Mkapa apanda kizimbani Kisutu

Mkapa ni rafiki wa karibu sana na Mahalu, hilo linafahamika fika. Manunuzi hayo ya nyumba ya ubalozini kwetu Italy yalikuwa ya kifisadi yakifanywa na Mahalu akishirikiana na huyo dada (Grace) ambaye alikuwa hawara yake kiasi cha kuharibu na ndoa yake wakishirikiana na mamaafia wa Kiitaliano.

Inasemekana pia kuwa CCM walikuwa na mgawo katika pesa hizo nafikiri ndo maana Mkapa amejitokeza hadharani kumtetea swahiba wake asiangukie mikononi mwa pilato ili hali pesa hakula yeye peke yake.

Na kwa mtiririko huu wanaelekea kushinda kesi wadai fidia kwa kuzalilishwa na mishahara yao maana wamekuwa wakilipwa mishahara nusu tangu wasimamishwe kazi.

Mkuu nitatofautiana kidogo na wewe!maana J.k alijua kila kitu juu ya ununuzi,gharama na mkataba wa jengo ilo,na hata issue ya mikataba miwili aliifahamu,na serikali ilibariki ilo na J.K akiwa kama waziri wa mambo ya nje alibariki ununuzi huo na hata kukutana na mama muuzaji wa jengo ilo,na hata baadhi ya vielelezo vimewakilishwa mahakamani vikiwa na sahihi ya ******!hii kesi ni wazi imefunguliwa kwa kukomoana,kwa kua tu ni kweli ulicho ongea kua Grace ni hawara wa Mahalu na mpaka ikafikia ndoa yake kuvunjika,na mume wa zamani wa Grace ni best mkubwa wa ******,na tatizo lingine Mahalu alikua akimdharau sana ******,ndio maana baada ya ****** kuchukua madaraka tu alichokimbilia ni kutengeneza kesi hiyo ili kuwakomoa,ndio maana awali kesi ilikua na watuhumiwa zaidi ya hao wawili lakini wengine wote walitemwa na wakabaki walengwa!hii kesi haina merrit kabisa,na hv visasi vya ****** vitakuja kumback fire tu!
 
Mkuu STEIN,

Chuki binafsi za JK ndizo zimepelekea kushitakiwa kwa Prof. Mahalu. Shahidi anayefuata kuitwa Mahakamani nimedokezwa kuwa ni JK mwenyewe (Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje). Kesi hii itatoa somo kwa viongozi wetu kwamba: "kama wamedhulumiana kwenye deals zao wasitumie Dola kukomeshana....wataishia kujiumbua wenyewe...ndo haya yanaelekea kutokea sasa."

Pamoja na Fedheha itakayopatikana, Wananchi wanyonge ndiyo watakamuliwa ili Serikali ipate Fedha za kulipa fidia.
Huko sahihi mkuu. Naamini JK siku hizi anajutia kuanzisha kesi hii ambayo inaonyesha wazi ilifunguliwa kumkomoa Mahalu. Ni kielelezo ama ushahidi jinsi vyombo vya uchunguzi,upelelezi na mashitaka ambavyo siyo huru,vinafanya kazi kwa shinikizo ya watawala. Na kwasababu tumekua tunasikia hukumu za ajabu ajabu toka kwa baadhi ya majaji wetu(wateule wa JK) basi tusije shangaa tukisia hukumu nyingine ya kijinga toka kwa hawa jamaa.
 
Mkapa anamtetea sana mahalu kuwa ni mwamiinifu na anamjua toka akiwa waziri. Anasema si mawasiliano yote yalifanywa kwa maandishi na kuwa baadhi yalikuwa kwa mdomo


Ninachokipenda kutoka kwa mkapa

1.Ana msimamo na siku zote yupo tayari kusimamia kile anachokiamini ni sahihi

2.Hana urafiki wa mashaka,kama ni rafiki yako atakuwa karibu na wewe muda wote

3.Hapendi unafiki kama walivyo wanasiasa wengine

kudos President Mkapa
 
Mkapa ni rafiki wa karibu sana na Mahalu, hilo linafahamika fika. Manunuzi hayo ya nyumba ya ubalozini kwetu Italy yalikuwa ya kifisadi yakifanywa na Mahalu akishirikiana na huyo dada (Grace) ambaye alikuwa hawara yake kiasi cha kuharibu na ndoa yake wakishirikiana na mamaafia wa Kiitaliano.

