Mkapa apanda kizimbani Kisutu

Mkapa apanda kizimbani Kisutu

[h=2]Mkapa atinga mahakamani[/h]

headline_bullet.jpg
Amtetea Profesa Mahalu
headline_bullet.jpg
Ashangaa mashitaka yake
headline_bullet.jpg
Amtaja kuwa mwadilifu

Mkapa(15).jpg

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akisindikizwa kuelekea chumba cha mahakama kutoa ushahidi katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam jana.(PICHA:TRYPHONE MWEJI)

Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa (73), amekiri mahakamani kwamba alikuwa na taarifa za kuwepo kwa mikataba miwili ya ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia, na kwamba kama Rais (wakati huo) alibariki ununuzi huo kufanywa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini humo, Profesa Costa Mahalu (63).

Kadhaka, Mkapa anakuwa Rais Mstaafu wa kwanza nchini kupanda kizimbani kutoa ushahidi wa kumtetea aliyekuwa mteule wake.

Profesa Mahalu na mwenzake wanakabiliwa tuhuma za kuisababishia serikali hasara ya Euro 2,065,827.60.

Mkapa alidai kuwa, yeye pamoja na serikali yake walifahamu utaratibu mzima uliotumika kuanzia mchakato hadi mikataba miwili ya ununuzi wa jengo hilo kukamilika.

Mkapa alitoa ushahidi wa utetezi wa Profesa Mahalu, jana mbele ya Hakimu Mkazi, Mfawidhi, Illivin Mgeta, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam.

Akiongozwa na Wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa, Mkapa alidai kuwa, kati ya mwaka 1995 na mwaka 2005 alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba Profesa Mahalu alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.

Alidai kuwa, alifanya mazungumzo ya ana kwa ana na Profesa Mahalu kuhusu mchakato mzima na umuhimu wa kununua jengo la ubalozi nchini Italia ambalo lilinunuliwa kwa Euro 3,098,741.40 ili kuepukana na kero ya majengo ya kupanga.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Wakili Mgongolwa na Mkapa:

Wakili Mgongolwa: Shahidi katika mwaka 1995 na mwaka 2005 ulikuwa wapi na wadhifa gani?

Mkapa: Nilikuwa Dar es Salaam kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakili Mgongolwa: Kabla ya kushika wadhifa huo ulipitia nyadhifa gani nyingine?

Mkapa: Kabla sijawa Rais niliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Canada na Marekani.

Wakili Mgongolwa: Ukiwa Rais wa nchi hii katika kipindi hicho, ulifahamu nini kuhusu ununuzi wa jengo la ubalozi nchini Italia?

Mkapa: Nilifahamu jengo la ubalozi wa Italia lilinunuliwa kwa Euro milioni 3.09 kwa maagizo ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakili Mgongolwa: Unakumbuka Balozi wa nchi hiyo wakati huo alikuwa ni nani?

Mkapa: Nakumbuka, wakati huo Balozi alikuwa ni Profesa Mahalu.

Wakili Mgongolwa: Je, Mheshimiwa serikali mlifahamu utaratibu uliotumika katika ununuzi wa jengo hilo?
Mkapa: Ndiyo.

Wakili Mgongolwa: Nani alikufahamisha machakato mzima?
Rais Mkapa: Balozi wetu Profesa Mahalu.

Wakili Mgongolwa: Katika manunuzi ya jengo hilo ulipewa taarifa kuhusu masharti ya mmiliki?
Mkapa: Nilitaarifiwa kabla ya ununuzi kufanyika kwamba mmiliki anataka alipwe kwa awamu mbili tofauti.

Wakili Mgongolwa: Kupitia akaunti za nani?
Mkapa: Kupitia akaunti za muuzaji wa jengo.

Wakili Mgongolwa: Je, Mheshimiwa kama Rais wakati huo, ulitoa baraka kuhusu ombi hilo?
Mkapa: Serikali yangu ilitoa baraka na mimi nilitaarifiwa kuhusu hilo.

Wakili Mgongolwa: Walikubaliana mkataba kwa maandishi au kwa njia gani?
Mkapa: Ninachofahamu walitakiwa kulipwa kwa mikataba miwili, lakini kama kulikuwa na suala jingine sifahamu.

