Mkataba wa UN kuhusiana na masuala ya ushoga, usagaji na kubadili jinsia

Ushoga ni kosa kwa mujibu wa sheria za nchi. Anayejihusisha
nao ni muhalifu kama wahalifu wengine.
Ni kweli ushoga ni kosa, je ni makosa mangapi umeshudia watu wakitajwatajwa hovyo? Kuvunja katiba ni kosa kisheria, kuua watu ni kosa kisheria, kuteka ni kosa kisheria, kukwepa kodi ni kosa kisheria, kufoji ni kosa kisheria, kuvunja mikataba ni kosa kisheria kusingizia ni kosa kisheria, je haya mengine hayana madhara isipokuwa ushoga?
Tume ziundwe hata kwa mambo ambayo husababisha kupoteza uhai.

Wengine wanadhani eti maadiko yanakataza na ni laana tusidanganyike; wizi,uasherati, uuwaji, uchawi uwabudu sanamu kutoheshimu wazazi nk zote huleta laana na tunaziona hapa nchini siyo kwasababu ya ushoga tu?
 
Wameichomeka kinyemela kwasababu ndo inayobaki kulinda masrahi yao, walianza na soko huria, vyama vingi na sasa haki zinazosimamiwa kuelekea mwisho wa dunia ni hizi chafu haijalishi mnazitaka ama hamzitaki ..mkizingua mnanyimwa misaada, nyie si maskini bwana!!!? mlipoambiwa na Baba wa Taifa mjifunze kujitegemea wengi mliishia kutaka kumpindua ..kumbe hamkumwelewa vizuri na akirudi leo akakuta mshaanza kushikwa matako hakika atalia sana

Alale mahali pema peponi!
 
Hahaha umekuja na huku? Hakuna neno.

Umeuliza swali ambalo jibu lake ni kubwa na pana sana. Sio kwamba sitolijibu, bali nitakupa jibu la faida ila usiwe mvivu wa kusoma na kuelewa.

Tanzania tuna mila, desturi na tamaduni zetu... Kuna watu mnadhani hazipo au hazijawa documented.. Leo nitawapatia mkazisome kisha mje tujadiliane.

Kwa ufupi, jibu lako lipo hapa > Culture of Tanzania - history, people, clothing, traditions, women, beliefs, food, customs, family

Nyingine kiasi > Traditions and Customs Only People From Tanzania Will Understand

Ongezea na hizi > https://answersafrica.com/tanzania-culture.html

Mungu akijaalia siku moja nitaanzisha thread maalum kuzielezea.
Haahaaa!! Mkuu platozoom!

Interest kajipiga piga huku akijaribu kuelezea the so called culture and related stuff! Alidhani nitaona taabu kusoma!

Sasa wewe Interest, ni wapi kwenye hiyo link ya juu walipoelezea exactly what's Tanzanian culture? Copy hiyo para na paste hapa! Binafsi nimesoma kwa haraka na nikakutana na hili hapa:
Despite the tremendous cultural and linguistic diversity among Tanzanians, ethnic groups are united by the use of a common language—Swahili—and a sense of national identity.
Kumbe basi, wala hakuna hicho kinachoitwa utamaduni wa Mtanzania manake kilichopo ni cultural diversity and we're only united with Swahili!

Na Kiswahili chenyewe sasa, kwa mujibu wa hilo hilo bandiko lako tunaambiwa:
The influence of Islam and Arab culture is strongly reflected in the Swahili language.
Kumbe hata Kiswahili chenyewe kimejaa makando ya tamaduni za Kiislamu na Kiarabu! But all in all--

SWALI: NI kwa namna gani Kiswahili ambacho kinaonekana kama ndio utamaduni wenyewe wa Tanzania, is related to your discussion?

Sikuishia hapo, nikaenda kwenye link yako ya pili! Kabla sijafanya chochote serious, nikakaribishwa na:
Tanzania is a culturally eclectic and largely homogeneous society that is extremely rich in age-old cultures and traditions.
You tell me now: how many cultures and traditions do we have?!

REMEMBER, we're looking for Tanzanian culture and not cultures!

