Fixed Point nimeipenda hii
"
ARE YOU AND YOUR SPOUSE SPEAKING THE SAME LOVE LANGUAGE?"
Hizi dini za kisasa ni za kuangalia sana, hakuna lolote huko zaidi ya kufarakanisha familia na ndoa!Hakuna dini isiyopenda kuona wawili wakiishi kwa amani na upendo!
Huyo mwanamke aambiwe tu achague moja dini yake au familia yake!
Hii tabia ya watu "kushikwa vibaya" na imani imekuwa kubwa sana siku hizi jamaa ikiwezekana ampeleke mkewe wa wataalam wa magonjwa ya akili(hasa Msongo)
Muhimbili. Tatitzo linatibika, kuna watu nawafahamu wamefunguliwa kutoka kwenye hali hiyo.
Mh...
Mungu ni mmoja mwenye nafsi tatu nae alituumba kwa mfano wake, akatuagiza tuyashike na kuyatenda yale yaliyo mema..na tukijua wajibu wetu na kuufuata.
Tafsiri ya maandiko katika Kitabu cha Mungu ni pana na wawezao kutafsri ndio waliofunuliwa kuwavuta hata wale ambao imani na matendo yao yanadhirishwa kwa mambo ya mwili na roho.
Pengine dini zetu zinatafiriwa kama "Bangi" ambayo ikikulevya sana, waweza kuchangaya ya "Kaisari" na yale ya "MUNGU"...Ipo mistari inaonya:
"Jihadharini na walimu wa Sheria ambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzu ndefu na kusalimiwa na watu kwa heshima sokoni; hupenda kuketi mahali pa heshima katika masunagogi, na kuchukua nafasi za heshima katika karamu. Huwanyonya wajane huku wakijisingizia kusali sala ndefu. Siku ya hukumu watapata adhabu kali!"
"Basi mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa! au Yupo pale! msimsadiki. Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo, watafanya ishara na maajabu, ili kuwapotosha wateule wa Mungu, kama ikiwezekana. Lakini ninyi jihadharini. Mimi nimewaambieni mambo yote kabla hayajatokea"
Je, yatupasa kushika imani ipi, ya Kristu au ya Madhehebu na Makanisa???..
Ubungoubungo nakuheshimu ! Sasa uliyoyasema yoote ni kweli kabisa. Swali linakuja kumheshimu Mungu ni kumdharau mumeo? Ili Mungu adhihirike kwa mumewe lazima matendo yake, tabia, na kila kitu kwanza mumewe alidhike navyo. Na kama ni otherwise sie Mungu huyo ni PEPO. Siku hizi mambo mengi yahee usikute kapata kajamaa huko kanamchelewesha anasingizia kanisa. Angekuwa Mungu huyo mume asinge complain maana kwanza roho ya Mungu ingeanza na mume kumuweka sawa ange feel confortable sana na asigelalamika.
hilo ndo kosa kubwa sana la kutokuelewa Biblia, umesema WATAWAAMBIA TAZAMA KRISTO YUKO HUKU AU KULE MSIWAAMINI, wewe umeshaweka kuwa alikuwa anaongelea madhehebu. kumbuka alisema, kama vile umeme uwakavo mashariki ukaonekana magharibi, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwa mwana wa Mungu, hakuwa anaongelea madhehebu hapa kuwa wale wanaohama madhehebu yasiyo ya kimungu wanakosea, alikuwa anaongelea mazingira. KUNA MTU ALISHAWAHI KUJA KWAKO KUKUAMBIA YESU AMESHASHUKA NA SASA YUKO KIMARA? AU YUKO MBAGALA, AU YESU AMESHASHUKA LEO SIKU YA MWISHO YUKO MASAKI, AU MBEZI BEACH, hii ndo ilikuwa maana yake.
ukweli unabaki palepale, kama ukiona dhehebu fulani halina njia ya kimungu, hama haraka kwasababu utakuwa unapoteza muda. madhehebu karibia yote yalivyokuwa yanaanzishwa yalikuwa na mkono wa Mungu, sasa kadiri muda unavyozidi kwenda, shetani huwa anayameng'enyua kidogokidogo baadaye anaharibu mfumo mzima wa kumwabudu Mungu, kiburi, kuabudu pesa na sanamu vinaingia, na Mungu akishaona hivyo tu ya kwamba watu sasa hawamwabudu yeye wanaabudu wafu, wanaabudu wanaowaita watakatifu, wanaabudu kupitia mwanadamu badala ya kupitia kwa Yesu, wanaombea wafu, wana kiburi cha fesha, Mungu huwa anaondoka anakwenda kwa mwanadamu mwingine ambaye atamheshimu, hivyo lile dhehebu ya kwanza linabaki kopo tu, hamna Mungu wala nini, Mungu ameshaondoka. HIVYO HAUWEZI KUWA NA AKILI TIMAMU KUSEMA KUWA UTABAKI KWENYE DHEHEBU LAKO HILIHILO MILELe, wakati pengine halina hata Mungu. utapoteza muda. ushauri ni kwamba, kama ukiona dhehebu halina Mungu, umefunguka macho ukaona hivyo, kimbia, jua hapo kuna shetani. kama hakuna Mungu basi kuna mkono wa shetani. ushauri wa bure.
inawezekana kabisa mchungaji akawa anatembea na huyo mwanamke......
wachungaji hawa wa makanisa yanayoibuka kila siku kwa kupenda wanawake hao.
hII BIBLIA NADHANI TUNAITAFSIRI TOFAUTI SANA.