Wakili Mgongolwa: Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi wakati wa uongozi wako, Martin Lumbanga, alikana kufahamu suala la mikataba miwili unasemaje kuhusu hilo?
Mkapa: Ninashangaa kwanini alisema hivyo, lakini serikali ilitoa idhini.

Wakili Mgongolwa: Kama wewe Rais ulijua inawezekana Lumbanga asijue suala hili?
Mkapa: Inawezekana asijue, lakini inakuwa vigumu sana.

Wakili Mgongolwa: Wewe ulijua na ukabariki?
Mkapa: Ndiyo mimi nilijua na nikabariki.

Wakili Mgongolwa: Kwa kumbukumbu zako, wizara ngapi zilihusika?
Mkapa: Wizara za Ujenzi, Ardhi na Fedha.

Aidha, Mkapa aliisomea mahakama taarifa iliyotolewa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (wakati huo Rais Jakaya Kikwete), aliyoitoa Bungeni kwamba kati ya mwaka 2001 na 2002 wizara ilinunua jengo la ubalozi nchini Italia kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi na ya Fedha.

Aliendelea kumnukuu Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo Kikwete kwa kusema:

“Mheshimiwa Spika hati ya jengo hilo tayari iko wizarani,” alimalizia kusoma taarifa hiyo iliyotolewa bungeni kuhusu ununuzi wa jengo hilo.

Wakili Mgongolwa: Una taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu matumizi mabaya ya fedha juu ya ununuzi wa jengo hilo?
Mkapa: Hapana sikuwahi kupata malalamiko.

Wakili Mgongolwa: Nini ufahamu wako kama Mstaafu kwa aliyekuwa Balozi wako?
Mkapa: Profesa Mahalu ni msomi, mfanyakazi mzuri, mwadilifu na mwaminifu.

Wakili Mgongolwa: Mawasiliano ya Balozi na serikali yalikuwa namna gani?
Mkapa: Balozi anaweza kuandika barua kwa Wizara ya Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi au kwa Rais.

Wakili Mgongolwa: Ni lazima kuwasiliana kwa njia ya maandishi?
Mkapa: Hapana, mara nyingi kwa maandishi, lakini hata kwa njia ya mdomo.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Wakili Mwandamizi wa Serikali, Visent Haule na Mkapa:

Wakili Haule: Je, Mheshimiwa jumla ya fedha zilizotumika ni kiasi gani?
Mkapa: Euro milioni 3.098 ndiyo ninavyofahamu mimi.

Wakili Haule: Nani aliagiza upelelezi ufanyike kuhusu ununuzi wa jengo hilo?
Mkapa: Mimi sijui.

Wakili Haule: Uchunguzi wa kesi hii ulifanyika ukiwa madarakani?
Mkapa: Mimi sijui nilishtukia Balozi ameshtakiwa nikiwa nimetoka madarakani.

Wakili Haule: Lini ulipata taarifa?
Mkapa: Siku aliyoletwa mahakamani kwa mara ya kwanza nilisikia kutoka kwa watu niliowateuwa kushika nyadhifa mbalimbali wakati nikiwa madarakani na siku ya pili yake nilisoma kwenye magazeti ndipo nikahakikisha.

Wakili Haule: Nani alikupa taarifa kama mmiliki wa jengo anataka kulipwa kwa awamu mbili (akaunti mbili) tofauti?
Mkapa: Kwa njia ya mdomo.

Wakili Haule: Nani alikupa taarifa?
Mkapa: Profesa Mahalu ndiye alinipa taarifa za kupata jengo.

Wakili Haule: Alikupa kabla au baada ya ununuzi?
Mkapa: Alikuwa ananipa taarifa kabla kwa sababu wakati huo kuna nchi zilikuwa na shida kama hiyo.

Wakili Haule: Unasema ulitaarifiwa na hukuzuia kwani ulitakiwa kuzuia?
Mkapa: Ningeweza kuzuia kwa sababu nilikuwa Mkuu wa nchi, lakini niliona umuhimu wake kama Profesa alivyonieleza.

Wakili Haule: Ulimruhusu Profesa Mahalu kununua jengo kwa awamu mbili au?
Mkapa: Nilimruhusu Mahalu kununua jengo masuala mengine hayakuwa mikononi mwangu.