Inasemekana pia kuwa CCM walikuwa na mgawo katika pesa hizo nafikiri ndo maana Mkapa amejitokeza hadharani kumtetea swahiba wake asiangukie mikononi mwa pilato ili hali pesa hakula yeye peke yake.

Na kwa mtiririko huu wanaelekea kushinda kesi wadai fidia kwa kuzalilishwa na mishahara yao maana wamekuwa wakilipwa mishahara nusu tangu wasimamishwe kazi.

Thank you.

Tanzanians are so easily fooled. Mahalu's friend and a known thief Mkapa testifies that everything was above board and people are ready to declare Mahalu innocent.

Mahalu is a thief but he will probably walk because fooling Tanzanians is pretty simple.
 
Yanayoendele hapa kwetu ni bora tusinge enda shule... Au tungeishia darasa la nne I mean kujua kusoma na kuandika.

ila kama umesogea Mbele kidogo kiasi cha kuweza kufikiria at least in two, three dimensions na kufanya reasonong kidogo utagundua Mabmo hayaendi kwa sababu ya kikundi fulani...

Mfano mzuri na mimi huwa najiuliza:

1. Ilikuwaje Ndege ya Jeshi la Qatar kuchukua wanyama zaidi ya 120 bila hata mtu mmoja kuuawa wakati wakata mkaa kila leo wanapigwa risasi????

2. Inakuwaje katika wabunge wa CCM zaidi ya 250 anakosekana mtu wa kumteua kuwa waziri wa wizara ya Afya hadi tukamchukue upande wa pili?

3. Inakuwaje Magembe na tuhuma zote za mbolea,, Korosho tandahimba.....etc, Lazaro nyalandu na Madiliyote aliyofanya Bado yuko kwenye Baraza la mawaziri????

4. Inakuwaje kuna watu wameshindwa kusoma, kusomesha watoto wao na hadi mlo mmoja unawashinda lakini bado wanadanyanywa na vielfu tano... tulaki moja na wanaishabikia CCM?

Poleni sana wana CCM na Poleni sana wabunge wa CCM

Umenipandisha hasira,m4c daima...ccm ccm ccm ccm who are this gs?
 
RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa (73) amepanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kumtetea aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Katika kesi hiyo, Profesa Mahalu anadaiwa kuiibia Serikali Sh. bilioni 2 katika ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Huku Mahakama hiyo ikiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, Mkapa aliwasili saa 4.45 na kutoa ushahidi kuanzia saa 5.32 asubuhi na kumaliza saa 7.08 mchana.

Katika ushahidi wake, Mkapa alimmwagia sifa Profesa Mahalu kuwa ni mchapa kazi, mwenye heshima na mwaminifu mkubwa.

Alidai kuwa hajui aliyemshitaki mahakamani ni nani kwa sababu mpaka anaondoka madarakani, mchakato wa ununuzi wa jengo hilo anajua ulikwenda sawa.

“Namfahamu Balozi Mahalu kama msomi mzuri, mtumishi mwadilifu …na balozi wetu Bon, Ujerumani,” alidai mahakamani Mkapa alipoulizwa anamfahamu vipi Profesa Mahalu.

Huku akiongozwa na Wakili wa Upande wa Utetezi, Alex Mgongolwa mbele ya Hakimu

Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ilvin Mgeta; mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
Wakili: Mwaka 1995 hadi 2005 ulikuwa wapi?

Mkapa: Nilikuwa Dar es Salaam nikishika wadhifa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania.

Alipoulizwa uzoefu wake katika mambo ya kimataifa, alifafanua kuwa alipata kuwa Ofisa wa Mambo ya nNje na Balozi wa Tanzania katika nchi za Nigeria, Canada na Marekani.

Wakili: Ukiwa Rais unafahamu nini kuhusu ununuzi wa jengo la ubalozi nchini Italia?

Mkapa: Nilifahamu Balozi wetu alifanya ununuzi wa jengo kwa euro 3,098,741.40 kwa maagizo ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa wakati huo alikuwa Profesa Mahalu.

