NDUGU WAPENDWA KUSUDI LA MUNGU KUTUUMBA SISI NI ILI TUPATE KUMCHA YEYE MUNGU USIKU NA MCHANA, NA KAMA BABA YETU ADAMU NA MAMA YETU HAWA WASINGEFUKUZWA KTK BUSTANI YA EDENI KWA KUKOSA,HIYO NDIO INGEKUWA KAZI YETU SAWASAWA NA KULE MBINGUNI, HIVYO KUMCHA BWANA HAKUNA WAKATI, BALI PIA TUMEPEWA MAJUKUMU MENGINE BAADA YA KUKOSA ,KWAMBA KWA JASHO LETU TUTAILIMA NCHI ( TUTAKULA )mtoa hoja amesema MAMA AKITOKA KAZINI ANAISHIA KANISANI NAPENDA KUKUMBUSHA YAFUATAYO:
1.KWA HUYO MKE " 1TIMOTHEO 5:8 '' LAKINI MTU YEYOTE ASIYEWATUNZA WALIO WAKE,YAANI WALE WA NYUMBANI MWAKE HASA ,AMEIKANA IMANI ,TENA NI MBAYA KULIKO MTU ASIYE AMINI''
2.JE MUME ANA UPENDO KWA FAMILIA??!!! ANAMWAMINI MUNGU??? ANA HOFU MBELE YA MUNGU??? KAMA HAYO HANA NENO LA MUNGU LINASEMA:
" TORATI 28:30 "UTAPOSA MKE NA MUME MWINGINE ALALALA NAYE, UTAJENGA NYUMBA USIIKAE, UTAPANDA MIZABIBU USITUMIE ( USIFAIDI ) MATANDA YAKE.
3.WAKE WENGI WAMEPELEKEA WAUME ZAO KUWA WALEVI NA MALAYA KWA MIDOMO YAO KWA KUKOSA UVUMILIVU PIA WANAUME WENGI KABISA WEMETEKWA NA MAKAHABA NA ULEVI WAKAZISALITI NDOA ZAO NA KUSABABISHA WAKE ZAO WAJAE HOFU NA KUTAFUTA MSAADA WASIUPATE HIYO HUJISALIMISHA KWA BWANA MUNGU ASIYESHINDWA NA CHOCHOTE.
umeongea vyema mwishoni, lakini kuna maneno mengine hapo, bora usingechangia kabisa kwasababu unakuwa kama unapromote watu wasiwe wanaenda kanisani. imefika mahali tuenende kwa roho na wala si kimwili tena, pamoja na kwamba Mungu ametupatia akili na utashi wa sisi wenyewe kuamua mambo, lazima tujue ya kuwa, akili ya kibinadamu, hekima za kibinadamu kamwe haziwezi kuwa juu ya kile ambacho Mungu amesema. NASAPOTI ASILIMIA MIA huyu mama aendelee tu kwenda kanisani, huko atapata pumziko la moyo, na Mungu atamsaidia kwa chochote anachokitafuta. unaposema mtu asiyewakumbuka wa kwao ni mbaya kuliko hata yule asiyeamini, hauna uhakika kama ni kweli huyo mama amewasahau wa kwao. umeanza kumhukumu tu bila kujua kama huwa anaweka mazingira mazuri kwaajili ya watoto wake kwanza ili pale atakapokuwa ameenda kanisani wasipate shida. kuna makanisa mengine hapo Dar es salaam, ibada zao zinaanza saa kumi na moja, mfano ni pale ubungo kwa ufufuo na uzima.nasikia wamehamia kawe kwa sasa. watu wanafunguliwa na wanapona mambo mengi, wanaacha kwenda kwa waganga wa kienyeji wanamtegemea Mungu. inawezekana huyu mama huwa anakuja kusimama hapo kupata ibada kabla ya kwenda home, na ibada haichukui muda mrefu. so instead of judging her kwamba amesahau wa kwao, ungesikiliza kwanza upande wa pili, usiamini kila mada inayoletwa hapa yenye upande mmoja biased, tayari ukaanza kuponda mambo ya Mungu kwamba wanaoenda kanisani wamesahau wa kwao, I HOPE HAUTARUDISHA ROHO ZA WATU WENGINE WATAKAOSOMA MSG YAKO HAPA NYUMA, kwasababu kwa ufahamu ninaouona kwako wa neno la Mungu, utadaiwa wewe. acheni wanaomtafuta Mungu wamtafute wapendavyo, na ninyi msiomtafuta Mungu endeleeni na dunia yenu...siku inakuja wale waliokuwa wanaonekana wapumbavu watakapoonekana wana akili. watu wengi wametanguliza dunia mbele kuliko hata mambo ya Mungu, wametoa muda kidogo sana kwaajili ya Mungu, wakatoa muda mwingi sana kwaajili ya dunia. na watu wengine bado wanasapoti, ati mtu awe anakumbuka wa kwao, are we sure kwamba hakumbuki wa kwao? wakati issue hapa iko wazi, huyu mwanaume anampiga vita huyu mama asiende church, ndo tatizo hapa, na wala si kusahau watoto. hakuna mlokole anaesahau watoto wake nawaambieni, hivyo naomba usijiunge na watu wanaowachukua watu waliookoka, ambao siku zote msg zao huwa ni kuponda na kudharau watu waliompa Bwana Yesu maisha yao, labda kama na wewe uko kwenye kundi hilo....usijiunge kwenye kundi la wapinga kristo, labda na wewe kama ni mpinga kristo. acha watu wamwabudu Mungu, hata kama ni masaa yote, unayajua mazingira ambayo huyo mama na familia yake wanaishi?unamjua huyo mume alivyo?
pengine mume mlevi wa kubebwa kwenye tolori, mzinzi na ameshaleta ukimwi ndani ya nyumba kwa mama watoto aliyekuwa ametulia yeye akaenda kuchuma ukimwi kwa machangu doa huko baaa, sasa mama wa watu anahangaika na mzigo ambao hakuuchuma yeye. you never know, don'g judge kabla ya kufikiria kuhusu upande wa pili, hasa katika mambo ya Mungu, utajikuta umetumika na shetani hivihivi. ndo ushauri wangu huo kwako.