Wakili Haule: Wakati unatoa ruhusa hiyo kulikuwa na mtu mwingine?
Mkapa: Hapana.

Wakili Haule: Ulitoa kwa njia ya mdomo au simu?
Mkapa: Ilikuwa na mazungumzo ya ana kwa ana kabisa.

Wakili Haule: Baada ya maagizo hayo nani mwingine ulimuagiza kuhusu ununuzi wa jengo hilo?
Mkapa: Nilitoa maagizo utekelezaji ni suala la wizara.

Wakili Haule: Sawa. Je, nani alihusika?
Mkapa: Ilikuwa ni wajibu wake Profesa Mahalu kuieleza wizara yake kwamba hayo maamuzi yalikuwa sahihi.

Wakili Haule: Kwa hiyo, wizara hukuiambia chochote bali ni Mahalu tu ni kweli au siyo kweli?
Mkapa: Kama Rais ilikuwa wajibu wangu kutoa amri tu.

Wakili Haule: Mheshimiwa jibu kama kweli au siyo kweli?
Mkapa: Sikumbuki.

Wakili Haule: Je, unafahamu kuna viongozi wengine uliowahi kuwateua wakati wa uongozi wako na wameburuzwa mahakamani?

Mkapa: Ndiyo, nafahamu kuwa Basil Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja.

Naye Wakili wa Serikali Mwandamizi Ponsiano Lukosi, alimhoji shahidi kama ifuatavyo:

Wakili Lukosi: Mheshimiwa, Lumbanga alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi wakati wa utawala wako?
Mkapa: Ni kweli.

Wakili Lukosi: Aliongoza miaka mingapi?
Mkapa: Miaka yote niliyokuwa madarakani.

Wakili Lukosi: Sifa za Lumbanga na Mahalu zinalingana?
Mkapa: Yah, ni sawa.

Wakili Lukosi: Lumbanga alikanusha kufahamu mikataba miwili ni sawa?
Mkapa: Nashangaa kama hili hakulijua.

Wakili Lukosi: Ulizindua lini jengo hilo la ubalozi?
Mkapa: Nilizindua Februari 23, mwaka 2003.

Wakili Lukosi: Ulikwenda Italia kuzindua jengo au?
Mkapa: Hapana, nilikwenda nchini Italia kikazi hivyo nikaalikwa kuzindua jengo hilo.

Naye Wakili wa Utetezi Mabere Marando alimhoji shahidi kama hivi:

Wakili Marando: Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) waliwahi kukuambia kama kuna uchafu umetokea kuhusu ununuzi wa jengo hilo?
Rais Mkapa: Hapana hawakuniambia.

Kesi hiyo inaendelea leo ambapo mshtakiwa wa pili, Grace Martin, atatoa ushahidi wake.

ILIVYOKUWA MAHAKAMANI

Mapema saa 3:45 asubuhi, Rais Mstaafu Mkapa, aliingia kwenye viunga vya mahakama hiyo akiwa kwenye gari yenye namba za usaji T 745 BQE aina ya Toyota Land Cruiser V8 ya rangi nyeusi pamoja na walinzi wake.

Rais huyo maarufu kwa jina la Mzee wa Uwazi na Ukweli, alikuwa amevaa kaunda suti ya rangi ya kijivu na viatu vya rangi nyeusi na aliongozwa moja kwa moja hadi ofisi ya Hakimu Mfawidhi kwa ajili ya kusubiri muda wa kuingia mahakamani kutoa ushahidi wake.

Saa 4:45 alianza kutoa ushahidi wa kumtetea Profesa Mahalu kwa kuongozwa na Wakili Mgongolwa hadi saa 7:17 mchana kisha kuondoka katika viwanja vya mahakama hiyo.

Mapema jana saa 1:45 asubuhi NIPASHE lilishuhudia walinzi wa Rais huyo wa zamani wakiwa katika viunga vya mahakama hiyo kwa ajili ya maandalizi ya bosi wao kufika mahakamani hapo.

Wakili Marando alisema kuwa Mkapa alipaswa kutoa ushahidi wake leo, lakini aliombwa kufika jana kwa kuwa leo atasafiri nje ya nchi.

