Mke anashinda Kanisani !!

Mke anashinda Kanisani !!

Hii kitu ni ngumu sana... Kuna ndugu yangu ana-experience the same thing. Mke wake halali nyumbani anasema anaenda kwenye mikesha. Hajui watoto wamekula nini au wamelala vp, kibaya zaidi hata huyo HG hana, anategemea mtoto wake wa miaka 10 ndio amuhudumie baba yake. Hivi hapa mwanaume akiamua kuoa mke mwingine anaweza kulaumiwa??
 
Dah mpe pole yake
Huyo mama naona imani imempitiliza ndo yale yale wajinga waliwao. Mchungaji anadumisha mila kama kawa wao wanajiliwaza na vimaneno ati usifuate matendo ya mchungaji fuata neno haya jama, na wachungaji wa siku hizi wanajua kutengeneza fweza vibaya mno wanawakamua wauumini mpaka wanaimba haleluya. Bongo bana.
 
Rafiki yangu analalamika....,

Ndoa yake na mkewe haina muda mrefu sana , wote wana toka katika familia ya kikristu wa dhehebu la Kiroma na ndipo walipofungia ndoa yao.

Mungu kawajalia watoto na kazi nzuri pia.

Kwa takriban miezi saba sasa, Mkewe ambaye anaelimu na kazi nzuri amekuwa akisali katika moja ya haya makanisa ya "upendo/upako". Alianza kidogo kidogo kwa kuhamasishwa na wenzake sasa amebobea kuliko hata "mama mchungaji", imefikia kiasi cha kuwa kama amerogwa na "neno", kila siku anachelewa kurejea nyumbani toka kazini na mume akimuuliza anamjibu alikuwa kanisani...na akirudi nyumbani ni mapambio tu kwenda mbele,

Kwa siku za jumamosi na jumapili, inakuwa kama mama hayupo kabisa nyumbani na huwaacha watoto na msichana wa kazi akidai yeye yupo kanisani kuiombea familia yake.

Rafiki yangu anasema amejaribu kumsihi sana mkewe amunguze hiyo kasi ya kanisani ili pengine aangalie familia na asiache muda mwingi wa majukumu yake unachukulia na msichana wa kazi. Lakini sasa mke imefikia mahala anasema hawezi kamwe kuacha kanisani hata sekunde moja na ni heri aachike kuliko kupoteza ufalme wa mbingu...na anamweleza mumewe kuwa akizidi kumkera kwa hili la kushinda kanisani itabidi akaombe maombi maalumu ya kufunga kwa ajili yake kwani anaona yeye sasa ni kama ibilisi.....

Hivi hali inapofikia hivi, tunajenga au tunabomoa??...

hili ni tatizo kubwa sana siku hizi;

jamaa inabidi aangalie kwani mara nyingi mpaka mwanamke aamue kubadili dhehebu na kushinda kanisani inatokana na masumbuko ya moyo aliyonayo na mara tunayasababisha sisi wanaume!

he needs to look back, see where he messed up and clean up! mimi nina dada likua hivyo kutokana na jamaa kuwa kifimbo cheza na mlevi na walikua wanagombana sana; dada alishinda huko mpaka na akawa mchungaji (orginally alikua rRC); jamaa amebadilika na mama amepunguza hata muda wa kukaa kanisani

we have to admit kwamba hata wanawake wanahitaji peace of mind na wengine huitafuta mitaani na wengine kwenye nyumba za ibada

its a sad truth, but we hvae a big role to play
 
Watu wengi wanakuwa obssessed na hizi dini bila kuelewa nini lengo la hawa wenye makanisa. Asilimia kubwa ya makanisa yanayochipuka yanakuwa ni kukidhi matakwa binafsi ya wenye makanisa. Mengi ni vitega uchumi vya waanzilishi wake.

Neno la Mungu lasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Hakuna hata kanisa moja litalompeleka mtu mbinguni. Watu wengi wanatapata kwa kubadilisha makanisa kila kukicha kama fasheni hasa akina mama.

Wokovu wako uko juu yako mwenyewe na wala si mhubiri fulani kwa kuwa anatenda miujiza na kujitukuza. Unachotakiwa ni kulijua neno la Mungu na kuliishi.

Kwa huyu mama anaeshinda kanisani ameshidwa kutambua kuwa familia ni zawadi kutoka kwa Mungu na hana budi kuitumikia familia yake na kuipenda maana Mungu asema usipompenda ndugu yako unaemuona utampendaje Mungu usie muona? Kristu mwenyewe alisema mpe kaizari yaliyo ya Kaizari na Mungu yaliyo ya Mungu.

