Mkasa wa kusikitisha sana na tafsiri ya viongozi wetu-ubungo

luckman

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,211
371
Nchi yetu kamwe haiwezi kuendelea kwa kuwa na viongozi wa sampuli hii, tumekuwa tukihimiza utawala wa sheria na uwajibikaji

Ni juzi kati wakati dada mmoja anatoka zake Zanzibar, kafika bandarini Dar es salaam, aliposhuka akaamua kukodi tex, wakati anaingia kwenye gari, dereva wa tax akazunga kutafuta abiria wengine ili wawe wengi na gharama zipungue kumbe dada wa watu anaingizwa mkenge! baadae kama kawaida dereva aliwapata abiria wengine wawili wanaume ambao kimsingi walikuwa ni watu aliopanga nao kwa ajili ya kufanya unyama waliokuwa wameupanga!

Gari liliondoka na kuelekea kuelekea barabara ya alihasan mwinyi, dada alikuwa anaelekea makongo, gari lilipofika maeneo ya mlimani city wale abiria wawili wa nyuma walimbana dada ili asipige kelele na dereva akshika njia ya changanyikeni, walipofika lango la chuo njiapanda ya kuelekea msewe hadi baruti pale msituni walimtupa dada nje huku akiwa amenyanganywa kila kitu, Mungu si athumani wakiti wanamtupa na kutokomea akatokea bodaboda, dada akaomba msaada wakaanza kulimimbiza gari, walilifata kwa kasi na kufika maeneo ya msewe primary gari liliishiwa mafuta na kuzima, bahati nzuri wakati linazima na yule dada na bodaboda wakawa wamefika na kuanza kupiga kelele

watu walijaa na kuwakamata wale majangiri, afisa mtendaji wa eneo hilo bwana Jafari Nyaigesha akawa amefika na kuwaamuru watu wawe wapole, kweli watu walitulia na kuwachukuwa wale majambazi hadi ofisini kwa mtendaji, wakati wapo mle ndani watu walishikwa a butwaa baada ya wale majangili kumuita kwa jina bwana jafari! kumbe ni watu wanaojuana sijui kwa lipi lakini wanafahamiana.

watu walipoona hivo wakaanza kupiga kelele, kweli walienda kwenye gari na kutoa mizigo ya dada na pesa zote shilingi 40,000/= na kumrudishia yule dada, dereva alianza kudai yule ni mpenzi wake na wamegombana baadae wale majangiri waliagiza mafuta na kujaza kwenye gari, wakampa bwana Jafari sh 8,000.00 nayeye akanunua soda na kuwapa watu waliokuwepo ofisini na kuwomba yaishe huku dada akilia mithili ya mtoto mdogo kwani pamoja na maelezo yote aliyoyatoa hakuna aliyemjali

mwisho wa yote wale watu waliondoka kimchezomchezo tu huku mtendaji akiwaacha na kuwaomba watu waachane nao,
Huyu ni mtu anayeasume madaraka ya rais katika kata yake, ni mtu anayetakiwa kutekeleza sheria ya nchi, ni mtu anayetakiwa kushirikiana na polisi kuwasaka majambazi cha ajabu anashirikiana na majambazi kuwwangamiza raia wema wasiokuwa na hatia, John Mnyika haya mambo yamefanyika kwenye jimbo lako, naomba ufatilie huu mkasa, afande wa kanda maalum, naomba uingilie kati na umfatilie huyu mtendaji aseme hawa watu ni wa wapi na inawezekana ni kazi yao na wanampa fungu kwa ujangiri wao ambao unalindwa na ofisi za serrikali! wananchi wanaitafsiri vp serikali ambayo inaendeshwa kwa kodi zao?

Huyu mtendaji amekuwa kimbilio la majambazi na wahuni, anazo siri nyingi sana na akibanwa barabara atasema unless serikali iwe inajua na inasupport matendo yake!, nawasirisha
 
Kuna tatizo lazima serikali ishughurikie tatizo hili!huyu mendaji aeleze hawa watu wako wapi?
 
Tunatoa taswira gani kwa wananchi juu ya uongozi huu na serikali yao?
 
Dada ungetakiwa kwenda polisi moja kwa moja siyo kwa mtendaji ile ni njia ya kupitia,ofisi hiyo haina mamlaka makubwa kiasi hicho
 
Mmmh! Mnyika pls tengeneza jina nafasi yako katika Jimbo through this point!
 
Kweli kabisa ina bidi mtendaji huyu ashughulikiwe kabisa.

Huu ni udhaifu mwingine.
 
Kweli kabisa mngelilichoma hilo Taxi na kwani wanaongezeka abirua wa2 kiti cha nyuma asipige kelele?
Nampa pole na iwe fundisho km ni kweli arudi kituo chochote cha Polisi ashtaki Bodaboda ipo, Mtendaji Jafaru Nyagesha yupo na Taxi mtaikuta paleoale Bandarini wachukuliwe hatua
 
1. Kule golana Msewe uongozi huu umekula 60,000,000 + za mradi wa maji wa GODI
2. Police Post ya msewe imechukua miaka ~20 kukamilika, hii ni baada ya Juhudi za Mnyika na Diwani wake
3. Juzi kuna kijana amepigwa risasi, kuna harufu ya huyu kuhusika
4. Songas wanatoa pesa kwa huyu, hazijulikani ziendako (Watu wanalalama)
5. Haijawahi kutokea, mapato na matumizi ya serikali ya huyu jamaa kusomwa, miaka 15 hivi.
6. Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi, imefutwa bila ridhaa ya mlalamikaji.
7. Kuhusu mambo ya kuhodhi majambazi, polisi waangalie kama huyu jamaa hana matatizo huko. TISS wangekua serious wangejua mengi zaidi kwa manufaa ya umma.
8. Kuna minara ya simu Msewe, fedha hazieleweki zinalipwaje?
9. Kuna malalamiko kuhusu daraja la mzee kimolo, Msewe bondeni, Pesa zimeliwa (Wanakijiji wanalalama)
10.Yapo mengi yalishaandikwa magazetini, na ameshitaki baadhi ya magazeti, lakini?


