Mkapa vs kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa vs kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by pcman, Sep 22, 2010.

 1. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  WanaJF nimeikopi hii mahali, Tafakari, chukua hatua

  KIONGOZI BWM Vs JK
  MWAKA 2000 -2004 Vs 2005-2009

  Unga 460 Vs 1000 = 217%
  Mchele 600 Vs 1200 = 200%
  Sukari 760/kg Vs 1600/kg = 210%
  Mkate 250 Vs 700 = 280%
  Maharagwe 360/kg Vs 1000/kg = 277%
  Mafuta ya taa 450/lt Vs 1050 = 233%
  Mafuta ya uto 178/lt Vs 720/lt = 404%
  Nazi 100 Vs 550 = 550%
  Mchicha/tembele 50 Vs 150 = 300%

  unalipwa 100,000/-kwa mwezi kwa jedwali la hapo juu kila siku lazima
  ununue unga robo 400, mchele nusu 300, uto kibaba 125, mafta taa
  kipimo 300, sabuni nusu kipande 50, sukari robo 400, maharagwe robo
  250, mkaa nusu kisado 300, nauli go & return 500, maji ya kunywa 500,
  hapo ni bachalor kwa siku ni 3,125 mara 30 = 93,750 kwa mwezi. Okay
  kodi kwa mwezi 20,000/- umeme 6000 kwa mwezi =total kwa mwezi ni
  120,000/- je hiyo 20,000/- ziada katoa wapi????? ndo hizo mwisho wa
  siku zina wapeleka jela au kuwanaachishwa kazi. Je maisha bora hapo
  atoe wapi? Na je angekuwa na mtoto wa shule au watoto wawili? hapo
  hajaumwa, hajatembelewa na mgeni akamnunulia soda, hajanunua nguo
  nyingine!!!! Huyu mnaempigia kura hayajui hayo na hatambui kama una
  familia kijijini pia. wao wanatibiwa na serikali, mafuta ya magari
  kwao ni sawa na kumuuliza bibi akupigie story ya sungura. wenzie
  wakitaka ongezo la mshahara wanajadiliwa in 2Hrs jibu tayari ila
  waalimu na wenzao.........! 3 years.

  Yeye huyu JeyKey na hao wapambe wake na hao wanajipendekeza kama
  Shigongo waulizeni watoto zao ni akinani? utaambiwa mbunge, mara yuko
  BOT mara yule wa mwisho yuko ulaya kamtembelea shangazi yake, mara
  yuko busy na tenda ya kusuply komputa Wizarani. Wewe je unae mpigia
  kura tupe wasifu wako hata hao watoto wako na wategemezi wako. Hata
  baiskeli kule kijijini huna wala wazazi wako ndo unakesha kuwaombea
  wasiumwe kwa kuwa gharama za hospitali zitakuwa zako.

  Muulize kesi za mafisadi vipi? Na je wanampango gani? utaambiwa yuko
  busy na harakati ya kutafuta ulaji kwa mara ya pili.

  Hao wapambe wake na mawaziri wanaendesha magari gani utaambiwa aah
  wana tano tano kila wizara VBV8, uliza bei zake kila moja, inatumia
  mafuta kiasi gani kwa mwezi, na majukumu yake ni yapi? Na je
  zinakoenda akina RAV4, Suzuki, BMW ndogondogo hawafiki? Utaambiwa
  wanawahi kuwasilisha agenda. KWEEELI?

  Na je hizo gharama za uendeshaji fedha zinatoka wapi? Utajibiwa kwenye
  mfuko wa serikali. Waulize serikali ina miradi gani ya kuweza
  kuendesha hayo magari tu achana na posho zao na mengineyo? Jibu ni
  KODI ZENU wananchi waungwana tulio na amani na utulivu kwetu. KWEELI
  kwa mshahara wa laki mbili zangu/zako?

  FUNGUENI MACHO NA AKILI ZENU WAUNGWANA. Wenzenu Zenji wameshaliona
  hili wameamua kujicholea MIPAKA yao Mapema.

  MTAENDELEA KUZUBAISHWA NA STORI ZA KUTUNGA NA UDAKU NA KUSHANGILIA
  MISAFARA MIREFU YA KAMPENI INAYOUNDWA NA KODI ZENU.
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  duu yaani sijui inakuwaje natamani watanzania woote wayajue haya!
   
 3. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hizi ndio data wagombea wa Chadema wanatakiwa wazimwage kwenye mikutano ya hadhara wavijijini wapate kuelewa udhalimu wa CCM!!
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kumlinganisha mkapa na kikwete ni sawa na kumlinganisha Sir Isac Newton (Mkapa) na mwalimu wa UPE (makamba)
   
 5. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #5
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Waliokua wanasema MUNGU Aturehemu muda ndo huu, Ametuonyesha Rehema zake kwa kumleta mkombozi atakaye tutoa kwenye utumwa na udhalimu wa mafarao wa sisi-m. Usifanye makosa 31 oct.
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  Kikwete hajui alifanyalo, ndio maana anajidondosha majukwaani ili wapiga kura wamuonee huruma.
   
