BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,792
- 287,994
Mkataba wa TRL hauvunjwi ng'o !
17 September 2009
Majira
Waziri wa Miundombinu Dkt. Shukuru Kawambwa akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu azma ya Serikali kuboresha vipengere vya mkataba wa Kampuni ya RITES na Serikali ili kuepuka kuuvunja mkataba huo. (Picha na Charles Lucas)
*Waziri asema lengo ni kulinda mazingira ya uwekezaji
*Adai serikali inahofia fidia kubwa inayoweza kutozwa
*Pia inaogopa kuchafuliwa na mwekezaji nje ya nchi
*Hata hivyo akiri upungufu mkubwa wa mwekezaji
Imeandikwa na Benjamin Masese na Gladness Theonest
SERIKALI imesema kamwe haiwezi kuvunja mkataba wake na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ili kulinda mazingira ya uwekezaji nchini na kuhofia gharama kubwa inazoweza kutozwa endapo itachukua uamuzi huo.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Chama Cha Wafanyakazi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRAWU) na wadau wengine kutaka mkataba TRL uvunjwe kutokana na kusuasua kwa mwekezaji kampuni ya RITES kutoka India kuendesha reli hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Miundombinu, Dkt. Shukuru Kawambwa alisema kuvunjwa mkataba huo kunaweza kusababisha mwekezaji atakayefukuzwa, kuitangaza Tanzania vibaya nje ya nchi.
"Kuvunjwa mkataba wa TRL kutasababisha Watanzania kuingia gharama kubwa kulipa fidia wawekezaji hao. Serikali haiwezi kuvunja mkataba kirahisi kama wengi wanavyofikiria kwa sababu mkataba huu ni wa kimataifa unaohusisha nchi tatu, ambazo ni Tanzania, India na Msumbiji, hivyo badala yake ina uharaka wa kutenga fedha nyingi za kuboresha reli, hata kama mwekezaji ataendelea kuwepo.
"Umoja wa Mataifa una orodha ya nchi zinazovunja mikataba iliyosainiwa kihalali, tukivunja huu tutashtakiwa baadaye. Kama itahitajika kuuvunja, utakuwepo utaratibu maalum wenye maridhiano baina ya pande zote mbili. Huu ni mkataba wa kimataifa hautavunjwa kamwe!" Alisema Dkt. Kawambwa.
Huku waandishi wa habari wakionekana kuwa na hamasa kuuliza maswali juu ya kile kinachoonekana kuwa utendaji mbovu wa TRL, Waziri Kawambwa, alikiri kudorora huduma za reli hiyo tangu TRL ilipokabidhiwa jukumu hilo.
Alitaja kasoro zinazosababisha kudorora huduma hizo kuwa ni pamoja na matatizo ya kiuendeshaji na uwezo mdogo alinao mwekezaji huyo.
Pia alikiri kuwepo upungufu ya mtaji katika utekelezaji wa mkataba wa ukodishaji ambapo alisema hali hiyo imesababisha uhaba wa pesa ambazo zingetumika kufanyia matengenezo njia ya reli na kukarabati vyombo vya uendeshaji.
Akizungumzia uhalali wa ukodishwaji wa lililokuwa Shirika la Reli ya Tanzania (TRC), uliozaa wa sasa wa TRL, alisema Waraka wa Baraza la Mawaziri Na. 29/2006 uliruhusu utumike utaratibu wa ubia katika kuendesha na kugharamia TRL, kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya RITES kutoka India.
Dkt. Kawambwa alikiri kuwa mkataba huo una matatizo ambayo ni; TRL kutozingatia mkataba wa ukodishaji, uongozi wa TRL kutotekeleza makubaliano ya nyongeza ya mshahara wa kima cha chini kati yake na TRAWU.
Kuhusu uhalali wa RITES kuidai TRL injini na mabehewa na kuamua kusitisha matumizi ya vifaa hivyo, mpaka itakapolipwa dola za Marekani milioni 13.42, Dkt. Kawambwa alisema serikali haina habari na deni hilo kwani mkataba huo ni kati ya TRL na RITES.
Alisema serikali itaendelea kuikopesha TRL vipuli na vitendea kazi vingine. Alitoa rai kwa wafanyakazi na kuendelea kuchapa kazi kwa mujibu wa kanuni za ajira na kuacha kuingilia majukumu ya serikali ambayo ndiyo ilisaini mkataba.
"Nchi ni yetu sote lazima tufuate kanuni na utaratibu wa utawala bora, hivyo wasifanye maamuzi yoyote ya kuiondoa manejimenti ya TRL, wafanye kazi walizopangiwa.
"Wananchi wawe wavumilivu kwa kuwa hali ya sasa ya TRL ni ya mpito ambayo itarekebishwa na kupatiwa ufumbuzi wa kudumu," alisema Bw. Kawambwa.