Give her time,
Kama intention zako it's to save your marriage,
Mpe muda, pia uwe mkimya and let her do what she does!
Ukimya wako itakua psychological treatment yake if it doesn't heal her and asilimia 100% she is cheating on you.
Kila lakheri.
Nimekupata sana mkuu ngoja nitulie niskilizie.

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Sasa Mke unayekutana nae wakati was likizo tu yani kwa mwaka mara 2 au 3 ndio Mke gani.
Kiufupi hapo wote mnafanya uzinzi,wewe unagonga huko ulipo na yeye anagongwa huko alipo mkikutana mnaambukizana tu magonjwa.

Ni kazi gani hiyo inayokufanya usiishi na Mkeo had I mkutane kipindi cha likizo pekee?
 
Kwahiyo licha ya kukaa na ukame kwakuwa mbali nawe hata alipokuja hajakutunuku? Kaa kimya toa matumizi yote na jua likitua tu potea home nenda kuangalia mpira au bar kunywa soda na kurudi usiku.

Tabia hii nenda nayo mpaka likizo iishe akisepa endelea na maisha Yako. Hii itamfanya ajione kumbe yeye si chochote si lolote na uwepo wake haukustui.

Atanyooka tu, kiburi kikizidi unahama nyumba wakati wa likizo akifika unaenda kupanga chumba Cha kulala tu. Yaani Kila akija utakuwa home muda wote ila kulala hulali hapo.
 
Hamna funguka mkuu hamja talafiana kwa jambo dogo mwana mke hakisusa chumbani ni either uliingiza demu kwenye mashuka au kitantandani kwa ke au unamahusiana na mwanamke mgine ila hutaki kusema, kwanavo jua wanawake wanakua na hamu ya mahusiano kuliko wanaumme kama ni jambo dogo angekuja tu.
Mkuu sijaingiza demu wala nini ila muda mrefu nimegundua huyu mwanamke hana upendo wowote na mimi na yale matarajio yake ameona yapo tofauti. Ni mwanamke ambaye nilikutana enzi nasoma chuo, na tumezaa watoto ila kitu ambacho nimekiona huyu keshachoka ndoa na mimi maana kila mgogoro mdogo anakimbilia kusema tuachane bora aishi msimbe na mdangaji. Ila awamu hii nimeamua nimkalie kimya

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom