Marco Polo
JF-Expert Member
- Jan 16, 2014
- 8,988
- 12,442
Kuna jamaa tunafanya nae kazi nje ya mkoa wa Dar ameoa (ndoa ya kikristo) na ana watoto wa 3 mke ni mfanyakazi katika taasisi moja ya kibenki. Huyu mke jamaa ndio kamsomesha kuanzia degree mpaka post graduate.
Wamekuwa na ugomvi na mke wake siku nyingi tu ila kama miezi 5 iliyopita ugomvi wao umepitiliza, mke akawa anahitaji talaka na jamaa hataki kumpa mkewe talaka akidai kwamba bado anampenda.
Kabla hawajagombana jamaa alikuwaga na kawaida ya kwenda Dar kusalimia familia yake basi ikawa kila jamaa akija home kwake mwanamke anaondoka halali home na mshikaji akiondoka kurudi kazini mwanamke anarudi kiufupi mwanamke hataki kukaa pamoja na mumewe.
Bas visa vimeendelea mara achelewe kurudi Mara asije kabisa nyumbani yaani ili mradi ni shida tu. Mume alipoamua kumfuatilia mke wake akagundua anatoka na mwanajeshi. Jamaa kwa sasa ameamua kutoenda Dar mwezi wa pili huu wakati mwanzoni ilikuwa kila week yupo Dar home kwake kisa tu anahofia kuuawa kwa juju na mke wake.
Jamaa kwa sasa huku alipo anatangatanga kwa waganga tu ambao mimi naona wammalizia pesa na huko Dar, mwanamke naye anashirikiana na mama yake nao wanamuwinda jamaa kwa juju wammalize (maneno ya mume). Mpaka sasa hivi kuna mashindano ya nguvu ya giza kati ya mwanamke akishirikiana na mama yake dhidi ya jamaa.
Mimi nilimshauri jamaa amwache tu huyo mkewe ila ndio hivyo jamaa bado anashikilia akiamini waganga wanaweza okoa ndoa yake.
Sijui ungekuwa wewe ungemshauri vipi huyu jamaa maana nikimwangaliaga anatia huruma kwakweli na mwili wote umeisha maskini.