Jihadharini na Makanisa yanayochipuka kila uchao kwani si mpango wa Mungu. Maana Kristu alisema iweni na umoja kama mimi na Baba tulivyo na umoja. Matengano na mafarakano ni kazi za shetani.
 
Kama huyu Mama ana hausigeli ameula wa chuya. Kama hana, ajiandae kusoma namba kwani watamdaka mumewe huko uraiani. Anamtia mumewe majaribuni - atachoka kusihi....
 
Nakumbuka hata wakati Kakobe anapamba moto miaka ya 1996-1998 ndoa nyingi zililegalega kama si kuvunjika kabisa, akina mama wengi walichagua kuishi kanisani kwa Kakobe kuliko kushinda na family zao home. Huo mama Ajue kabisa kwamba ndoa ni mungu aliiweka saa anakiuka kiapo chake mwenyewe? anatenda dhambi bila yeye kujijua, nadhani bado mapepo hayajamtoka vizuri anahitaji KUPUNGWA kwa sala na maombi

hivi huyu jamaa baada ya Tanesco na nguzo zao, ameishia wap? ule umeme ulikataa kuwaka kama alivodai ama?
 
Neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi; bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu: - 1Wakorintho 1:18 Ndivyo biblia inavyosema - ndio maana wengine hawaoni umuhimu wa kuabudu au kusikia neno la Mungu au kumsifu Mungu au kuomba katika nyumba ya Ibada (Kanisani) kwa muda mrefu - siku nzima au hata mkesha (usiku kucha); Kwao kukesha kwenye pombe, clubs, kukesha kuangalia mipira, TVs etc ni sawa ila Kanisani wanaona ni upuuzi

Pia katika Biblia imeandikwa: "LAKINI NATAKA MSIWE NA MASUMBUFU. YEYE ASIYEOA HUJISHUGHULISHA NA MAMBO YA BWANA AMPENDEZEJE BWANA; BALI ALIYEOA HUJISHUGHULISHA NA MAMBO YA DUNIA HII, JINSI ATAKAVYOMPENDEZA
MKEWE. KADHALKA ...................... YEYE ALIYEOLEWA HUJISHUGHULISHA JINSI YA KUMPENDEZA MUMEWE" 1Wakorintho 7: 32-35.
Kifupi ni kuwa watu wengi (Wanaume/Wanawake) wamekuja kumjua Bwana Yesu baada ya kufunga ndoa - (NA JINSI ILIVYO RAHA KUMPATA YESU MAISHANI) wanatamani kuwa na Yesu na kufanya mambo ya Yesu 24 hrs. ili hali wana familia - kwa kweli inabidi tu wabalance -
inabidi MWANAMKE AJIPANGE - TENGENEZA CHAKULA, SAFISHA NYUMBA, HAKIKISHA MAMBO YA NYUMBANI KWAKO YAKO SAWA - KISHA NENDA ZAKO KANISANI HALAFU MWOMBEE SANA MUMEO ILI AKUELEWE KWANI KUPITIA WEWE ANATAKASWA (Bible inasema hivyo)

Wana JF - onjeni muone YESU alivyo mwema ........... kuliko pombe, sigara, uzinzi, mipira, ufisadi, umbea etc. - na Karibuni anarudi tena - sio dini wala dhehebu - ni YESU
Ifike FAMILIA ZISHINDE KANISA (BABA, MAMA NA WATOTO INCLUSIVE) ili wote siku moja TUISHI MILELE NA BWANA
 
kweli, mara mia, bora washinde kanisani, kuliko wale wanaoshinda bar, kwenye madanguro wakidangura na wanaume wengine, kuliko wale wanaokula supu na mguu wa mbuzi baa wakati watoto wanakula wali au ugali na housegirl. nakwambia, kati ya vitu vyema huyo mama amechagua, ni kukimbilia kwa Yesu,na huyo jamaa ashukuru Mungu tu, kwasababu akimharasi sana huyo mama akarudi nyuma, ataenda kumpata bar anakunywa na wanaume wengine, hapo tena atarudi hapa aje kualamika mke wake kaacha kanisa sasa amekuwa mlevi na mzinzi. asisumbue akili zetu hapa, hili ni jambo la kushukuru wala si kulalamika.

