MWANAMASOKO
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 213
- 94
NILIWALIZA NAMI NIKALIZWA
Wewe uliwaliza nawe ukalizwa ,unamaanisha nini?Robin alikuwa anamuuliza rafiki yake amfafanulie maana ya maneno aliyoambiwa na rafiki yake huyo anayeitwa Frank.
Dah Robin ni story ndefu mno yaani niliwaliza kweli kweli nami nika\lizwa haswa.Alisema Frank.
Oya acha kunichanmganya,nieleze nini maana ya hayo maneno?Alifoka Robin.
Aha tulia kaka,naona una hamu sana ya kujua kilichojili mpaka unafoka?Haya ni hivi,,,,,,.
Mwaka 2000 nilimaliza kidato cha sita shule ya sekondari Azania na kupata alama za juu sana katika mitiani ya taifa na kuwa Tanzania One almaarufu kama T.O nikimaanisha mwanafunzi aliyepata alama za juu mno kuliko wanafunzi wote kwa mwaka huo.Nilifurai sana \nilipotangazwa kuwa T.O .Wale wengine walioingia tatu bora tulikwenda kuonana na Mheshimiwa Raisi pale Ikulu na kutupongeza sana na kutupa zawadi mbalimbali na kututaka kila mmoja achague nchi anayotaka kwenda kusoma masomo yake ya elimu ya juu nikimaanisha masomo ya chuo kikuu.Wenzangu wakataja nchi wanazotaka kwenda ila mimi nikamwambia kuwa nataka kubaki hapa hapa bongo.Alinishangaa sana na kuniuliza kwa nini nataka kubaki bongo na sitaki kwenda kusoma nje ya nchi kama wenzangu.Nikamwmbia mimi ni mzalendo siwezi kuiacha nchi yangu na kwenda kusoma nje,nikifanya hivyo ni kama nimeizarau elimu inayofundishwa hapa nchini.Nikamweleza mbona elimu ya sekondari sijasoma nje ya nchi lakini nimesoma hapa hapa bongo na kuweza kuongoza kitaifa hivyo elimu ya hapa bongo ni nzuri na waokimbilia nje ya nchi ni malimbukeni na wanakwenda kuwa watumwa wa elimu za nchi nyingine.Mheshmiwa Raisi aligwaya kwa jibu nililompa,akulitegemea kabisa.Akainuka kwenye kiti na kunifuata na kunikumbatia na kusema WEWE NI MZALENDO WA KWELI NA KUANZIA SASA UTAKUWA MSAIDIZI WANGU NDANI YA IKULU HII HUKU UKIENDELEA KUSOMA.UTAPOKEA MSHAHARA MNONO KILA MWEZI NA UTAPEWA NYUMBA NA GARI LA KUTEMBELEA LA KIFAHARI HUKU UKIFANYA KAZI HAPA IKULU. Nilifurahi sana kuambiwa vile hata wenzangu walinionea wivu.
Nikaanza masomo chuo kikuu cha Dar es salaam nikisomea sheria.Nilikuwa mwanachuo pekee niliyekuwa naingia na gari ya kifahari chuoni mle.Jina langu likapaa na kuwa maarufu sana ukizingatia mimi ndiye nilikuwa T.O hivyo nikawa nazungumziwa kila mara,kila nilipokuwa napita nikawa naitwa Tanzania One wengine wananiitaT.O mpaka nikayazoea hayo majina.Kama kawaida yangu nikawa naliongoza darasa langu kila mitihani tuliyokuwa tunafanya kwani nilikuwa na usongo sana nisome kwa bidii ili nimfuraishe mheshimiwa Raisi kwani ameshanipatia kazi na mara kwa mara nilikuwa nipo Ikulu nikiwajiba kwa kazi nilizokuwa naagizwa nizifanye huku nikiwa kijana mdogo kuliko wote kwa watumishi wa mle ikulu.Sifa zangu zikaenea kila mahali chuoni na wakajua kuwa nafanya kazi Ikulu.Hapo sasa fujo zilipoanza,mhadhili wa kike anayenifundisha akanipenda sana,akanishawishi kwa kila hali nimkubalie kwani na mimi sikuwa najiusisha na mapenzi toka utotoni yaani wenzangu walikuwa wananitania mimi ni bikra wa kiume.Ukizingatia mhadhili yule ni mzuri na mrembo sana ingawa alinizidi miaka nane mwishowe nilishindwa kukwepa vishawishi vyake tukawa wapenzi.Aha nilipoonjeshwa utamu wa mapenzi nilipagawa mtoto wa kiume.Muda wote nikawa nawaza mapenzi tu.Nikawa mimi na mapenzi,mapenzi na mimi.Huku nikiendelea kimapenzi na mhadhili wangu wanachuo wa kike nao wakawa wanajileta wenyewe kutoka kila kozi iliyofundishwa chuni mle.Mwanaume sikujivunga nikawa nawala kama sina akili nzuri.Mhadili wangu alipogungua kuwa mimi ni kicheche alilia sana na kila aliponiambia nitulie nae nikawa namjibu kuwa yeye kashazeeka wacha mimi nile damu changa zenye umoto umoto.Alinivumilia lakini mwishowe aliniacha baada ya kugundua kuwa natembea na mlezi wa wanafunzi.
