Jamani jamani, Mkapa ni Msaliti wa taifa. Ni mtu ambaye baba wa taifa alizunguka nchi nzima kumnadi kwa ndiye mtu safi. Kweli jamaa alikuwa safi ukilinganisha na walijitokeza wakati huo(kama sio alikuwa bado kazubaa). Kiuwezo wa akilia na ufanyaji kazi jamaa ni safi kabisa. Tukamwamini baba wa taifa, tukamuunga mkono, tukijua Waarabu hawatapata nafasi ya kuchukua Loliondo nyingine. Uuuuuwiiiii! Usimuamshe aliyelala, jamaa kajanjaruka, kalaghaiwa na wazungu, eee bwana eeee....wacha aipige nchi mnada. Huku htaki kusikia la mtu. Wabunge wakakandamizwa, atakayeleta fyoko,harudi bungeni next time! Dhahabu yetu ikapigwa mnada, migodi mikubwa ikafunguliwa 1999, 2000, 2002, 2003 baada tu yule aliyemweka hapo alinde mali hizo kumrudia muumba wake! Kajiuzia mgodi mkubwa wa makaa ya mawe kwa shiling millioni 700 akatanguliza milioni 70, akaanza kuvuna! Milioni 700 kwani unanunua nyumba Temeke? Mgodi wenye thamani ya mabilioni! Kumbukeni kauli mbiu ya uchaguzi mwaka 1995 ilikuwa "hakuna biashara ikulu". Asiyejua kosa kubwa tulilofanya wakati wa Mkapa kama nchi ni uuzaji wa maeneo ya DHAHABU, ikishachimbwa hatakaa ijitengeze milele. Wamechukua bure! kama huamini fuatilia Ghana, SA, Mali na Zimbabwe, utagundua jamaa alituingiza mjini kama yeye si Mtanzania! Watu wanasema ni wa Msumbiji, yawezekana kabisa.
Jamaa ni msaliti kabisa, uwezo alikuwa nao lakini akautumia kuumiza nchi. Mazuri aliyofanya ilikuwa ni ghiliba kutuibia, naamini hivyo.