CHANZO: NIPASHE
 
Tanzania inafilisiwa na viongozi kwa kuondoka na mamilion na badae kujiwekea kinga na kulindana lindana kwa maovu, hii tabia walionayo vigogo wa ccm ndio inayo ifanya nchi kuingia mashakani na Watanzania waliowengi kuwa mafukara, huku vigogo wakifuja mali za umma.

Jee kweli tutafika twendako? ikiwa 2015 Chadema hawakuchukuwa Dola basi Tanzania hakuna tena maisha ya mnyonge ni kutoka katika BAD kwenda kwenye WARST.
 
Baada ya kufuatilia kwa ukaribu mlolongo wa kesi na maswali na majibu kutoka mahakamani, ni wazi kuwa hii ni kesi dhidi ya 'Kikwete na Mahalu',sasa nashindwa kuelewa walitofautiana nini ama walishindwana katika 'deal'?? Na hivi kwanini huyu Rais wetu ana 'visasi' sana?, ni wangapi wanahusishwa na uhujumu uchumi na hawachukulii hatua stahili?? Inasikitisha.
 
"MKAPA AMKAANGA JK"
RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, jana aliikaanga serikali ya Jakaya Kikwete mahakamani akidai kuwa hakuna ubadhirifu wowote uliofanywa na aliyekuwa Balozi wa Italia, Prof. Costa Mahalu, katika ununuzi wa jengo la ubalozi nchini humo.
Akiongozwa na wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa, baada ya kuapa alieleza kuwa kati ya mwaka 1995-2005 akiwa Rais alifahamu ununuzi wa jengo la ubalozi nchini Italia kwa euro 3,098,741.40, na kuwa hata aliyekuwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye ni Rais wa sasa, Jakaya Kikwete alikubaliana na ununuzi huo.
Mkapa ambaye ni shahidi wa Mahalu katika kesi hiyo alisema mwaka 2003 yeye ndiye aliyekwenda mjini Rome-Italia kulizindua jengo hilo la kisasa, Profesa Mahalu akiwa balozi.
“Serikali yangu iliarifiwa bei na taratibu za kulinunua na mimi kama Rais wa nchi nilitaarifiwa kuwa muuzaji alitaka malipo yafanywe mara mbili tofauti katika akanti zake …na mimi kwa niaba ya serikali yangu nikatoa idhini linunuliwe kwa mtindo huo nilioutaja hapo juu,” alidai Rais Mkapa.
Mahalu anatuhumiwa kuidhinisha kwa niaba ya serikali ununua wa jengo la ubalozi kwa thamani ya euro milioni 3 kwa njia ya mikataba miwili na kwa akaunti mbili.
Mawakili: Wewe au serikali ya awamu ya tatu iliwahi kupokea malalamiko toka serikali ya Italia kuwa ubalozi wetu nchini humo ulivunja sheria kuhusu mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo?
Mkapa: Hapana, sijawahi kupokea malalamiko.
Mawakili: Ukiwa Rais hujawahi kupokea malalamiko kuwa fedha za serikali yetu zilizotumwa kwa ajili ya kumlipa muuzaji wa jengo hilo kuwa hazijamfikia?
Mkapa: Hadi leo hii natoa ushahidi hapa mahakamani sijawahi kupokea malalamiko ya aina hiyo.
Mawakili: Uliwahi kupata malalamiko toka kwa CAG, Wizara ya Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi, Waziri wa Mambo ya Nje, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wala Ofisi ya DPP kuhusu ubadhirifu wa ununuzi wa jengo hilo?
Mkapa: Sijawahi kupata.
Mawakili: Nini ufahamu wako kuhusu utumishi wa Profesa Mahalu?
Mkapa: Namfahamu kama msomi mzuri, mchapakazi, muadilifu na kiongozi anayetenda haki.
Mawakili: Mawasiliano kati ya serikali na balozi yanafanyika kwa njia zipi?
Mkapa: Balozi anaweza kuwasiliana na serikali yake kwa njia ya barua kwa Wizara ya Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi, Rais au kwa njia ya mdomo. Na mawasiliano siyo lazima yafanyike kwa njia ya maandishi tu kwa sababu maelekezo mengine ambayo anapewa balozi na serikali yake ni ya siri kwa maslahi ya taifa hivyo anaweza kuitwa nyumbani na kupatiwa maagizo hayo kwa njia ya mdomo.