Hiyo link nyingine imeelezea tu the so called WEIRD Tanzanian culture!! Of all, hakuna hata moja related to your subject! Am I missing something here?!

Will you please try to dig deeper and come with something else :D:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D?!
 
Ni kweli ushoga ni kosa, je ni makosa mangapi umeshudia watu wakitajwatajwa hovyo? Kuvunja katiba ni kosa kisheria, kuua watu ni kosa kisheria, kuteka ni kosa kisheria, kukwepa kodi ni kosa kisheria, kufoji ni kosa kisheria, kuvunja mikataba ni kosa kisheria kusingizia ni kosa kisheria, je haya mengine hayana madhara isipokuwa ushoga?
Tume ziundwe hata kwa mambo ambayo husababisha kupoteza uhai.

Wengine wanadhani eti maadiko yanakataza na ni laana tusidanganyike; wizi,uasherati, uuwaji, uchawi uwabudu sanamu kutoheshimu wazazi nk zote huleta laana na tunaziona hapa nchini siyo kwasababu ya ushoga tu?
Akikujibu hayo maswali, naomba uni-tag tafadhali!!
 
Binafsi sipendi ushoga na namwomba Mungu sana hili swala nyumban kwangu lisiingie iwe kwa watt wa kike au wa kiume
 
Bado napambania maslahi ya Mama Tanzania!

Wizara ya Mambo ya Nje ilikuja na taarifa kuhusu Tanzania kutambua ushoga. Yaani, inaheshimu mikataba ya Umoja wa Mataifa ambayo inataka Haki za Binadamu zitambuliwe na kutekelezwa. Taarifa hiyo iliambatana na kusema haiitambui operesheni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda dhidi ya mashoga. Kwamba ni mawazo yake binafsi na sio msimamo wa Serikali!

Nimejipa muda kufuatilia. Sijaona mkataba wowote wa UN/Kimataifa unaotambua Ushoga kuwa ni sehemu ya Haki za Binadamu. Sasa huku kuufyata kuhusu ushoga kunatoka wapi?

Badala yake, nimeona Mikataba 2 ambayo inazungumza tofauti na hivyo.

1. Mkataba wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (the International Covenant on Economic, Social and Cultural Rights):
Kifungu cha kwanza cha makataba huu kinatambua haki ya kila jamii kujiamulia yenyewe bila kuingiliwa mambo yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni (Article 1: All peoples have the right of self-determination. By virtue of that right they freely determine their political status and freely pursue their economic, social and cultural development.). Ndivyo mkataba huu unavyosema. Sio maneno yangu!

Sasa iweje leo nchi yetu ilazimishwe kufuata mifumo ya uchumi ya wengine? Iweje leo tulazimishwe tuishi kwa mila za wengine? Kwanini leo tulazimishwe tuige utamaduni wa wengine? Kwanini huu mkataba hauheshimiwi?

Kwa kuzingatia mkataba huu tunayo kila sababu kama wanachama wa UN kukataa mashinikizo yote yanayoingilia uhuru wetu wa kujiamulia tuishije kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Wale wenye dhamana wawakumbushe hawa jamaa kuwa kuna mkataba wa UN unatupa haki yetu ya kuamua tuishije kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Ni mpaka hapo mkataba huu utakapofutwa ndio watakuwa na uwezo huo.

2. Mkataba wa haki za kiraia na kisiasa (the International Covenant on Civil and Political Rights).
Mkataba huu umetoa haki kwa mtu au binadamu mmoja mmoja. Hakuna kipengele hata kimoja kimempa mtu au binadamu uhuru wa kuingiliana kinyume na maumbile. Kama kipo naomba nionyeshwe. Hakipo! Na hakipo kwa kuwa mwaka 1966 mkataba huu uliporidhiwa watu hawakuitambui hii kama haki ya kijamii na ya kisiasa ya binadamu! Hata kwenye kifungu 23 haki hii haikutambuliwa.

