Mke anashinda Kanisani !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke anashinda Kanisani !!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ngoshwe, Apr 28, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Rafiki yangu analalamika....,

  Ndoa yake na mkewe haina muda mrefu sana , wote wana toka katika familia ya kikristu wa dhehebu la Kiroma na ndipo walipofungia ndoa yao.

  Mungu kawajalia watoto na kazi nzuri pia.

  Kwa takriban miezi saba sasa, Mkewe ambaye anaelimu na kazi nzuri amekuwa akisali katika moja ya haya makanisa ya "upendo/upako". Alianza kidogo kidogo kwa kuhamasishwa na wenzake sasa amebobea kuliko hata "mama mchungaji", imefikia kiasi cha kuwa kama amerogwa na "neno", kila siku anachelewa kurejea nyumbani toka kazini na mume akimuuliza anamjibu alikuwa kanisani...na akirudi nyumbani ni mapambio tu kwenda mbele,

  Kwa siku za jumamosi na jumapili, inakuwa kama mama hayupo kabisa nyumbani na huwaacha watoto na msichana wa kazi akidai yeye yupo kanisani kuiombea familia yake.

  Rafiki yangu anasema amejaribu kumsihi sana mkewe amunguze hiyo kasi ya kanisani ili pengine aangalie familia na asiache muda mwingi wa majukumu yake unachukulia na msichana wa kazi. Lakini sasa mke imefikia mahala anasema hawezi kamwe kuacha kanisani hata sekunde moja na ni heri aachike kuliko kupoteza ufalme wa mbingu...na anamweleza mumewe kuwa akizidi kumkera kwa hili la kushinda kanisani itabidi akaombe maombi maalumu ya kufunga kwa ajili yake kwani anaona yeye sasa ni kama ibilisi.....

  Hivi hali inapofikia hivi, tunajenga au tunabomoa??...
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ubomoaji with horns raised high up!
  Mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe!...Haiwezekani ukapotelea kanisani na kuacha majukumu ya kifamilia...Ndo shida ya kulimbukia dini hizi!...Mungu alijua wazi mambo hayo na ndo maana aliweka siku 6 za kazi na akastarehe siku ya saba, ambayo ndo hasa tunaitumia kuabudu na kujumuika, tofauti na siku zingine!
  Hakuna jambo lisilokuwa na kiasi!...Mwambieni huyo mama kwamba hata kuhudumia familia ni ibada!
   
 3. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  na hiyo kurudi nyumbani na mapambio yake, hapo unakuta kelele mtindo mmoja kama anapunga mapepo vile, awe na kiac....wokovu nao ukiuingiza sana kwenye maisha unaleta shida jamani, sasa mama wa familia unashinda kanisani mbona hata kwako kunaweza kuwa kanisa tu na sala/maombi yako yakackika?
   
 4. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #4
  Apr 28, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hii kali. kanisa gani hilo wanalotakiwa kwenda kila siku na kurudi usiku? kwani hawezi kuombea akiwa nyumbani hawezi kuombea familia hadi aende kanisani?
   
 5. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hizi dini za kizungu ukichanganya na udaku flani wa kiswahili zinakuwa fujo tupu. Bora turudi kwenye jando na unyago.
   
 6. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #6
  Apr 28, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  hahahah jamani mbona sometimes wanawake tunakubali kuchezewa akili hivi? hivi huyo mchungaji anayeturubub=ni yeye huwa hayuko karibu na mkewe mama mchungaji? Mungu mwenyewe kasema tuwe na kiasi, hata kama tunasali tunatakiwa kupause na kwenda kujiliana kisha twarejea tena salani sasa hii ya non-stop imeletwa na mungu yupi yarabi??

  Shangazi yangu ambaye aliolewa na kubadilishwa dini toka uislamu na uncle wangu alijakuja mlokole kupindukia akawa anashinda kanisani akiulizwa anadai yesu wake hamruhusu kushare meza moja na shetani mlevi (yaani uncle wangu) uncle akanyamaza na kuamua kusitisha huduma kwa miezi sita, shangazi akendalalamika miezi imepita hajapewa haki yake- uncle akajitetea kuwa hakujua kama yesu wa mke wake anaruhusu kushare kitanda na shetani mlevi!!

  Shangazi amegeukia roma- kanisani ni jumapili kwa jumapili na jumuiya za hapa na pale!!
   