Wanachuo wa kike waliokuwa wakjileta wenyewe nikawa nawabadilisha kama nguo na kila mara fumanizi lazima litokee.Walikuwa wanapigana wenyewe kwa wenyewe mpaka wanapasuana na kupelekana polisi wakinigombania.Wasichana wengi walikuwa wakinililia sasa sikujua walikuwa wananipenda kweli au walitamanishwa na mali na umaarufu wangu.Nilitembea na wanafunzi mpaka nikawachoka na kuanza kutoka na majimama au mashangingi kama yanavyoitwa .Aise huko napo nilidatishwa,majimama matamu bwana tena yanajua mapenzi balaa na ukiwa dogo dogo utalelewa kama mtoto mchanga.We niliwabadili na walikuwa wananililia kama mimi Mungu vile ili nisiwaache lakiniwapi kila mara nilikuwa natafuta jimama lipya.Nikiwa chuoni mwaka wa mwisho nilikutana na msichana mmoja chotara wa kisomali na mwarabu akiwa mwaka wa kwanza weeeeeeeeeeee kaka mtoto alikuwa mzuri sijapata ona maishani mwangu.Wala yeye hakunipapatikia kama wenzake bali mimi ndo nikampapatikia.Kwa mara ya kwanza nikampapatikia msichana toka niyaanze mapenzi.Mtoto wa kike akajifanya mgumu lakini mwishoew nikamweka himayani mwangu.Wacha nijilie mautamu kaka yaani sitomsahau yule binti mhm aha mapenzi matamu bana.Yule binti baada ya miezi sita akaumwa ghafla na kufariki.Nililia sana kwa kufariki kwake ,Baada ya mwezi nikaanza kuumwa sehemu zangu za siri.Zilikuwa kama zinaoza na kuuma sana,nililia mpaka nikawa napoteza fahamu,niliangaika kila hospitali hapa bongo lakini sikupona.Sehemu zangu za siri zikawa zinazidi kuaribika ni kama embe lililoiza na kuanza kuoza na kutoa funza.Mheshimiwa Raisi ndiye aliyenipeleka Uingereza nikatibiwe baada ya kupewa taarifa zangu.Uingereza nikatibiwa kwa miezi miwili ndo nikapona na kurejea bongo.Nilipofanya uchunguzi nikagundua ugonjwa ule niliambukizwa na yule chotara wa kisomali na ndo uliomuua huo ugonjwa kwani wa kwake ulikuwa umekomaa sana kiasi kwamba ukashindikana kutibika.Nilizani nimeambukizwa na ukimwi lakini nilipopimwa Uingereza nikaonekana sina ukimwi.Daah kaka sikuwa na hamu tena na wanawake toka nilipopona.Ikanibidi nirudie mwaka wa mwisho lakini chuo kingine kwani nilikuwa naona aibu kutokana na habari zangu kuonea sana pale chuoni UD.Niliamia Mzumbe ndipo nilipohitimu shahada yangu ya kwanza ya sheria.Baada ya kuhitimu siku moja nikiwa na Mheshimiwa Raisi nyumbani kwake aliniomba nimsimulie kisa cha kusababisha mimi kuumwa vile ndipo nilipomsimulia.Nilipomaliza akaniambia WEWE ULIWALIZA NA WEWE UKALIZWA. Hiyo ilitokana na machozi yaliyokuwa yanawatoka wale wasichana kwa ajili yako wewe ukiwatenda ndivyo sivyo.Hivyo ni kama laana ya wasichanaa juu yangu ndiyo iliyosababisha mimi kuumwa vile na ningetakiwa kufa kabisa sema Mungu tu ndo ameninusuru.Alisimulia Frank.
Aise pole sana Frank lakini nadhani umepata fundisho hivyo ukome kuwatenda vibaya wanawake kisa mali na umaarufu wako.Alisema Robin.
Nilishakoma, nimekoma na nitaendelea kukoma ama kweli ukitenda ubaya utalipwa ubaya na malipo ya ubaya ni hapa hapa duniani,duu niliwaliza nami nikalizwa sina hamu mie mweee.
MWISHO.
The Marketer.