Mkataba huu bado uko hai. Haukutambua ushoga, usagaji, kujibadili viungo kama moja ya haki za kiraia na kisiasa za mwanadamu. Mkataba huu umetambua ndoa ya watu wanaoweza kupata watoto. Mkataba huu umetambua familia kama muungano wa mwanamke na mwanaume wanaoweza kuzaa. Na hakuna mkataba wowote wa umoja wa mataifa ulioridhiwa ambao umehalalisha ushoga na hayo mengine. Hawa wanaodai ushoga, usagaji na uchafu mwingine ni haki ya binadamu wanatoa hoja yao kwenye mkataba upi wa UN?

Nijuavyo mimi, baadhi ya nchi zimehalalisha mambo hayo kwenye sheria za nchi zao. Tunalazimikaje kufuata maagizo yatokanayo na sheria ya nchi nyingine? Ni vyema wenye dhamana wawakumbushe kuhusu uhai wa huu mkataba. Wakitaka waufute kwanza. La sivyo wanakiuka mkataba wa UN kutulazimisha mambo ambayo hayapo kwenye huu mkataba!

Nimalizie kwa kuwahimiza vijana na wanadiplomasia wetu wajenge utamaduni wa kusoma kwa umakini mikataba ya UN ambayo ndiyo kila mara wapiga debe wanaitumia kutaka tufuate uovu.
Hakuna mkataba wa UN umehalalisha ushoga, usagaji na hayo mengine, yaani LGBT kwa ujumla.

NB: Bernard Membe alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje, aliwahi kusema walivyoenda kwenye Mikutano ya Umoja wa Mataifa, walijadiliana kuhusu Haki za Binadamu na kukubaliana mambo kadhaa. Suala la Ushoga halikuwepo kwenye ajenda na hata viongozi wa mataifa flani walipojaribu kuwashawishi (pembeni) wakubali kuitambua LGBT, waligoma.

Yaani nimeshangaa sana leo hii Serikali ya Tanzania kuingia kingi kizembe kwenye mtego huu!
Don't loudly make argument if you did't trouble to make research. Open this link: OHCHR | LGBT UN Resolutions
Also this link: OHCHR | LGBT UN Resolutions
 
Attachments

  • International-Human-Rights-Law.pdf
    85.7 KB · Views: 20
Na nyie nao tumewachoka na mada zenu za kijinga kila siku mambo hayo hayo hamna cha kuongea??

unaongea vitu viwili tofauti unaviweka katika kitu kimoja, umeshasema UN wanatetea Haki za Binaadam hapo hapo unasema wanalazimisha muukubali ushoga ndio nini sasa wapi walisema hayo?

Unasema washukiwa walitajwa wafikishwe mahakamani unaona kabisa hiyo ni haki?? unajua hao waliotajwa wamechafuliwa vipi status yao kwa jamii? wengine wana wake na watoto, wana wazazi na ndugu, wana mashabiki ambao kimsingi ni role model je watajisafisha vipi? siku hizi ushoga unapimwa kwa utanashati na kulamba lips? huko ni kuvumvunjia mtu haki yake na kumnyanyasa na kumnyongesha katika nchi yake mwenyewe ndio hicho wanachokipigania UN na mataifa mengine, kwanini hamuoni hili??

Wewe baba yako akitajwa kua ni shoga utashangilia apelekwe mahakamani? au kwa vile waliotajwa hawakuhusu ndewe wala sikio?

Tunarudi na nini shida mtu akiwa shoga? mimi ni lesbian, ninafanya kazi, nalipa bills, nalipa kodi, naipenda familia yangu na watu wote, kipi labda kilichobadilika kwa mimi kua lesbian kwenda kwa jamii?? faragha yangu mimi inaathiri jamii kwa nyanja ipi?? je mtu akiwa jambazi au mchawi wanaweza kua sawa na gay au lesbian?

Uongozi wa Jf ifike muda sasa mada hizi wawe wanazifuta au zianzishiwe special thread mtu akiwa na dukuduku lake anaenda kutupia huko maana mnatukera sasa kama kueleweshwa watu wameeleweshwa ila mtu hataki kufungua mawazo yake kakomaa na kile alichokiingiza kabla.
Again, MNAKERA.
 
Sasa kwani nimesema wasilindwe? Hata muuaji anapaswa kulindwa, sio shoga tu.

Lakini kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ni wajibu wa mamlaka kwa sababu sheria zetu zinatambua ushoga ni kosa/iuhalifu.