 7. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Hahhahaha! Roman ndilo kanisa lenye masharti nafuu kuliko yote nafikiri.
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  kuna mama mmoja ndoa imevunjika kwa style hii ..yeye alikuwa ni kanisa ,mkesha na yeye..mme akamwambia ameamua kumuacha aendelee na kanisa na yeye kuoa mwanamke anayempenda na kumjari .
  mama atakaejua amekula ameoga na amelala wapi ..sasa dada anatapatapa hana cha kufanya na mme ndo kishaoa mke mwingine
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Fixed Point nimeipenda hii
  "
  ARE YOU AND YOUR SPOUSE SPEAKING THE SAME LOVE LANGUAGE?[​IMG]"
   
 10. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Unajisikiaje weye Mwanaume pale mkeo mzuri, kijana, mmeona kwa ndoa ya kanisani, anaacha dhehebu alilokulia na kufungia ndoa anakwenda dhehebu jingine Akiwa hukoa anakuambia hataki kabisa kutoka na akiwa huko akakuwa na adabu kweli kwa "Baba Mchunga"(kama unavyoona akina mama an akina dada wanavyomshangilia Mzee wa Misukule, Kakobe, Mtume na Nabii Mwingira au Mzee wa Upako kwenye Runinga). AKirejea nyumbani kanuna, anapiga mapambio tu ukimuuliza anasema sema "YUPO NA YESU" ana amani.

  HIVI NI KUSEMA ANAMPENDA YESU ASIYEOMWONA N KULIKO WEWE MUMEWE??. NA UKIJARIBU KUMWELEKEZA ANAKUIMBIA VIPAMBIO Eti "HAKUNA MWANAUME KAMA YESU ......HALELUYA (Mipasho ya dini)

  Mabinti wengi sasa wamevurugikiwa na haya madhehebu Mapya, wengine wanasema ndo wanaenda kuomba mungu awape mume, awape kazi, awape watoto nk. LAKINI WAKIPATA inakuwa ndo wanapitilizia huko huko na kusahau yale waliopata...Mchungaji anakuwa na Amri juu ya Mwili wa Mkeo kuliko wewe..
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  NI KWELI MKUU PK
  LAKINI LAZIMA TUUJUE KILA MTU AMELETWA DUUNIAN ANA WITO WAKE....SASA BASI HAPO NI HUYO BABA KUOMBA HEKIMA NA REHEMA MUNGU AMUONYESHE
  KAMA NI WITO WA HUYO MAMA KUWAOMBEA WATU HANA JINSI ZAIDI YA HAPO ANATAKIWA AMSAPOTI HUYO MAMA KWENYE HUDUMA YAKE IKIWA VINGINEVYO NA KWELI AMEITWA BASI HUYO BABA ATAPOTEZA NDOA YAKE......

  PILI KABLA YA KUOANA AKUWA ANAJUA WITO WA HUYU DADA???PAMOJA NA HAYO MUNGU ANAMUDA WAKE KUKUTUNUKIA KIPAJI CHAKE SO NAFIKIRI NDUGU ULIELETA MADA MWAMBIE ASIICHUKULIE KIBINADAMU ZAIDI ATAUMIA AMWOMBE ROHO MTAKATIFU AMWONGOZE JAMANI AKUNA NYUMBA YA MUNGU YENYE MAFARAKANO.....UKIONA HIVYO MUNGU AKUPE NGUVU YA KUKAA NA KUMWELEKEZA MKEO NA HAPO NDIPO MTAENDELEA NA SI KUJA KWENYE MITANDAO KUTAFUTA MISAADA MINGINE INAKUWA """""""""""misukule"""""""""""""""""" unapoteza ndoa yako
   
 12. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Haya ni matokeo ya kutokulijua Neno vizuri.
   
 13. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  mpe pole kama ni wewe POLE YAKO
  HUYO AJAOA ANAZINI NDUGU NENDA KWENYE BIBLIA
  TAFUTA SEHEMU INAYORUHUSU KUOA MWINGINE TUSIJE KUWAJAZA
  WATU UJINGA ....................WATAPOTEA
  MKWE WANGU
   
 14. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  dini hizi bana !!1
   
 15. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Nakumbuka hata wakati Kakobe anapamba moto miaka ya 1996-1998 ndoa nyingi zililegalega kama si kuvunjika kabisa, akina mama wengi walichagua kuishi kanisani kwa Kakobe kuliko kushinda na family zao home. Huo mama Ajue kabisa kwamba ndoa ni mungu aliiweka saa anakiuka kiapo chake mwenyewe? anatenda dhambi bila yeye kujijua, nadhani bado mapepo hayajamtoka vizuri anahitaji KUPUNGWA kwa sala na maombi
   
 16. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #16
  Apr 28, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,029
  Likes Received: 561
  Trophy Points: 280
  Hilo sio kanisa bali ni kitu kingine. Vp mchungaji wake ni yule wa viti maalum CCm asiye ishi na mume?
   