kwa habari ya huyu mama, siamini kama haachi chochote kwaajili ya watoto kama inavyoongelewa hapa, hakuna mchungaji anayeweza kuwaruhusu washirika wake kufanya kitu kama hicho, kwanza hiyo ingekuwa dhambi, na ni kosa la jinai kwa kutokuwapa watoto wako haki za msingi. kwa mama mwenye uchungu wa labour, hawezi kuwatelekeza watoto wake hivyo. hapa huyu jamaa kinachomuuma si mama kutohudumia watoto, ni huyu mama kwenda makanisa ya kilokole. sasa endelea kumharas, atakaporudi nyuma akaenda kunywa mipombe akarudi chakali akakupiga na vibao ndo utakuja tena hapa kutusumbua na maswali yako. huu ni ushauri wa bure, yakikupata usiseme nilikuwa na mdomo mbaya.
 
Heri akakae kanisani kuliko baa. Kuna waume wengi wanachelewa sana kurudi nyumbani wanarudi wamelewa watoto wamewasahau, hao ndio wabaya zaidi.
 
Preacher... you dont have to be uni-dimensional kamwe; sidhani kama kwenye hii thread tunaongelea pombe, sigara, uzinzi au mipira... we are talking of the family na nadhani unaelewa vyema kuliko mistari miwili au mitatu uliyoamua kui-quote kuhalalisha mtu kukaa mbali na familia yake full time

we dont condemn mtu kusali, but we condemn extremism kiasi cha kuacha jukumu mama la familia

Je yesu alishinda kanisani kutwa?
Ukishinda kanisani utasaidia vipi kuwavuta waliopotoka?
je wewe unashinda kanisani?
je tukishinda kanisani tutakula mbao?
Je unadhani kama unashinda kanisani kutwa wakati unahukumu kila aliye nje ya kanisa ndivyo tulivyofundishwa?

MImi si strong muumini kama unavyoji-portray wewe lakini kumbuka [i read it somewhere though] kwamba bible imeandika neno wisdom mara nyingi kuliko neno salvation!!!!

ask your self why?

DN
 
kweli, mara mia, bora washinde kanisani, kuliko wale wanaoshinda bar, kwenye madanguro wakidangura na wanaume wengine, kuliko wale wanaokula supu na mguu wa mbuzi baa wakati watoto wanakula wali au ugali na housegirl. nakwambia, kati ya vitu vyema huyo mama amechagua, ni kukimbilia kwa Yesu,na huyo jamaa ashukuru Mungu tu, kwasababu akimharasi sana huyo mama akarudi nyuma, ataenda kumpata bar anakunywa na wanaume wengine, hapo tena atarudi hapa aje kualamika mke wake kaacha kanisa sasa amekuwa mlevi na mzinzi. asisumbue akili zetu hapa, hili ni jambo la kushukuru wala si kulalamika.

kwa habari ya huyu mama, siamini kama haachi chochote kwaajili ya watoto kama inavyoongelewa hapa, hakuna mchungaji anayeweza kuwaruhusu washirika wake kufanya kitu kama hicho, kwanza hiyo ingekuwa dhambi, na ni kosa la jinai kwa kutokuwapa watoto wako haki za msingi. kwa mama mwenye uchungu wa labour, hawezi kuwatelekeza watoto wake hivyo. hapa huyu jamaa kinachomuuma si mama kutohudumia watoto, ni huyu mama kwenda makanisa ya kilokole. sasa endelea kumharas, atakaporudi nyuma akaenda kunywa mipombe akarudi chakali akakupiga na vibao ndo utakuja tena hapa kutusumbua na maswali yako. huu ni ushauri wa bure, yakikupata usiseme nilikuwa na mdomo mbaya.

another one... naona mnataka kubadilisha mada kutoka kwenye family focus kuingia kwenye pombe na ma-bar!!!

someni ile post ya kwanza vizuri na mjue kama jamaaa anashinda bar au vipi---- speed in a wrong direction is irrelevant ! alisema mwanazuoni Mahatma
 
Jamani sie binadamuhatutabiriki.Kama angekuwa anacheat kwa uzinzi nje ya ndoa angeonekana shetani.anakwenda kanisani bado anamuona mbaya badala ya kumshukuru Mungu.Uliposema for better for worse ni pamoja na situation kama hizi.akae chini na mkewe wazungumze na aaribu kumuelewa na kumuonyesha upendo zaidi.Atabalance muda vizuri ili upande wowote usiathirike.
NB.asimkataze kwenda kanisani,baada ya kitambo akikomaa kiroho atakuwa mke bora sana na hata yeye atapata baraka na ulinzi wa Mungu kupitia mkewe.
 