Kwa kifupi, huku hatuna serikali ya mtaa. Kuna Mzee mmoja anaitwa Komba na Mtendaji ndio watuhudumia, na wana ustaarabu

Kama anabisha aitishe mkutano wa wananchi wote wa Msewe aone cha moto. kawaida huwa anaitisha vikao vya wananchi kwa mbinu ambazo hukwaza mahudhurio. Mfano kuwatangazia baadhi tu ya watu, au kuitisha ghafla Nk. Kuna mtandao unamsaidia. Hawa ndio wanaua CCM Msewe.
 
Hii ni habari ya kumpelekea Kova moja kwa moja, ili sheria zichukue mkondo.
Huyu hawezi akawa anatumwa ni tabia yake atakuwa anaasili ya ujambazi..!
 
Hii ni habari ya kumpelekea Kova moja kwa moja, ili sheria zichukue mkondo.
Huyu hawezi akawa anatumwa ni tabia yake atakuwa anaasili ya ujambazi..!
Kama kuna mtu ana uchungu na huyu jamaa ni watu wa Msewe. Anayebisha itisheni uchaguzi wa serikali ya mtaa huu na msimamie vizuri muone matokeo. Hizo tuhuma mbona zimezungumzwa sana huko nyuma. Jamaa anapeta tu, si CCM bwana.
 
Kwani huyo mtendaji angewafanyanini raiaya kama wangeamua kuwakamata hao wezi na kuwapeleka kituo cha polisi??
Viongozi wa sampuli hiyo ni action ndo zinawafaa, maneno matupu hayasaidii.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nchi yetu kamwe haiwezi kuendelea kwa kuwa na viongozi wa sampuli hii, tumekuwa tukihimiza utawala wa sheria na uwajibikaji

Ni juzi kati wakati dada mmoja anatoka zake Zanzibar, kafika bandarini Dar es salaam, aliposhuka akaamua kukodi tex, wakati anaingia kwenye gari, dereva wa tax akazunga kutafuta abiria wengine ili wawe wengi na gharama zipungue kumbe dada wa watu anaingizwa mkenge! baadae kama kawaida dereva aliwapata abiria wengine wawili wanaume ambao kimsingi walikuwa ni watu aliopanga nao kwa ajili ya kufanya unyama waliokuwa wameupanga!...

Diwani tunakuomba ufuatilie habari hiii.
 
Kwani huyo mtendaji angewafanyanini raiaya kama wangeamua kuwakamata hao wezi na kuwapeleka kituo cha polisi??
Viongozi wa sampuli hiyo ni action ndo zinawafaa, maneno matupu hayasaidii.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Kwani hajawahi kuita Police haohao kuvuruga mkutano wa wananchi Golani akashindwa? Lakini nakubaliana na wewe, bahati mbaya wenye msewe hawakuwepo?
 
Sehemu hizi za pembezoni mwa mji kuna watendaji mamluki wengi tu.
Mbezi Jogoo kuna jamaa anaitwa Juma Munanka, huyu vile vile ni kibaka kwa jina la mwenyekiti wa serikali za mitaa.
Anashirikiana sana na wahalifu pamoja na kuuza maeneo ya wazi.
Hata polisi wanamfahamu huyu lakini kwa vile kavaa ngozi ya serikali hachukuliwi hatua yotote.
 
Serikali ina udhaifu mkubwa sana, sio haya tu ni mengi huyu jamaa anafanya, kipindi cha nyuma kulikuwa na ulizi shrikishi yaani sungusungu, watu wakikamatwa usiku hata hawajulikani wanadai apigiwe simu Jaffary, wakimpigia anasema huyo mwachie namfaham mchezo ukawa uleule, namwisho watu wakakata tamaa na kuacha kabisa! Naomba vyombo vya usalama, ka hawahusiki, wamtumie huyu mtu anajua mambo mengi sana yanayotendeka na yeye anapata mgawo thats why amekuwa kimbilio la majambazi na vibaka!
 
Serikali ina udhaifu mkubwa sana, sio haya tu ni mengi huyu jamaa anafanya, kipindi cha nyuma kulikuwa na ulizi shrikishi yaani sungusungu, watu wakikamatwa usiku hata hawajulikani wanadai apigiwe simu Jaffary, wakimpigia anasema huyo mwachie namfaham mchezo ukawa uleule, namwisho watu wakakata tamaa na kuacha kabisa! Naomba vyombo vya usalama, ka hawahusiki, wamtumie huyu mtu anajua mambo mengi sana yanayotendeka na yeye anapata mgawo thats why amekuwa kimbilio la majambazi na vibaka!

Tatizo kuna wakubwa wanamlinda, lakini kuna siku yataisha, huku msewe wanaishi binaadamu sio kuku.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom