Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,360
- 11,588
>UPDATES: Imeendelea kwenye reply #36
Kwanza kabisa nianze kwa kuwasalimu wale wote mliosoma katika shule za boarding kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... ama kweli, tuliupiga mwingi! Nilisoma shule moja ya kibabe inayopatikana mkoani Kilimanjaro, Kuna kitu kinaitwa Interschool Bush!
Basi bhana! Sherehe ikapangwa, usiku wa siku ya kesho ya sherehe watu waliandaa kodi zao, waliofahamiana na viongozi walikimbizana ofisini kwa ajili ya kuzinyoosha nguo zao! Kundi jingine la wanafunzi lilimwelekea Waziri wa Social kwa ajili ya kujipatia kuponi kwa shilingi elfu nne tu! Wakina sisi tulioiota kesho yetu tulikuwa kwenye darasa mojawapo kwa ajili ya kuendelea na liheso ili siku ya kesho yake watu wapate mtumbuizo wa namna yake kutoka kwetu! Dancers walifanya mazoezi yao kama kawaida!
Siku ya kesho yake mida ya saa tatu hivi, hiace nne ziliingia shuleni hapo, kisha sketi za kupendeza kwa sura, shape na mavazi ziliteremka kwenye hiace tayari kuelekea mapokezi! Walikuwa ni warembo haswa! Mamen ambao walikuwa wagumu kutoa mchango walining'inia madirishani kwenye floor za ghorofa za aggrey kuona kama wataupunguza ugwadu kwa macho! Huku wengine waki save images za watoto wale wazuri ili ziwasaidie hapo baadae!
Case study, tumzungumzie binti mmoja tumpe jina la Catheline ambae nahisi ndo alikuwa mzuri kuliko wote, mwenye kisauti fulani hivi cha mahaba, shape lake sijaona kwa star yeyote hapa bongo, trackle mbinuko na kamwili fulani hivi, mtoto ambae babae ni mrwanda na mama yake ni mtanga! Binti huyo alipokelewa na rafiki yangu, tumpe jina "M" ,kwa ucheshi wake akawa kanipiga gap, nikaamua kuachana na Catheline na kutafuta mwingine! Basi bhana sherehe ikafana mpaka muda wa kuperform nikapanda stagin nikaporomosha verse!
Watu walishangilia uimbaji wangu na sauti tamu iliyoshusha melody nyingi zaidi ikiwa ni pamoja na Iyola ya Harmonize! Baada ya hapo, nilitoka nje ya ukumbi huku nikisindikizwa na macho ya warembo waliokuwa kwenye seat na mabasha wao! Nikasogea fish pond nikawa nimetulizana huku nakunywa maji yangu baridi! Dakika si nyingi, Mwalimu mmoja, labda tumpe jina la Benteke, alisikika akisema,"Wageni mnaruhusiwa kutoka nje walau kuangaza mazingira ya shule yetu!
Chonde Chonde, tusione mgeni yeyote akielekea maeneo ya nyuma ya shule ama sehemu hatarishi kwa afya yake" Baadhi ya wasichana walikuwa wakitoka nje wakimpuuza mchekeshaji aliyekuwa stegin anachekesha huku anatia huruma, labda tumuite Rostam ili tusijichanganye mbele ya simulizi!
Ghafla bin vuu, sauti ya mwanadada iliskika maskioni kwangu, mwanadada ambae hakufunga vishkizo viwili vya shirt yake nyeupe peee iliyonyooshwa na pasi ya gesi! huku mwili wake ukisambaza harufu ya kuvutia ya aroma, kisketi chake kifupi kilichoyaacha mapaja yake nje bila kuyahurumia! alinisogelea kisha kunitizama usoni, macho yake yalikuwa meupe pee yenye kulialia.
Kabla ya kuongea chochote alivua cheni yake iliyokuwa na letter C kisha kunivisha shingoni kwangu, akasogeza kiti mbele yangu akavishika viganja vyangu kwa viganja vyake, ndipo nilipomuona Mzabzab kwa mbali aliyekuwa anakuja upande wetu huku amefula hasira kali kwa ajili ya kuliamsha tifu katika shule yetu hiyo ya kibabe!
Narudi sasa hivi kuendeleza kisa...
>UPDATES: Simulizi imemalizikia kwenye reply #49