 17. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #17
  Apr 28, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hekima na kiasi tu vimekosekana.
  Hakuna kanisa la kukufanya uwe mtumwa na usitekeleze wajibu wako kwa familia na taifa
  Lazima kuna tatizo hapo la kiufahamu kwa mhusika
  Mbarikiwe
   
 18. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #18
  Apr 28, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Asante FL1. unatakiwa kuongea the same love language na shem. na the most important ni kuelewa love language yake hata kama you dont speak the same language
   
 19. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #19
  Apr 28, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwanza Roman Catholic sio dhehebu ila makanisa mengine yote ya kikristu ndio madhehebu

  Hapa inategemeana, Je wakati wanafunga hiyo ndoa wote walikuwa Roman Catholic au mwanamke alikuwa mlokole?

  Tunabomoa!
   
 20. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #20
  Apr 28, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Acheni ujinga nyie, hivi mkiambiwa Mungu na mume bora nini? mume si udongo tu, Yesu alishasema na watu kama nyinyi kuwa, mtu kama hataacha familia yake ni kunifuata, hataurithi uzima wa milele, hakumaanisha uwachukie au uondoke home, bali alimaanisha kuwa, unatakiwa umuweke Yeye wa kwanza ktk kila kitu, Yesu ni mwa muhimu kuliko mume wako au mke wako. Mungu ndiye mwumbaji wetu unajua?....Mungu anatakiwa aheshimiwe kuliko hata mume wako, Mungu anatakiwa atafutwe kuliko hata mume wako, hata kama utapita kwenye moto alimradi unamtafuta Mungu ni bora.

  Huyo jamaa ashukuru sana Mungu kwamba mke wake anashinda kanisani. kwasababu anamuombea na yeye, na pengine anaishi leo kwa maombi ya mke wake tu. kuna watu hivi ninavyoongea wanalia mchozi, wanatamani wake zao wangegusa hata uwanja wa kanisa tu, wanatamani wanawake wao wamche Mungu, lakini wapi, wanashinda kunywa mipombe, wanashinda wakitoka nje ya ndoa, hawana hata hofu ya Mungu katika mioyo yao.

  Kukimbilia kwa Mungu kuna faida sana. huwezi jua kwanini huyo dada kakimbilia kanisani, inawezekana kuwa ameamua kwenda kanisani kwasababu tu Mungu amemgusa, akaamua kuokoka. pili ni pengine ameenda kanisani kutokana na matatizo ya kindoa ambayo huyo mwanaume anayo, angeongea yeye ndo tungepata picha halisi.

  ila kwahabari ya kwenda kanisani, nawatangazie enyi nyote msioenda kanisani, msiookoka na kumpa Bwana Yesu maisha yenu kama Bwana na mwokozi wa maisha yenu, bora mfanye hivyo mapema kabla usiku haujaingia, mtakapotafuta hata mtu wa kuwahubiria tu msimpate, mtakapotafuta walau hata pambio au nyimbo za dini lakini hamtazipata....wale wote waliompokea Bwana Yesu watakuwa wameshanyakuliwa na mpinga kristo atakuwa ameshaanza kuwatandika fimbo hapa duniani. MTAANI NINAPOKAA KUNA MAMA ANAFANYA KAZI NZURI SANA, anaendesha magari mazuri sana ya garama, ana nyumba nyingi zingine masaki, lakini anakunywa pombe, anakuja amekunywa kila siku. pamoja na usomi wote, kuendeshwa na mashangingi mazuri, ANAPIGANA NA MME WAKE KARIBIA KILA SIKU. mmewake hanywi, yeye akirudi amelewa anamfanyia fujo mmewe.

  Heri enyi mnaowaruhusu wake zenu kwenda kusali kumtafuta Mungu, kwasababu kwa mafundisho ya Mungu wanayoyapata watawafundisha na watoto wenu wakakulia katika njia ya Bwana, kuliko watoto wakakulia kwenye kufuga malasta, kuvuta mibange, kusuka nywele kama wanawake na mwishowe kuvaa heleni kama wanawake. kuna faida kubwa sana kumruhusu mkeo aende kanisani kumtafuta Mungu. kila mtu ataubebe msalaba/furushi lake peke yake mbele za Mungu, wewe kama unakatanzwa na mme wako usiende kanisani na unakubali, utaenda naye motoni. Mungu ni wa muhimu kuliko mume. mumeo akifa leo si utabaki na Mungu? au na wewe utakufa? kama hauombi na kumtafuta Mungu, tumaini lako ninini, ni mume wako? Mungu na awasaidie sana. natamani ningekuwa pauloniwaite wagalatia msiokuwa na akili....
   
Loading...