Storika Tz
Member
- Dec 18, 2023
- 17
- 47
Ep 01
Sikuwahi kufikiria wala kuwaza kama kuna siku nitakuja kumchukia kwango cha kumlaani marehemu kaka yangu na Mkewe. Kiufupi, nawachukia sana, yeye marehemu kaka na bibi harusi wake, nawachukia sana, tena sana. Popotea ulipo marehemu Kaka Fred, iwe motoni au peponi, naomba ujue nakuchukia sana, wewe na bibi harusi wako.Wote wawili nawachukia sana, na mlaaniniwe ile laana ya nguruwe .
Naomba ungana nami kwenye hii simulizi kujua lipi ni lipi.
SEHEMU YA KWANZA.
Sikuwa tayari kuona Kaka yangu, Fred , akizikwa kwenye lile kaburi. Nilimfata baba na kumnongoneza. Baba aliniangalia kama mtu niliyechanganyikiwa. Aliyashangaa maneno yangu.
“ Hutaki azikwe kwenye hili kaburi?” Aliniuliza. Bila kupepesa macho nilimjibu. “ Ndio baba , sitaki.”
“ Kwahiyo ulitaka azikwe wapi?” Aliniuliza.
“ Tuchimbe kaburi lingine tumzike” Nilimwambia.
“ Ach masihara, naomba usiongee tena hilo jambo. Watu wakikusikia hapa wanaweza kukuhisi vibaya.:”
“ Lakini baba……..”
“ Hakuna cha lakini, naomba fanya kama nilivyokuambia. Sitaki uongee kuhusu hilo jambo.Tena kaa kimya kabisa.” Aliniambia Baba.
Nikiwa nawaza nifanye nini, Padre alimaliza kulibaliki kaburi, aliwaruhusu watu washushe mwili wa kaka Fred kaburini. Vijana waliweka kamba vizuri kwenye jeneza na kuanza kulishusha.
“ Yaani naruhusu huu upumbavu ufanyike mbele yangu! Hapana, kaka hawezi kuzikwa kwenye hili kaburi.” Nilijiambia moyoni. Niliwasogelea wale vijana na kuwasimamisha. “ Kaka yangu hawezi kuzikwa kwenye hili kaburi. Naomba msiendelee kushusha jeneza.” Niliwaambia.
“ Eeeeh!” Watu wote walishangaa. Vijana waliokuwa wanashusha jeneza waliangaliana kwa mshangao. Sura zao zilijaa maswali yasiyokuwa na majibu.
“ Mnashangaaa nini! Naomba toeni hilo jeneza humo, tutachimba kaburi lingine hapa pembeni.” Niliwaambia. Walinitii na kuanza kulivuta juu, lakini Kabla hawajamalizia kulitoa, Ndugu zangu waliwaambia waendelee, walinisogelea na kunishika mkono.
“ Kwanini unataka kuharibu msiba wa kaka yako?” Aliniuliza Baba.
“ Siwezi kukubali azikwe kwenye hili kaburi.Kamwe siwezi kukubali hilo.” Nilimwambia.
“ Tunashindwa kukuelewa John, hili kaburi lina nini?” Aliniuliza Mjomba Chriss.
“ Aaaah! Nyie hamuoni? Yaani hamuoni kabisaaa, eeeh! Hamuonii….”
“ Hatuoni ndio mana tunakuuliza, kama kuna lolote la ajabu tuambie. Usilete vurugu bila sababu.” Aliongea Baba.
Nikiwa najibizana na ndugu zangu, Jeneza lilishushwa kaburini.Kitendo cha kuniongelesha huku jeneza linashushwa kaburini kilinikera, niliona ndugu wananifanyia mchezo, wananizonga kwa maswali hili watu wazike. Niliamua kuwapita ili niende kuzuia tena.
“ Niliwaambia msishushe Jeneza! Nani aliyewaruhusu?” Niliwauliza wale vijana huku nikiwasogelea. Jeneza lilikuwa kaburi tayari. Akili yangu iliniambia niingie nikalitoe. Nilishika nguzo ya kaburi na kutaka kuingia.
Kabla sijaingia, nilivamiwa na ndugu na kutolewa pale msobe msobe.
“ Niacheni…niacheni…..” Niliwaambia huku nikijaribu kujinasua kwenye miili yao.
“ Msimuache, mpelekeni nyumbani….” Aliongea baba.
Walinifunga kamba na kunibeba msobe msobe mpaka nyumbani. Walinifungia chumbani na wao wakarudi makaburini kuendelea na mazishi. Nilijaribu kuvunja mlango nilishindwa, nilijaribu kukunja nondo za dirishani ili nitoke, nilishindwa pia.
“ Nafanyaje?” Nilijiuliza.
“ aaha…aha..aha…….aaaaaaaaaa….aaaaa……” Nilipiga kelele kuomba msaada. Hakuna aliyefika kunifungulia mlango.Nilikata tamaaa.
“ Nisamehe Kaka Fred, nimeshindwa kukusaidia.Nisamehe sana kaka.” Nilijisemea moyoni.
“ Lakini bado, vita haijaisha. Nitafanya jambo kukuokoa. Niamini mimi Fred, nitafanya jambo kukuokoa.” Nilijisemea moyoni tena.
…………………
Baada ya masaa kadhaa kupita, nilisikia sauti za watu wakija kutoka makaburini. Kuridi kwao kulimaanisha kaka yangu Fred amezikwa kwenye lile kaburi. Hii ilimaanisha nimeshindwa kumtetea.
Mlango wa chumba nilichofungiwa ulifunguliwa, aliingia baba akiwa na ndugu wengine. Walinikarisha chini na kunisema. Kwa muda wa masaa karibu matatu walinisema bila kunipa nafasi ya kujieleza. Walinieleza jinsi gani nilivyowadharilisha.
Sikutaka kubishana nao wala kuwaambia sababu ya kile nilichofanya.
Baada ya kisemo cha muda mrefu sana, waliondoka na kuniacha. Giza lilikuwa limeingia. Niliendelea kukaa mle ndani bila kutoka nje. Dakika ziliyoyoma, masaa yalikatika.
……………………
Majira ya saa nane usiku, nilitoka mle ndani. Watu wote walikuwa wamelala.
Niliingia store na kuchukua chepe, bila kuonwa na mtu yeyote nilikimbia kuelekea makaburini.
“ Ni lazima nimuhamishe kaka, siwezi kukubali azikwe kwenye lile kaburi.” Niliwaza huku nikielekea makaburini.
Dakika kadhaa mbele nilifika, niliyatoa mataji yote na kuyaweka pembeni. Nilianza kulifukua kaburi. Kwakuwa walizika siku ile ile kazi ya kufukua haikuwa ngumu, nilifukua mpaka mwisho, lakini Ajabu,Jeneza halikuwepo ,Kaburi lilikuwa tupu.
“ Eeeeeh!” Nilistaajabu.
Nakuja