 7. T

  Tata JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,734
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Wrong! hajidondoshi. Afya ndiyo inayomsumbua na kumsababishia kudondoka.
   
 8. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,355
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Atakapochaguliwa tena haya yanaweza tokea!

  Muhula wa kwanza v/s Muhula wa pili

  Unga 1000 Vs 2500
  Mchele 1200 Vs 2400
  Sukari 1600/kg Vs 3200/kg
  Mkate 700 Vs 1800
  Maharagwe 1000/kg Vs 3000/kg
  Mafuta ya taa 1050/lt Vs 2000
  Mafuta ya uto 720/lt Vs 1600/lt
  Nazi 550 Vs 1200
  Mchicha/tembele 150 Vs 600

  Na mshahara utakuwa huo huo maana alisema hata kwa miaka nane hamtaongezewa!!

  Be careful hapo Oct 31!
   
 9. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Nami niongezee kidogo juu ya hapo

  Cement 6000 vs 12500 asilimia jaza mwenyewe
  Kodi ya chumba uswazi 10,000 vs 25,000 malizia
  mabati ......
  ndoo ndogo ya mafuta ya kula (10L) 10,000 vs 22,000

  nenda mbele zaidi na uyaone maisha bora ya kila mtanzania
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Nadhani wanauchumi wanaweza kutueleza vizuri zaidi katika hili kuendana na kuimarika au kuanguka kwa sarafu ya TZ, kama hatujaona kasoro hapa basi may we rest in peace, Amen.
  Guys. Tanzanians, open up your eyes and watch the rotten state and a decaying country at our own pace and cost. Wajukuu wetu watatulaumu sana kwa kuliacha taifaletu liangike kiasi hiki!
   
 11. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mi nitatoa kopi 10. harafu ntawapelekea wabishi wanao shabikia ccm ili wanaposhabikia ccm wajue wanajimaliza wenyewe.

  Naamini kila mwana JF akitoa kopi 10 tu, italeta tofauti kwenye upigaji kura. HEBU TUGAWE HII MSG KWA WATU. BIG UP PCMAN
   
 12. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Nyange, karibu.
   
 13. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Watanzania kweli tuna msiba wa watu wanaoendelea kushabikia ccm huku hawajui watoto wao watafanya nini miaka ijayo. wakati wao January Makamba na Rizwani tayari wamesha anza kula bata. Mi niliona shabiki mmoja wa ccm amevaa kandambili zote za mguu wakulia!!.

  KWELI WAMEWATUMIA WATANZANIA MASIKINI KUWA MTAJI WAO.
  Mwenyekiti wa maadili wa ccm ndo anakashfa ya rushwa ya Rada. waulizeni mbona naye hawajamfanyia usanii wa kufungua kesi ili waendelee kuzuga??
   
 14. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mkuu mi tangu nizaliwe sijawahi kupigia kura ccm na kamwe sintafanya hivo make sijawahi kuridhika na bajet za serikali. How can you pend let say 800,000 while your income is only 300,000?. Kama hii haiwezekani kwa mwananchi, vile vile haiwezekani kwa serikali.

  Kuna bwana mmoja rafiki yangu anafanya kazi wizarani, alinieleza kuwa:
  'Nafanya kazi kwenye mradi mmoja wa Serikali, wakitpa shs, 50,000,000 ziende kwenye mradi, zitakazo fika kwenye huo mradi ni kama sh. 500,000. tu nyingine lazima zitabaki kwa waziri, katibu mkuu, na sisi (wao) tutajilipa posho mbali mbali, harafu tusubiri mwakani ili tuongezewe nyingine!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 15. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  Chaguo la Mungu
   
 16. mdoe

  mdoe JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 436
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimechoka kukaa chini na kutoa machozi. Nachukua hatua. Sijali kama itanigharimu kitu gani, ninachojua ni kwamba sitajutia uamuzi wangu mwisho wa siku. Naipenda sana Tanzania.
   
 17. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wanauchumi wetu ni waaajabu sana pamoja na mfuko wote wa bei watasema uchumi unakua. Swali unakua kwa anani kama wanachi hoi, serikali nayo inasema haina hela za kufanya almost kila kitu
   
 18. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  jamani hivi hziz data zinzwafikiwa watu kweli??nina uhakika kila zitakayemfikia lazima ampige chini down kikwete.
   
 19. MANI

  MANI Platinum Member

  #19
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Jana Dr Slaa aliwaambia wananchi wa Hai bei ya vitu na huduma haibagui mtu kwa kigezo cha kadi ya chama natumaini watakuwa wameelewa.
   
 20. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimeshaicopy na kuisambaza kwa email contact zangu zote za wa TZ !!!

  We real need change Ahhhaaa. I can't wait anymore !!!!
   
Loading...