Mikataba ya UN niliyoiweka kwenye thread pale juu unaizungumziaje?
unatumia njia gani kuwajua mashoga? utawakamataje bila kuwajua?
 
Binafsi sipendi ushoga na namwomba Mungu sana hili swala nyumban kwangu lisiingie iwe kwa watt wa kike au wa kiume
Lea watoto wako kwa kutumia nidhamu kali siyo mtoto wa kiume unamlea kama mwanamke aidha mtoto wa kike usimuhamasishe kuvaa na kupenda mambo ya siyo na maadili!
 
Sheria ipo ndio ila kabla haijakukamata na kuthibitisha kama unafanya huo mchezo wala haina mamlaka ya kukutuhumu. Sasa kilichokuwa kinafanyika ni tuhuma tu na hili linamanisha ni kwenda kinyume na haki za binadamu.

Mfano mzuri kama wewe ukitajwa kama shoga na ukabisha unaelewa nini kinaenda kufanyika?

Je uyo aliekutaja una uhakika upi kama yeye si shoga?

Hivyo hili swala lina mlolongo mkubwa sana by nature, kuna watu nimesoma nao yaani walivyokuwa wanaishi ni kama watoto wa kike lakini sikuwahi sikia au shuhudia hayo mambo kwao, wengine homoni tu na mengine mengi tu.

Hebu tuongelee hili kwa imani zaidi, Makanisani na msikitini hawaruhusu kabisa uzizi, ulevi au ushoga na sheria zao zipo wazi kbs lakini ulishawahi ona watu wanatolewa nje zaidi ya kupewa onyo otherwise ukaidi onyo zaidi na zaidi, Hukumu anaitoa mungu peke yake. Sawasawa na serikali hukumu inatolewa na mahakama tena baada ya uthibitisho wa kutosha.

Mimi kama kiongozi, katika kuilinda sheria na katiba yangu nilipaswa kuwakumbusha watu juu ya swala hilo kama ni kinyume na taratibu za nchi na mtu/watu kutojihusisha nayo na atakaekamatwa atahukumia kadiri sheria inavyosema ila siyo ule upuuzi. No one anapenda ushoga utendeke ila ukweli lazima usemwe.
 
Tuliambiwa twende shule na tuwe serious na shule.

Ok so wakati 1st, 2nd na 3rd generation zinapitishwa na serikali yetu ikakubaliana nayo ilitakiwa imaanishe nini?

Siyo ilitakiwa kumaanisha kwamba inazitambua haki zote ambazo hizo generation zilioffer?

Hizo haki zinajumuisha mtu kua na maamuzi yake. Ambayo hayakua specified ni maamuzi gani.

Now haki hupingwa na haki nyingine au na sheria.

Serikali yetu ilikua smart, ikaazimia kwamba ok wewe jioneshe tu kua unapakuliwa ila sheria yetu inasema usifanye hiko kitendo kwakua kukifanya ni sawa na kufanya mapenzi na mnyama. Hivyo ikionwa ushahidi unajitosheleza basi utafungwa miaka 30 au maisha.

Tulisaini mikataba ya ushoga? Hapana. Tulisaini mikataba ya kuruhusu free expression? Ndiyo.
 
Bado napambania maslahi ya Mama Tanzania!

Wizara ya Mambo ya Nje ilikuja na taarifa kuhusu Tanzania kutambua ushoga. Yaani, inaheshimu mikataba ya Umoja wa Mataifa ambayo inataka Haki za Binadamu zitambuliwe na kutekelezwa. Taarifa hiyo iliambatana na kusema haiitambui operesheni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda dhidi ya mashoga. Kwamba ni mawazo yake binafsi na sio msimamo wa Serikali!

Nimejipa muda kufuatilia. Sijaona mkataba wowote wa UN/Kimataifa unaotambua Ushoga kuwa ni sehemu ya Haki za Binadamu. Sasa huku kuufyata kuhusu ushoga kunatoka wapi?

Badala yake, nimeona Mikataba 2 ambayo inazungumza tofauti na hivyo.