Mawakili: Kwa wadhifa wako ule wa urais, kabla ya kwenda kuzindua jengo hilo Januari 23, 2003, hukuwahi kupokea taarifa toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na DPP za kukukataza usiende kuzindua jengo hilo kwa sababu kulikuwa na harufu za ubadhirifu wa fedha za umma?
Mkapa: Ofisi hizo hazikuwahi kunipatia taarifa hizo.
Yafuatayo ni mahojiano baina ya mawakili wa serikali
Mawakili: Hebu ieleze mahakama ni kwa nini bei za jengo zinatofautiana maana risiti za manunuzi zinaonyesha lilinuliwa kwa euro milioni 3 na hansard ya Bunge iliyosomwa na Kikwete bungeni mwaka 2004 inasema ilinuliwa kwa shilingi bilioni 2.9?
Mkapa: Kazi yangu siyo kufanya uthamini wa fedha za kigeni kwamba wakati huo hizo euro milioni 3 zilikuwa na thamani gani kwa fedha Tanzania (kicheka).
Mawakili: Nani aliagiza upelelezi wa manunuzi ya jengo la Italia ufanyike?
Mkapa: Sijui.
Mawakili: Uchunguzi wa jengo hilo ulifanyika wakati wewe ukiwa madarakani?
Mkapa: Sijui, nilikuja kuona Balozi Mahalu kashtakiwa mwaka 2007 nikiwa tayari nimestaafu. Nilithibitisha taarifa hizo kupitia vyombo vya habari kuwa ameshtakiwa.
Mawakili: Nani alikupa taarifa za muuzaji wa jengo hilo anataka kulipwa kwa mtindo huo wa akaunti mbili?
Mkapa: Ni Mahalu na alinipa taarifa kwa mdomo na alikuwa ameandaa ripoti juu ya ununuzi na akawa anaomba ridhaa ya serikali kabla ya kulinunua.
Mawakili: Ulisema hukuweza kuzuia ununuzi wa jengo, je ulikuwa na madaraka ya kuweza kuzuia lisinunuliwe?
Mkapa: Eh! Mimi ndiye nilikuwa Rais wa nchi; nilikuwa na madaraka hayo na badala yake fedha hizo zingeelekezwa kwenye mahitaji mengine ila kwa sababu nilikuwa ninajua umuhimu na faida ya nchi kununua jengo lile ndiyo maana nikaridhia kwa mdomo linunuliwe.
Wakili: Ulitoa maelekezo kwa nani?
Mkapa: Nilitoa maelekezo kwa njia ya mdomo kwa watendaji na maagizo hayo yalipaswa yatekelezwe na Wizara ya Mambo ya Nje na ilikuwa jukumu la Mahalu kuieleza wizara hiyo na ubalozi utekeleze maagizo yangu.
Wakili: Kwa hiyo unaieleza mahakama kuwa Wizara ya Mambo ya Nje, ilituma malipo kwa mtindo wa akaunti mbili tofauti?
Mkapa: Inahusu nini sasa? Mimi nilitoa maagizo, hivyo lilikuwa ni jukumu la Balozi Mahalu kuieleza wizara yake. Sasa suala la hayo makaratasi ya kufanya mchakato wa kulinunua, mimi kama Rais siwezi kuingilia. Watendaji walipaswa watekeleze.
Mawakili: Utajisikiaje tukikwambia kuwa yule muuzaji aliyetuuzia jengo kwa mtindo wa akaunti mbili alikuwa akikwepa kodi kwa serikali ya Italia?
Mkapa: Aaah! Mi’ sioni tatizo; kikubwa hapa Tanzania tumepata jengo, Alhamdulilah (kicheko).
Mawakili: Utajisikiaje ukisikia Mahalu alitumia zile euro milioni 3 kwa matumizi yake binafsi?
Mkapa: Nitashangaa sana. Pia wewe wakili wa serikali ndiyo nitakushangaa zaidi kwani hansard ya Bunge iliyosomwa na Kikwete bungeni imetamka bayana kuwa serikali ilimlipa muuzaji wa jengo na kwamba taratibu na sheria ya manunuzi ya umma zilifuatwa na hadi sasa huyo muuzaji hajawahi kulalamika kuwa hajalipwa fedha zake.
Rais Mkapa aliingia mahakamani hapo saa 3:45 asubuhi akiwa katika gari aina VX lenye namba T 745 BQE akiongozwa na walinzi wake.
Maafisa toka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) walionekana kuingia katika viwanja vya mahakama hiyo kabla ya kiongozi huyo kuwasili.
Hakimu Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ilvin Mugeta, aliahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo mshtakiwa wa pili aliyekuwa Meneja Utumishi na Utawala wa Ubalozi huo, Grace ataanza kujitetea .... Source Mjengwa blog
 
