Mke anataka waachane, mume hataki bado anampenda

Mke anataka waachane, mume hataki bado anampenda

"Watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa" hayo ni maneno ya Biblia.

Mganga hatomsaidia kitu sana sana atamuongezea idadi ya mapepo tu na kummalizia pesa yake.

Kama ndoa imefikia kiwango hicho ni kama haiwezi kurekebishika tena.yeye cha kufanya apige moyo konde afungue shauri mahakamani la kudai talaka, mgawanyo wa mali na custody ya watoto.

Lakini kabla ya kufungua kesi akusanye kwanza ushahidi wa kujitosheleza wa kumuwezesha kushinda kesi.

Au kama anampenda mkewe amsamehe, atafute washenga wake na wasimamizi wa ndoa yao kwa ajili ya kutafuta muafaka. Nadhani mkewe ana ndugu wengine wanaoweza kumuweka chini na kumkumbusha kiapo alichokula na udanganyifu wa mchepuko wake .

Na yote hii imesababishwa na mahaba ya mbali, wakati mume anakuja mwisho wa wiki kuna ambaye anakuwa naye mara kwa mara , ndiyo tujifunzepo na siye wengine kuwa mahaba ya mbali kuchapiwa lazima. labda kwa mtu ambaye ana hofu ya Mungu ambayo si ya kawaida.
 
Hii ndio shida ya ndoa zinazobebwa na material things. Huyu mwanamke hakuwa na mapenzi na mumewe ila alikuwa anataka kusomeshwa then akisimama kwa miguu yake amuache jamaa.
Jamaa akubali tu kuwa huyo sio wake tena, amuache aende! Aanze upya!
 
Nguzu za giza hazizimwi/kumalizwa kwa nguvu za giza. Zaidi anaenda tu kujiongezea maagano hapo ambayo baadaye yatamsumbua tu. And asije akapoteza tu maisha yake kisa ndoa, watoto wakamkosa baba yao na akawaachia uchungu wazazi wake bure. Mtu hakutaki, unataka hadi utolewe roho khaa
Point!!!
 
aachane nae tu kuokoa nafsi yake.
Jamaa sijui ni nn anachomn'gan'gania huyu mwanamke.....labda anaogopa wakiachana watagawana Mali maana wamejenga NA kuna baadhi ya Mali pia wamechuma wote.
 
Kwa waganga tena karne hii..jamani mbona maombi yako kila mahali

jaribu kumshauri rafiki yako aende maombi kulingana na dini yake

SI ajabu hata mke hajamuendea kwa mganga Ni uongo wa hao waganga ili wazidi kumlia pesa.
 
Haswaa, waganga ni waongo sana na wafitinishaji wakubwa, atamuongezea matatizo huyo jamaa na kumdanganya kuwa ni mkewe anamfanyia ili jamaa aendelee kuwa mteja wake. Inawezekana kabisa hata mke hamlogi, ila Mganga keshamharibu akili jamaa.

Btw, upendo haulazimishwi, kama huyo mke hamtaki basi abakie zake huko aliko aanze maisha kivingine, wasije 'wakampalestina' bure.
 
Nguzu za giza hazizimwi/kumalizwa kwa nguvu za giza. Zaidi anaenda tu kujiongezea maagano hapo ambayo baadaye yatamsumbua tu. And asije akapoteza tu maisha yake kisa ndoa, watoto wakamkosa baba yao na akawaachia uchungu wazazi wake bure. Mtu hakutaki, unataka hadi utolewe roho khaa
hajielewi huyo halafu ndoa bwana mwanamke yaani akiitaka itaishi na akiikataa hata ufanyeje hairudi tena!
Mwanamke kama hakutaki hakutaki tu!
 
mwambie aachane na mambo ya waganga, na pia aachane na huyo mke wake, aanze upya
 
mwambie jamaa aache ujinga hana mke mwishowe walogane wafe waache watoto wakiwa hawana malezi na mwelekeo wa maisha.. mwanamke kashaamua kuwa mbinafsi na ndiyo asili ya kila binadamu basi ubinafsi wao usiwaumize watoto jamani.... mwambie kama ni mapenzi hamna hapo , kipapa hapewi, pesa hapewi sasa kinachomgandisha ni nini sasa? aangalie ustarabu mwingine hizo hela anazowapa waganga afungulie watoto akaunti aweke humo loh
 
hajielewi huyo halafu ndoa bwana mwanamke yaani akiitaka itaishi na akiikataa hata ufanyeje hairudi tena!
Mwanamke kama hakutaki hakutaki tu!

Kwa kweli mwanamke akigoma ni amegoma, unless huko kwingine yamkute ndo atabadili gear. Ila kumbe kuna wanaume nao wanang'ang'ania ndoa mweee
 
Kwa kweli mwanamke akigoma ni amegoma, unless huko kwingine yamkute ndo atabadili gear. Ila kumbe kuna wanaume nao wanang'ang'ania ndoa mweee
Anafikiria alivyomsomesha,gharama alizotumia kumuweka classic leo hii wajanja wanakula kwa urahisss!!
Hvyo ndo wanavyowaza wanaume kugawana Mali akifikiria ndo anazidi kupagawa!
 
Kwenye ulimwengu huu ambao kinadada, kinamama wamejaa kila kona mtu anaenda kuloga apate penzi, hio si kawaida alishapewa limbwata,
Ushauri ni kwamba kwa mganga achukue dawa ya kinga tu afu aachane na huyo mwanamke kabisa koz vita ya uchawi sio nzuri inahamia ata kwa ndugu, marafiki kama watamshindwa
 
Back
Top Bottom