Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 4,188
- 9,165
Wadau huu ni mkasa wa kweli kabisa miaka kumi na nne imeisha lakini Bado majeraha hayakauka. KISA kinaendelea;Miaka hiyo nilipewa uhamisho kikazi Mkoani rukwa nikiwa Sina mke. wala Mwana. Nilipoambiwa naenda kwanza niliogopa kwenda lakini wenzangu walinambia nisihofu huko ni kama mikoa mingine muhimu nijiheshimu. Sikuwahi elewa maana ya neno kujiheshimu Hadi siku yaliponifika nikakumbuka na kuelewa rafiki yangu alimaanisha nini. Nilikuwa Sina nyumba ya kupewa na mwajiri wangu nilipanga maeneo ya Jirani na ofisi yangu. Namshukuru Mungu nilipewa makaribisho mazuri sana na mwenyeji wangu Mzee mwenye hekima na aliyekuwa akipewa heshima kubwa na wenyeji. Mzee huyo alikuwa na mkewe ambayealikuwa bado mdogo sana labda kwakuwa alikuwa Bi Mdogo. Wenyeji wangu hao walikuwa na mabinti wawili.mapacha ambao walifanana sana kwa sura yaani identical twins na kwa urembo pamoja na mienendo Yao.Nilianza maisha mapya kwa kupewa maelezo muhimu kuhusu mkoa huo na siku za mwanzoni nikishiriki chakula pamoja na familia wakinipa heshima ya ukaka. Ukweli nilijisikia vema sana na Ile hofu yangu ikaanza kuondoka. Mzee huyo alinikubali sana ndani ya muda huo mfupi. Mkewe naye alinipenda kama ilivcyokuwa Kwa wanae mapacha. Nilanza kazi baada ya kupokelewa na kupewa abc za wafanyakazi wenzangu ambao walipokea vizuri kabisa. Maisha yalikuwa mazuri na nilimshukuru. Mungu wangu