Wakili: Katika ununuzi mlipewa masharti yoyote?

Mkapa: Ndio, mimi nilielezwa kuwa mmiliki wa jengo alitaka alipwe mara mbili, kiasi kimoja akaunti moja na kiasi kingine akaunti nyingine na akaunti zote ni za mtu mmoja ambaye ndiye mmiliki wa jengo.

Maelezo mengine ya Mkapa

Mkapa aliendelea kudai kuwa Serikali ilitoa baraka na yeye alitaarifiwa na hakuzuia, kwa sababu nia yake ilikuwa ni kupata jengo kwa ajili ya ofisi za ubalozi, hivyo masharti hayo hayakuwa kizuizi kwake.

Kuhusu mikataba miwili iliyosainiwa katika ununuzi wa jengo hilo, Mkapa alidai kuwa yeye hakumbuki kama alijulishwa, anachojua ni kwamba fedha zingelipwa katika akaunti mbili.
Amshangaa Lumbanga

Rais huyo mstaafu alidai kumshangaa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa mashitaka katika kesi hiyo, Matern Lumbanga, kwa madai yake mahakamani hapo kuwa Serikali haitambui ununuzi wa jengo hilo.

“Namshangaa sana, kwa nini alisema hivyo wakati mimi Rais nilikuwa na taarifa!” Alisema huku akionesha mshangao.

Mkapa katika ushahidi wake alidai kuwa angeweza kuzuia ununuzi wa jengo hilo, lakini aliona umuhimu wa kulinunua akatoa amri linunuliwe, ingawa nchi ilikuwa kwenye matatizo ya fedha na fedha za ununuzi huo zingeweza kwenda katika mambo mengine.

JK atajwa

Mkapa alipewa taarifa ya kumbukumbu za Bunge ambamo Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo (Rais Jakaya Kikwete), akitoa taarifa bungeni kuwa mwaka 2001/02 wizara hiyo ilinunua jengo hilo la ofisi ya ubalozi Italia kwa Sh bilioni 2.9.

Kikwete katika taarifa hiyo ya Bunge, alieleza kuwa lengo ni kuondokana na adha ya kupanga kwenye majengo ya watu na kwamba ununuzi wake ulifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na ushauri wa watathimini wa Wizara ya Ardhi na Wizara ya Ujenzi.

Baada ya kusomewa taarifa hiyo, Mkapa aliulizwa na Wakili Mgongolwa kama kuna usahihi katika taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo, akajibu kuwa taarifa hiyo ilikuwa sahihi na ndicho anachotambua yeye akiwa Rais wakati huo.

Mkapa alipoulizwa kama kuna malalamiko yoyote kuhusu mchakato wa ununuzi wa jengo hilo yaliyotolewa na Serikali ya Italia au mmiliki wa jengo kuwahi kuyapata baada ya ununuzi, alijibu kwa kifupi. “Hapana.”

Kuhusu mawasiliano kati ya Serikali na Balozi Mahalu, Mkapa alidai kuwa balozi anaweza kuandika barua kwa waziri wake ambaye ni wa Mambo ya Nje, au Katibu Mkuu Kiongozi au kwa Rais moja kwa moja na kuongeza kuwa mawasiliano mengine yanaweza kufanyika kwa mdomo tu.

Aliongeza:“Inategemeana na unyeti wa jambo mnalowasiliana.”

Mawakili wa Serikali

Katika maswali na majibu na mawakili wa Serikali, Wakili Vincent Haule alitaka kujua tofauti kati ya kiwango alichodai kufahamu cha ununuzi wa jengo hilo cha euro milioni 3.09 na kiwango kilichotajwa bungeni kuwa ni gharama ya jengo hilo Sh bilioni 2.9.

Mkapa alijibu kuwa yeye mambo ya viwango vya kubadilisha fedha hakuyajua kwa wakati huo, ndiyo maana akataja bei aliyokuwa akiijua na kwamba hiyo haikuwa kazi yake kujua.