NI DINI GANI INAYOFUNDISHA KUJUA MUNGU YUPO HAPA AU PALE KAMA SI YA KRISTO?? NA UTAITAMBUAJE HIYO KAMA SI IMANI YAKO AMBAYO INAONGOZWA PIA NA UTASHI WA KUJUA KUSALI SI LAZIMA UKASHINDE KANISANI UKIFOKA NA KUPWAYUKA KAMA MWENDA WAZIMU SIKU NZIMA NA BADAE UKAMULIWE KWA KUTOA MAPATO YA KAZI YA MIKONO YAKO UKAMPE MTU AMBAE ANAISHI MAISHA MAZURI KWA JASHO LA WENGINE ETI KISA YEYE NDIE ANAYEJUA KUTAFSIRI NENO LA MUNGU NA KUIONGOZA ROHO YAKO (BABA NA MAMA MCHUNGANI)??
NI DINI GANI INAYOTUFUNDISHA TUSHINDWE PENGINE KUTIMIZA WAJIBU MWINGINE WA KIDUNIA??
kWA NINI BASI NA TUSISALI MAJUMBANI MWETU INAPOFIKIA KUONA MAKANISA NA MADHEHEBU YOTE YAMEPOTOKA NA HAYANA MUNGU??
IKIWA TUNAENDA KANISANI KWA KUMTAFUTA MUNGU, JE, YUPO KIONGOZI YEYOTE WA DINI AU DHEHEBU LINALOONGOZWA KWA KUFUATA MISTARI YA BIBILIA (IWE HATA KWA KUPOTOSHA) ANAYEWEZA KUSIMAMA MBELE YA WAUMINI WAKE AKASAME KUWA YEYE NI NABIII WA UWONGO NA KWAMBA KANISA LAKE HALINA MUNGU KAMA HATAKUWA PUNGUANI ???
WOTE WAKISEMA WAO NDO KANISA LA KWELI, UKIWA NA UTASHI SAHIHI WA KIROHO HUWEZI KUONA KUWA KANISA AU DHEHEBU NDILO LITAKUONGOZA KATIKA KUMJUA MUNGU, KWANI KANISA NI KRISTO ALIYE MOYONI MWAKO NA NDIE KIONGOZI WA UKWELI KATIKA ROHO NA NI NJIA YA PEKEE YA KUEPUKA KUHANGAISHWA NA BUSARA ZA WANADAMU AMBAZO PENGINE ZIMEJAA MANENO MATAMU YA UPOTOSHAJI KULIKO ASALI !.
kUNA HAJA YEYOTE YA KUZUNGUKA HUKU NA KULE KWA HISIA LABDA HAPA AU PALE NDIPO KWENYE MUNGU??
TUNAKOSA NINI TUKISALI KIMOYO MOYO, TUKIONGOZWA NA ROHO NA KUMWOMBA MUNGU HAYA TUKIWA NA FAMILIA ZETU??
bwana mdogo, nilikuwa nakujibu swali tu, kwasababu niliona wewe haujaelewa sehemu fulani hivi ya bible inaposema ya kuwa, siku za mwisho watatokea makristo wa uongo, ya kwamba, mkisiikia yuko jangwani msiende, mkisikia yuko huku msiende, kama vile umeme uwakavyo mashariki ukaonekana magharibi ndivyo kutakavyokuwa kuja kwa mwana wa adam. Nilikuwa nakusaidia kukuelewesha uelewe kuwa hii haikuwa inamaanisha madhehebu, ilikuwa inamaanisha mazingira physically kabisa, mashariki mangaribi,kaskazini kusini, jangwani, nyikani etc. Kuna watu wachache wameshajitokeza kusema wao ni yesu ameshuka kulichukua kanisa, lakini wanapotea tu, ni shetani. Yesu alikuwa anamaanisha kuwa, siku hiyo yeye atakapokuja kulichukua kanisa lake, kufumba na kufumbua watu woote duniani watasikia parapanda yake, aliyeko marekani atasikia muda uleule na aliyeko ubungo na mbagala. Ndio maana alisema umeme ukiwaka mashariki muda huohuo unaonekana magharibi, akimaanisha kuwa, atakapokuja kulichukua kanisa lake tu, muda huo hakuna cha kuulizauliza, watu wote duniani watakuwa wameshajua kilichotokea kwa wakati mmoja, sio kwamba wamarekani au waarabu wajue kuwa yesu amekuja halafu wale walioko moshi na kenya wasijue, no, ndio maelezo hayo yesu aliyokuwa anasema.