Kitendo cha Mkapa kwenda Mahakamani kumtetea Mahalu kitafungua ukurasa mpya. Inamaana kama anaweza kusimama kumtetea mtuhumiwa na yeye pia anaweza kujisimamia ajitetee...
 
• WALIOTEMWA UWAZIRI WAMSUSA

Hakimu Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ilvin Mugeta, aliahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo mshtakiwa wa pili aliyekuwa Meneja Utumishi na Utawala wa Ubalozi huo, Grace Martin, ataanza kujitetea.

Source Tanzania daima
 
Kwa kweli wadau mie mpaka sasa sielewi msingi wa kesi hii ninini. Ina maana huyo balozi Mahalu anatuhumiwa kula fedha za ununuzi wa jengo au kwamba alinunua jengo kwa bei ya kugushi kisha akala 10%???. Kwa sababu kama suala ilikuwa ni kwamba mmiliki wa jengo kutaka kukwepa kodi huko kwao Italia,si ingekuwa ni jukumu la serikali ya kwao kumshtaki huyo muuzaji? Mwenye ufahamu wa jambo hili tafadhali.
 
Uliisha wahi ona wapi fisi akamtetea mbuzi,na kumuacha fisi mwenzie aangamie?
 
baada ya miaka kama 10, raisi mstaafu amtete prof mahalu
1995-2005 akiwa Rais alifahamu ununuzi wa jengo la ubalozi nchini Italia kwa euro 3,098,741.40, na kuwa hata aliyekuwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye ni Rais wa sasa, Jakaya Kikwete alikubaliana na ununuzi huo. Mkapa ambaye ni shahidi wa Mahalu katika kesi hiyo alisema mwaka 2003 yeye ndiye aliyekwenda mjini Rome-Italia kulizindua jengo hilo la kisasa, Profesa Mahalu akiwa balozi.
“Serikali yangu iliarifiwa bei na taratibu za kulinunua na mimi kama Rais wa nchi nilitaarifiwa kuwa muuzaji alitaka malipo yafanywe mara mbili tofauti katika akanti zake …na mimi kwa niaba ya serikali yangu nikatoa idhini linunuliwe kwa mtindo huo nilioutaja hapo ju
 
Mhh kazi kweli kweli tutafika hata kama ni ahela.
 
RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, jana aliikaanga serikali ya Jakaya Kikwete mahakamani akidai kuwa hakuna ubadhirifu wowote uliofanywa na aliyekuwa Balozi wa Italia, Prof. Costa Mahalu, katika ununuzi wa jengo la ubalozi nchini humo. Akiongozwa na wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa, baada ya kuapa alieleza kuwa kati ya mwaka 1995-2005 akiwa Rais alifahamu ununuzi wa jengo la ubalozi nchini Italia kwa euro 3,098,741.40, na kuwa hata aliyekuwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye ni Rais wa sasa, Jakaya Kikwete alikubaliana na ununuzi huo. Mkapa ambaye ni shahidi wa Mahalu katika kesi hiyo alisema mwaka 2003 yeye ndiye aliyekwenda mjini Rome-Italia kulizindua jengo hilo la kisasa, Profesa Mahalu akiwa balozi. “Serikali yangu iliarifiwa bei na taratibu za kulinunua na mimi kama Rais wa nchi nilitaarifiwa kuwa muuzaji alitaka malipo yafanywe mara mbili tofauti katika akanti zake …na mimi kwa niaba ya serikali yangu nikatoa idhini linunuliwe kwa mtindo huo nilioutaja hapo juu,” alidai Rais Mkapa. Mahalu anatuhumiwa kuidhinisha kwa niaba ya serikali ununua wa jengo la ubalozi kwa thamani ya euro milioni 3 kwa njia ya mikataba miwili na kwa akaunti mbili. Mawakili: Wewe au serikali ya awamu ya tatu iliwahi kupokea malalamiko toka serikali ya Italia kuwa ubalozi wetu nchini humo ulivunja sheria kuhusu mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo? Mkapa: Hapana, sijawahi kupokea malalamiko. KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA MKAPA AMKAANGA JKGUMZO LA JIJI
 