1. Mkataba wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (the International Covenant on Economic, Social and Cultural Rights):
Kifungu cha kwanza cha makataba huu kinatambua haki ya kila jamii kujiamulia yenyewe bila kuingiliwa mambo yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni (Article 1: All peoples have the right of self-determination. By virtue of that right they freely determine their political status and freely pursue their economic, social and cultural development.). Ndivyo mkataba huu unavyosema. Sio maneno yangu!

Sasa iweje leo nchi yetu ilazimishwe kufuata mifumo ya uchumi ya wengine? Iweje leo tulazimishwe tuishi kwa mila za wengine? Kwanini leo tulazimishwe tuige utamaduni wa wengine? Kwanini huu mkataba hauheshimiwi?

Kwa kuzingatia mkataba huu tunayo kila sababu kama wanachama wa UN kukataa mashinikizo yote yanayoingilia uhuru wetu wa kujiamulia tuishije kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Wale wenye dhamana wawakumbushe hawa jamaa kuwa kuna mkataba wa UN unatupa haki yetu ya kuamua tuishije kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Ni mpaka hapo mkataba huu utakapofutwa ndio watakuwa na uwezo huo.

2. Mkataba wa haki za kiraia na kisiasa (the International Covenant on Civil and Political Rights).
Mkataba huu umetoa haki kwa mtu au binadamu mmoja mmoja. Hakuna kipengele hata kimoja kimempa mtu au binadamu uhuru wa kuingiliana kinyume na maumbile. Kama kipo naomba nionyeshwe. Hakipo! Na hakipo kwa kuwa mwaka 1966 mkataba huu uliporidhiwa watu hawakuitambui hii kama haki ya kijamii na ya kisiasa ya binadamu! Hata kwenye kifungu 23 haki hii haikutambuliwa.

Mkataba huu bado uko hai. Haukutambua ushoga, usagaji, kujibadili viungo kama moja ya haki za kiraia na kisiasa za mwanadamu. Mkataba huu umetambua ndoa ya watu wanaoweza kupata watoto. Mkataba huu umetambua familia kama muungano wa mwanamke na mwanaume wanaoweza kuzaa. Na hakuna mkataba wowote wa umoja wa mataifa ulioridhiwa ambao umehalalisha ushoga na hayo mengine. Hawa wanaodai ushoga, usagaji na uchafu mwingine ni haki ya binadamu wanatoa hoja yao kwenye mkataba upi wa UN?

Nijuavyo mimi, baadhi ya nchi zimehalalisha mambo hayo kwenye sheria za nchi zao. Tunalazimikaje kufuata maagizo yatokanayo na sheria ya nchi nyingine? Ni vyema wenye dhamana wawakumbushe kuhusu uhai wa huu mkataba. Wakitaka waufute kwanza. La sivyo wanakiuka mkataba wa UN kutulazimisha mambo ambayo hayapo kwenye huu mkataba!

Nimalizie kwa kuwahimiza vijana na wanadiplomasia wetu wajenge utamaduni wa kusoma kwa umakini mikataba ya UN ambayo ndiyo kila mara wapiga debe wanaitumia kutaka tufuate uovu.
Hakuna mkataba wa UN umehalalisha ushoga, usagaji na hayo mengine, yaani LGBT kwa ujumla.

NB: Bernard Membe alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje, aliwahi kusema walivyoenda kwenye Mikutano ya Umoja wa Mataifa, walijadiliana kuhusu Haki za Binadamu na kukubaliana mambo kadhaa. Suala la Ushoga halikuwepo kwenye ajenda na hata viongozi wa mataifa flani walipojaribu kuwashawishi (pembeni) wakubali kuitambua LGBT, waligoma.

Yaani nimeshangaa sana leo hii Serikali ya Tanzania kuingia kingi kizembe kwenye mtego huu!
Kwani enzi za Mwinyi, mkapa na kikwete mashoga na wasagaji hawakuwepo nchi hii? Kimetokea nini utawala wa awamu ya tano?
 
Msako wa mashoga si liliundwa jopo maalum kwa ajili ya kuwakamata washukiwa na kuwapeleka mahakamani? Hao waliofanya mob justice ndio wamekosea, siye aliyeunda jopo maalum.