Nikija kwenye swala lingine, ni wazi kwamba, madhehebu ni ngo tu ambazo watu wanaanzisha, na they are registered in the same status kama non-govermental organisations. Cha muhimu katika madhehebu ni msingi wake, msingi ukiwa umejengwa kwenye mabua na mchanga, icho kitakuwa ni kiti cha shetani. Msingi ukiwa umejengwa kwenye mwamba ambao ni yesu kristo aliye neno la mungu kulingana na yohana 1, basi yesu mwenyewe atakuwa pamoja na hil dhehebu. Kwasababu hii, mungu huwa anaangalia wako wapi wawili watatu waliokusanyika kwa jina langu ili mimi niwe papohapo katikati yao, akiona kuwa watu wamekusanyika kwa kufuata neno lake, atashuka na atakuwa pamoja nao, atakuwa mungu wao na atafanya mambo makubwa katika maisha yao. Akiona watu wamekusanyika katika michanganyo, kuabudu masanamu, kuabudu watu, kuombea watu wakati bible inakataza, hashuki hapo, haji ng'oooo.
Madhehebu mengi duniani yalianzishwa yakiwa na mungu, angalia rc lilianza vizuri sana na lilikuwa na mungu, lakini selikali ya kirumi ilivyolichanganya na siasa, wakaweka hekima za kibinadamu badala ya uongozi wa roho mtakatifu, walivyoanza kukwapua pesa kwaajiili ya msamaha wa dhambi, kukwapua pesa kwaajili ya kujenga st.peter kule vatican, walipoanza kutoza waumini pesa, na kufanya mambo mengi kwa kutumia akili za wanadamu, mungu akaondoka. Mungu akaonekana kwa watu wengine kama kina martin luther ambao mwanzoni walikuwa watu wa mungu, lakini baadaye wao pia kutokana na udhaifu wa mwanadamu, adui akaingia, ikawa dini isiyoongozwa na roho mtakatifu, matokeo yake mungu akaondoka kwasababu hawakuona kuwa yeye ni wa muhimu. Miaka ya arobaini hadi sitini kule marekani kwenye mtaa unaoitwa azuza street, watu wa mungu walipokuwa wakimwabudu, ndo kwa mara nyingine zaidi ya miaka mianne na ushee, roho mtakatifu aliposhuka, uamusho wa kanisa lililokuwa limejichanganya na siasa na akili/hekima za kibinadamu likaanza kuchipua kwasababu gani? Kwasababu roho mtakatifu alihusishwa kwenye ibada zao.
Walakinni yeyote yule asiyekuwa na huyo roho si wake, ukiona hauna roho mtakatifu wewe si mtu wa mungu. Ukiona unaabudu sehemu kavu, isiyokuwa na udhihirisho wa roho mtakatifu hapo kimbia hamna kitu. Mungu anajidhihirisha kwetu kupitia roho mtakatifu, ndo roho yake hiyo. Yesu alisema siwezi kuwaacha yatima, roho mtakatifu alikuwa ili tusiwe yatima, makanisa mengi yana majina lakini ni yatima, hayana msaidizi kabisa.
Kitu cha muhimu kukushauri ni hikii, na wote mtakaosoma. Ukiona unafanya jambo lolote lile bila uongozi wa roho mtakatifu, hili jambo mwisho wake ni uharibifu tu. Hata kama mungu ametupatia utashi na akili kama ndugu anavyosema hapa, lakini hakika yake hatuwezi peke yetu kwasababu hatujui yaliyoko mbele yetu, ndio maana ukiwa na mungu roho wake anatuongoza kufanya mambo mengi kwasababu anajua yaliyoko mbele yetu. Usijiamini sana ukaona wewe unaweza lolote ndugu yangu, hauwezi chochote, ni neema ya mungu tu hata kuongea hivyo. Unahitaji msaada wa mungu 100%, usifikiri kwasababu ya elimu yako, kwasababu ya chochote kile ulichonacho, ukafikiri wewe una hekima, utashi sana, au akili sana. Ajisifuye na ajisifu kwakuwa anamfahamu mungu. Mwanadamu akiwa na hekima nyingiiiiiii, hata mwisho, bado hajafikia hata kunusa tu hekima na ujuzi wa mungu. We are helpless, ile mungu ametupatia msaidisi roho mtakatifu.
Kwanini naongea yote haya, kwasababu makanisa mengi sana tz hayana uongozi wa roho mtakatifu. Mtu anakwambia tuombe halafu anaanza kusoma kitabu. Ibada zimekauka haziongozwi na roho. Yesu alisema siku zinakuja ambazo wamwabuduo halisi watamwabudu yeye katika roho na kweli kwasababu mungu ni roho nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. Kumwabudu mungu bila kumshirikisha roho mtakatifu ni bure. Mahubiri yasiyokuwa na uhuisho wa roho mtakatifu ni kande na mawe magumu hayana afya, ukihubiri hubiri katika uongozi wa roho, ukiomba omba kwa roho, ukifanya chochote cha kimungu fanya kwa uongozi wa roho. Nitaishia hapa nisije kumaliza ukurasa. But i have so much things to tell you my brother. God bless you, haleluya to the lamb of god!
Mtafute uyo mchungaji kwanza umuwashe mangumi kidogo,,. mafunzo gani hayo anatoa