Hajamkaanga katoa ushahidi mahakamani ulitaka aseme uongo?

kasema anachokijua kuhusu kesi hiyo.

mahakamani tunasema ukweli mtupu hakuna kukaangana
 
ɐuɐʞıןnظɐɥsǝbuı nɯnʞnɥ ɐɯǝpɐɥɔ ɐʍ ızobuoıʌ ɐʎ ɐʍnʞǝbuı ıuıʞɐן ıbuıʎu nʞıs ɐʎ ısǝʞ ııɥ
 
ɐuɐʞıןnظɐɥsǝbuı nɯnʞnɥ ɐɯǝpɐɥɔ ɐʍ ızobuoıʌ ɐʎ ɐʍnʞǝbuı ıuıʞɐן ıbuıʎu nʞıs ɐʎ ısǝʞ ııɥ
mkuu Excellent mbona posts zako zinapinduka?
 
Last edited by a moderator:
Usalama wa taifa as always. Kwa nini maagizo ya deal kubwa hivi yatolewe kwa mdomo? Halafu Mkapa anaweza kusema ana integrity kuhusu kuwabana wasiolipa kodi bongo kama anatetea wataliano kutolipa kodi??
 
Hakuna kesi hapo ni porojo tu, huyo mahalu atafungwa miaka kadhaa, lakini atakata rufaa (hapo inaweza ikawa amekaa jela kama mwezi hivi), then JK atalizika na ka roho kake kwambe amemkooa mahalu, then bifu litakuwa limekwisha...
 
wote ni wezi tu - kinachofanyika ni usanii tu!
 
RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, jana aliikaanga serikali ya Jakaya Kikwete mahakamani akidai kuwa hakuna ubadhirifu wowote uliofanywa na aliyekuwa Balozi wa Italia, Prof. Costa Mahalu, katika ununuzi wa jengo la ubalozi nchini humo. Akiongozwa na wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa, baada ya kuapa alieleza kuwa kati ya mwaka 1995-2005 akiwa Rais alifahamu ununuzi wa jengo la ubalozi nchini Italia kwa euro 3,098,741.40, na kuwa hata aliyekuwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye ni Rais wa sasa, Jakaya Kikwete alikubaliana na ununuzi huo. Mkapa ambaye ni shahidi wa Mahalu katika kesi hiyo alisema mwaka 2003 yeye ndiye aliyekwenda mjini Rome-Italia kulizindua jengo hilo la kisasa, Profesa Mahalu akiwa balozi. "Serikali yangu iliarifiwa bei na taratibu za kulinunua na mimi kama Rais wa nchi nilitaarifiwa kuwa muuzaji alitaka malipo yafanywe mara mbili tofauti katika akanti zake …na mimi kwa niaba ya serikali yangu nikatoa idhini linunuliwe kwa mtindo huo nilioutaja hapo juu," alidai Rais Mkapa. Mahalu anatuhumiwa kuidhinisha kwa niaba ya serikali ununua wa jengo la ubalozi kwa thamani ya euro milioni 3 kwa njia ya mikataba miwili na kwa akaunti mbili. Mawakili: Wewe au serikali ya awamu ya tatu iliwahi kupokea malalamiko toka serikali ya Italia kuwa ubalozi wetu nchini humo ulivunja sheria kuhusu mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo? Mkapa: Hapana, sijawahi kupokea malalamiko. KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA MKAPA AMKAANGA JKGUMZO LA JIJI
Wewe umekopi kazi za watu halafu unawadirect wengine wasome kwako, badala ya kuwadirect kwenye original source ambako wewe umeitoa. Hata muwe mnaacknowledge source basi. Tatizo la plagiarism linaonekana kuota mizizi sana miongoni mwa watanzania hivi sasa.
 
Back
Top Bottom