Ashtuka Mahalu kushitakiwa

Mkapa alidai kuwa hajui aliyeagiza upelelezi dhidi ya ununuzi wa jengo hilo na pia hajui kama upelelezi ulifanywa akiwa madarakani au la, ila alipata taarifa za kushitakiwa Mahalu siku aliyoletwa mahakamani kusomewa mashitaka na pia aliona kwenye magazeti kesho yake.

Alipohojiwa na Wakili Haule kuhusu ruhusa aliyoitoa kwa mdomo kwa Mahalu kama ilikuwa ya kuridhia mikataba miwili au kuingiza malipo ya jengo katika akaunti mbili alijibu: “Mimi niliagiza ununuzi huo mambo mengine sijui, si kazi yangu mambo ya makaratasi.

“Nilitoa maelekezo … utekelezaji ni kazi ya wizara, lakini mwisho tulipata ubalozi nilioutaka,” alisisitiza Mkapa.

Alipohojiwa na Wakili Ponziano Lukosi kuhusu uhusiano wake na Lumbanga, Mkapa alidai alimwamini Katibu Mkuu Kiongozi huyo wa zamani na kumshirikisha katika mambo yote na pia alijua ununuzi wa ubalozi si Italia tu, ila ni pamoja na Marekani, Uingereza na India na akashangaa kudai kwake mahakamani hapo kuwa hajui.

Alipoulizwa kama anakumbuka jengo lingine walilowahi kununua kwa mfumo huo wa kuingiza fedha katika akaunti mbili, alijibu kwa ukali kidogo; “nakumbuka lakini siwezi kusema…kwa sababu mambo mengine yanaweza kuharibu uhusiano wa nchi na nchi.”

Baada ya kuonesha ukali kidogo, Hakimu Mgeta aliuliza kama mazingira hayo yapo na Mkapa akajibu kwa kifupi: “Yapo”.

Akijibu swali la Lukosi, aliyetaka kujua kama kulipwa katika akaunti mbili muuzaji wa jengo hilo, haoni kuwa alikuwa akikwepa kodi katika nchi yake, alijibu: “Nitasema kuwa hilo ni tatizo la nchi yake, mimi nimepata jengo nililolitaka nasema alhamdulilah!”

Kuna wizi?

Akijibu swali la mwisho la Lukosi kuwa kwa ulipaji huo wa akaunti mbili haoni kuwa ulikuwa ni wizi wa mshitakiwa Mahalu, alijibu; “nitashangaa sana na nitakushangaa wewe, Mahalu ni ni mwaminifu sana.”

Baada ya jibu hilo, Mkapa alitaka kuongeza neno, lakini akasita akidai: “Unanichokoza utanifanya niongee mengine mengi (anacheka).”

Kesi hiyo inaendelea leo mahakamani hapo ambapo mshitakiwa wa pili, Grace Martin ambaye alikuwa ofisa wa ubalozi Italia atatoa ushahidi wake.

sosi: HabariLeo | Mkapa anguruma mahakamani Dar es Salaam
 
Kitu pekee nitakachomkumbukia huyu mzee ni kwamba anajiamini na anajua kutetea misimamo yake vizuri na hapindishi maelezo.tofauti kabisa na JK wetu Mr Smile.ambayo inageuka toka Smile na kuwa kilio kwetu wananchi....wacha nilale nasikia hasira sana
Alamsiki.........................................
 
Duuu jamaa anamsaidia Mahalu big time kuna ukiukwaji pale wa taratibu ingawa jengo tumelipata lakini kuna wizi na ukwepaji kodi kule italia kwa mmiliki ambapo sio lengo la mahakama hii...ni mtazamo wangu!!
 
Kama vile namuona ben membe naye kizimbani akikabiliwa na mashtaka...ah,nami ngoja nivute blanket., alamsik
 
Good for Mkapa, I like he stands for Mahalu Maten Lumbanga is the one who cause all this for him to look good under New Presindent Kikwete
 
Rais Mstaafu BWM atinga mahakamani jana na kudai alibariki ununuzi wa majengo mawiri.

Na anashangaa kwa nini anashitakiwa kwani ni mchapakazi shupavu

Aendelea kushangaa kwa nn serikali ya JK kumshutumu kwa ufisadi wakati hakuna kitu kama hicho
 
Back
Top Bottom