Mkasa

Mkasa

Mahmood

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2008
Posts
7,908
Reaction score
2,480
Mama: Mwanangu hebu mpigie simu babako mwambie chakula tayari.

Mtoto: Sawa mama.

Mtoto: Mama simpati.

Mama: Basi subiri kama baada ya dakika 5 halafu mpigie tena inawezekana ni mambo ya network hayo.

(Baada ya dakika 5)

Mtoto: Mama mimi baba simpati, simu yenyewe anayepokea ni Mwanamke.

Mama: haaa!! sawa mwanangu niachie mimi suala Hilo, wewe nenda kale.

(Baada ya dakika 30 Baba akabisha Hodi..
Akakaribishwa na bonge la kibao hajakaa vizuri sufuria mara mwiko ikawa balaa, Mume yuko katika hali ya mshangao.. akazidiwa)
Majirani wakaja kuamulia ugomvi, Kufika Mume yuko chini ya sofa Hoi bin Taabani.
Mama: Pu-mba-vu zako wewe kunifanyia Mimi??? hivi ukaenda kwa malaya zako kuniachia mimi nyumba?

Mwanangu hebu waambie majirani yule Mwanamke Alipopokea alisemaje?

Mtoto: Alisema, SAMAHANI MTEJA WA NAMBARI ULIOPIGA, HAPATIKANI KWA SASA!!!
Hahahahah....

Ingekua wewe ni huyo Baba ungemfanyaje Mkeo???
 
Ingekuwa mimi ningempa zawadi mke wangu kwa kujua kwamba ananipenda kwa dhati hajapuuzia kujibiwa na mwanamke japo kuwa alikuwa hajaelewa
 
Mahmood Ningecheka sana na maumivu yote yangeisha.
 
Last edited by a moderator:
ha ha ha ha ha ha ha !!!!!!!!!! nimeongeza siku za kuishi
 
Hapa unageuka na riteke ra nguvu na kama risime riko chirani unapiga mutu bapa na unamuwekea arama ya maisha Mura. Hapana chesea mume bhana.
 
Ningemng'oa meno yote ya sebuleni afu ningemkumbatia na tabasam....teh teh teh
 
kudadeki! mtoto pwagu mama pwaguzi. natembezea kichapo heavy kwao wote!
 
Ningejifanya sija mind,majirani wanaondoka.Usiku valangati kwa mama na bintiye
 
Back
Top Bottom