Hii kitu ni ngumu sana... Kuna ndugu yangu ana-experience the same thing. Mke wake halali nyumbani anasema anaenda kwenye mikesha. Hajui watoto wamekula nini au wamelala vp, kibaya zaidi hata huyo HG hana, anategemea mtoto wake wa miaka 10 ndio amuhudumie baba yake. Hivi hapa mwanaume akiamua kuoa mke mwingine anaweza kulaumiwa??

Mpe pole huyo nduguyo, ukitaka kujua undani wa hii mikesha na makambi yao na uchafu uliogubikwa kwa matendo yasiyofaa basi fanya kufuatilia huko yalipo makambi aidha kwa kujifanya na wewe ni muumini wa kutupa au wauulizie vijana or ma-Tax driver wanaoishi karibu na makambi yoyote ya waumini hao watakupa ukweli kwani wengine na wao wanakula na mizigo kiulaini na kupewa posho nzuri za huduma zote mbili, Ukweli ukimwi ni tatizo kubwa kuliko tunavyoliangalia
 
Jamani sie binadamuhatutabiriki.Kama angekuwa anacheat kwa uzinzi nje ya ndoa angeonekana shetani.anakwenda kanisani bado anamuona mbaya badala ya kumshukuru Mungu.Uliposema for better for worse ni pamoja na situation kama hizi.akae chini na mkewe wazungumze na aaribu kumuelewa na kumuonyesha upendo zaidi.Atabalance muda vizuri ili upande wowote usiathirike.
NB.asimkataze kwenda kanisani,baada ya kitambo akikomaa kiroho atakuwa mke bora sana na hata yeye atapata baraka na ulinzi wa Mungu kupitia mkewe.
hili nalo neno!
 
Kama huyu Mama ana hausigeli ameula wa chuya. Kama hana, ajiandae kusoma namba kwani watamdaka mumewe huko uraiani. Anamtia mumewe majaribuni - atachoka kusihi....

Ni kweli Tadeus anataka kumpoteza mzee ..kila kitu kinafanywa kwa kiasi asipomjali mme anategemea nin?
lazima apate msaidizi
 
Hilo sio kanisa bali ni kitu kingine. Vp mchungaji wake ni yule wa viti maalum CCm asiye ishi na mume?

I
nawezekena mchunguzi wake ni yule mzee wa mwenge mwenye kuvunja ndoa nyingi za wahumini wake,
 
Heri akakae kanisani kuliko baa. Kuna waume wengi wanachelewa sana kurudi nyumbani wanarudi wamelewa watoto wamewasahau, hao ndio wabaya zaidi.

Nawachukia wanaume hawa wanaona kama nyumbani ni kituo cha police anakosa mapenzi ya mke na watoto ..haipendezi hata kidogo...
 
TATIZO KUBWA NINALOLIONA HAPA NI HUYU MWANAMME KUTOKWENDA KANISANI. KAMA ANAMPENDA MKEWE, BASI NAE AANZE KWENDA HUKO,HUKO NDIKO ITAKUWA RAHISI KUMRUDISHA MKEWE KWENYE MSITARI. ITAFIKA WAKATI MAMA ATASEMA 'MUME WANGU TURUDI NYUMBANI WATOTO WAKO PEKE YAO.KAMWE USITATUE MATATITZO YA MAPENZI KWA KUYAKIMBIA AU KULAUMU.HUKO HUKO KANISANI AKAMBADILISHIE HUKO.NA YEYE MUME AKIKOLEA WAKAWA WOTE WANAIMBA MAPAMBIO USIKU KUCHA KUNA TATIZO GANI? WANAUME ISHINI NA WAKE ZENU KWA AKILI. Heeeeeh mke wangu hajarudi hadi saa nne usiku nimeganda tu home eti namngoja NO. hukohuko nami nitaendaimba mapambio hata kama siyajui..hivyo hivyo tu.
 
Heri akakae kanisani kuliko baa. Kuna waume wengi wanachelewa sana kurudi nyumbani wanarudi wamelewa watoto wamewasahau, hao ndio wabaya zaidi.

FL 1 inawezekana huko kanisani ni chakula cha mchungaji ndo maana anachelewa sana kurudi hm,kwa hiyo jamaa(mme) anaambulia mapambio tu.
hilo nalo tulifikrie
 
Kuna kisanga kimoja niliona hapa nilipo ilikuwa aibu tupu ..mungu atusamehe na aendelee kutupa imani iliyotimilifu
 
Back
Top Bottom