mnajipa majukumu yasiyo yenu kabisa, kwanini usitumie garama hiyo na muda huo kujitafutia maendeleo yako, sasa umepata nini mkuu
mnajipa majukumu yasiyo yenu kabisa, kwanini usitumie garama hiyo na muda huo kujitafutia maendeleo yako, sasa umepata nini mkuu
Ulishindwa kutumia huo muda kumwambia jinsi ulivyo vutiwa nae?
Wewe ndio umeharibu kabisa kwa uoga wako na kuhakikishia angekupenda hivyo hivyo sema umeshindwa kujiamini kwa mbwebwe alizo kuja nazo...! Pole sana uoga umekuponza.
Kuna mdada alikuwa anachangia sana humu JF, nilitokea kupenda sana uandishi na michango yake na nikajikuta naanza kumPM. Alikubaliana nami na tukapanga siku tukutane, alikuja na usafiri wake mpaka pale tulipoahidiana tukutane, lakini yeye alitangulia kufika kabla yangu.
Mimi nilifika baada kama dakika ishirini hivi kwa usafiri wa daladala.Nilipofika nilimkuta kaagiza kinywaji na akaniambia na mimi niagize chochote ila nilimkatalia kwa sababu nilikuwa nimebakiwa na 3000 tu ya nauli. Basi akaniuliza vipi mbona umechelewa kufika? Nikamjibu ninapoish ni mbali kidogo, akaniambia sawa na pole sana.
Basi baada ya muda na kupiga stori nying akaniaga akaniambia nataka kuondoka nawahi nyumbani na mimi nikamjibu sawa. Basi wakati anaondoka nilijua atasubiria boda boda, kumbe ana mgari aina ya V8, akaingia ndani akawasha akaondoka.
Wallah sikumpigia tena simu kwa sababu mimi sina hata baiskel na wa magari nitawaweza, nikasema bora aende zake maana akija kwangu ninapoish na jinsi kulivyo ataniaibisha JF zaidi.
mjomba confidence iliisha baada kuona sipo vizur kiuchum
Uoga wako ndio umasikini wako, maana inaonyesha hujiamini kwa kila kitu.
Nikweli na nilivyoandika hapo ni vichache ving nimeviacha,namuona humu jf ila namuogopa sana
Demu wa Jf atembelee V8 huyo atakua kaazima au dalali...Mkuu next tym usiwaogope bongo movie2 hao....mwenzako alikuja hvo akijua anakutana na don kumbe ptuuuuu....na uhakika alikua anakusonya njia nzima espcl akifikiria gharama za mafuta
Duuu! Kwanza pole sana kijana. Lakini story yako ina maswali mengi sana yasiyo na majibu. Hivi jamani tusaidiane kujibu hili labda tutamsaidie ili siku nyingine asirudie alichofanya na hiyo leseni yake ya kuwa mwanaume aendelee kuwa nayo.
1 Inawezekana vipi wewe mwanaume uwe na miadi na mwanamke tena ya kutongozana ubebe elfu 3 mfukoni kwa maana nyingine hukujiandaa? Au ulifikiri nani anaenda kulipa bill?
2. Au swali lingine au mlikutanata kituo cha basi jamani? Hamkupanga vizuri sehemu ya kukutania ili ujue kipi unapaswa kujiandaa nacho?
3. Kwa maelezo yako ulimpenda jinsi anavyochangia mada JF ndio ukavutiwa nae kwa nini usingesimamia yaliyo moyoni mwako juu yake badala ya kuangalia V8? Ujitahidi kutafsiri na kutenganisha aina za upendo.
4. Alafu unasema mlipiga story sana basi kama ni hivyo ww huko kujiamini kulipotea kabla hujaiona hiyo V8, sijui ulitishwa na perfume na poda? Vile vile kwa maongezi tu kwa wale profession hitter and rinner wangeshajijua siku nyingi waingie na gia gani wewe ilikuaje? Kaka hapa unahitaji kugwi.
Mwisho lengo si kukuvunja moyo lakini ujifunze siku nyingine basi kama ni bahati usije ukapishana nayo ingawa kisicho rizk hakiliki