Halafu let us be honest, unaamini kwamba hizi vurugu zinazoendelea ni kwa sababu ya hao jamaa kuwa concerned kwamba mashoga watakuwa harrased? Si kemeo tu lingetosha?

So, kwa logic yako, leo hii ikianzishwa operesheni ya msako wa machangudoa au wahalifu wengine, tutaambiwa tunakiuka haki za binadamu?! Na vyombo vya usalama vinavyofanya doria ya kusaka wahalifu mitaani wanavunja haki za binadamu?

Ushoga ni kosa kwa mujibu wa sheria za nchi. Anayejihusisha nao ni muhalifu kama wahalifu wengine.

Think kijana.
Tatizo hamjielewi huko lumumba, mashoga ni walipa kodi wazuri tu kwenye nchi zao hata kwetu huku, misaada yao na kodi mnapenda ila kuwalinda ndio mnaenda kinyume na mila na destuli zenu sio? Yaani unamwambia muumini usiuze gongo ni chukizo kwa mungu ila sadaka itokanayo na faida ya gongo unaipenda hutaki kujilidhisha kama imetokana na nn.
 
Ushoga ni kosa kwa mujibu wa sheria za nchi. Anayejihusisha
nao ni muhalifu kama wahalifu wengine.
Walikuwepo kabla ya uhuru wala hatujawahi kufikia hali hii, mnaharibu halafu mnataka tuungane tuwe wazalendo dhidi ya wazungu huo ni upuuzi
 
Hawajatulazimisha, tuna haki ya kufanya tunavyotaka ila tusiwashobokee tu. Ni kama nyumbani kwenu ukiwa hutaki kuendana na matakwa ya mzee anakata allowance ila hakukatazi kuishi. Mbona nchi tajiri hazina nongwa? China na Marekani hawawezi kuongelea huu upuuzi tukakope huko. HAMNA ANAETULAZIMISHA KUFANYA CHOCHOTE,
 
Hapana, hiyo haikuruhusiwa.

Ndio maana Makonda akasema kama mtu anamfahamu mshukiwa yoyote, majina yake yatumwe privately kwake. Na namba ya simu akatoa.

Hata Konki Masta alivyoanza kutaja ile list, Makonda akampiga stop na aliitwa Polisi kuhojiwa.
mkuu,
pia hii link Kwenye List ya MASHOGA, RC MAKONDA Awataja Bila Chenga JAMES DELICIOUS Na Wenzake! | YOUTUBE DOWNLOADER
hiki ndicho kitu ambacho watu hawakitaki..huu ni uvunjaji wa wazizi wazi wa haki za binaadam...kuna njia sahihi ya ku deal na hizi mambo lakini sio kuwataja watu hadharani hv....

tatizo mnaemtetea kaishia la 7
nafikiri wanasema "muungwana akikosea huchutama" basi jaribuni kuchutama kuliko kukaa humu mkitetea matumbo
 
Haki za binadamu ni kuwa bonadamu wote wana haki ya kuheshimiwa, kulindwa na kutambuliwa utu wao. Ndani ya haki za binadamu kuna aina zote za binadamu: wanawake, wanaume, watoto, walemavu, mashoga, watoto, wazee na vijana
 
Huu sio mkataba. Ni ripoti.
Halafu inawezekana aliyeweka hiyo report naye ni punga... watu wanatakiwa kujiongeza katika kufikiri. UN na hao wazungu wenu wanaongozwa na ILLUMINATI kwa kitu kinaitwa New World Order (NWO).. kwamba watu wote wasiokuwa illuminati hawana uwezo wa kufikiri wala hawatakiwi kuwa na utashi wa kufanya wanayayoyataka, bali NWO inavyotaka. Wazungu ni binadam hatari sana maana waliona walileta dini.. maboya ya kiafrika yakakubali ewaaah.. sasa mazungu yanaleta ushoga, lakini kwa wakati huu kwa njia ya blackmail.. kwamba kama hukubali misaada hakuna.

Kama nchi lazima ifike mahali tuwambie kwamba na sisi tuna haki ya kujiamulia mustakabali wetu wenyewe (right to self-determination).. hivyo watukome kabisaa na ushoga wao.
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom