Mkapa apanda kizimbani Kisutu

Mkapa apanda kizimbani Kisutu

Nikiwa raisi, ntawekeza zaidi kwenye magereza kuliko shule.
Nimegundua, siwezi rudi shule ila naweza enda gerezani.

Hiyo ni rahisi sana hasa kwa nchi zenye demokrasia ya kweli!
 
Mahalu mavalu valu makapa kapi tu itakuwa
 
Dawa yao hawa majamaa ni katiba mpya na chadema kukamata usukuni kama vipara havijatoa jasho
thn hivi huyu mr clean ana watoto wangapi????
Unajua huyu m2 simwelewi in deep!
 
Napendekeza katiba mpya waondoe kinga ya rais kutoshtakiwa

Mukalunyoisa,
Hakuna kinga ya kutoshtakiwa kwa Rais. Rais anashtakiwa baada ya kutumikia kipindi chake cha Urais kwa matendo yake yote aliyoyafanya kama Raia. Kinga pekee aliyonayo ni kwa matendo ambayo ameyafanya kwa title ya Urais.

Watu wanachanganya sana hapa. Tunaposema mambo aliyoyafanya kwa title ya Urais mifano yake ni kama pale anaposafiri safiri kwenda ughaibuni kuiwakilisha nchi kwenye mikutano mbali mbali, kuiingiza nchi vitani kwa ajili ya kuilinda au kuteua Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wabunge, Mawaziri, nk ilimradi hajakiuka misingi ya katiba.

TUMBIRI wa JF,
P.O BOX - PM JF.
 
Last edited by a moderator:
Huu ushahidi utakuwa mzito tosha kabisa kumfanya jamaa (Mshtakiwa) achomoke. Na usiposaidia basi kuja kwake huyu kibosile mahakamani itakuwa ni useless.
 
Nawaona Marando na Alex Mgongolwa
 
Two ministries involved... Wizara ya arhi na Wizara ya kazi; Wote wamethibitisha value ya jengo la ubalozi.
 
Rais Mstaafu Mkapa kizimbani Dar

*
Monday, 07 May 2012 12:47

?

?RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, yupo kizimbani muda huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumtetea aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu anayekabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi akidaiwa kuisababishia serikali hasara kubwa.

digg
Chanzo MwananchiNews

Kwa taarifa zaidi Ungana nasi baadaye
 
Last edited by a moderator:
Mkapa anamtetea sana mahalu kuwa ni mwamiinifu na anamjua toka akiwa waziri. Anasema si mawasiliano yote yalifanywa kwa maandishi na kuwa baadhi yalikuwa kwa mdomo
 
Wanayosoma ni maelezo ya Mkapa wakati akitoa maelezo akisaidiwa na mawakili wa Mahalu na baadae kuhojiwa na mawakili wa serikali
 
Mkapa: The first priority was to get the premises... Niliruhusu jengo linunuliwe sikufuatilia masharti
 
Mkapa:
Lakn nakumbuka kama kuna mtu alikuwpo wakati nawaruhusu kununua, nilitoa maelekezo tukiwa wawili hakukua na mtu.
Kama wizara ilikua na wasiwasi, ingeniuliza mimi.
Kuna mambo ya siri ambayo si lazima.
Nilikua namuamini Lumbanga, aliyekuwa Katibu Mkuu.
 
Mkapa:
Nilitoa maelekezo ya kununua jengo kama India, Us na Uingereza.
Sikuuliza kwanini ilikua akaunti 2 tofauti.
Siwezi kusema siri nyingine maana zinaweza kuleta matatizo ya Kidiplomasia na Italy. Thanks God Italy hawakuwahi kulalamika!
 
Mbona mnatuchanganya tupeni picha ya kweli au tupeni kinachoongelewa.Je ameshatoa ushahidi
 
Mkapa:
Kwangu issue ya kodi ya Italy ni yao, sisi tulitaka jengo na tulipata.
Hadi nsataafu hakukua na malalamiko toka Wizara ya nje wala yeyote, na nilienda kufungua jengo, sijaambiwa nisijihusishe na hilo jambo, ila imetokea baada ya mimi kustaafu!
 
Amesimama au amekaa vyovyote vile lakini kama yuko huko kutoa ushahidi hapa kuna kazi! Lakini Tz ni zaidi ya uijuavyo inaweza ikawa ni usanii umeandaliwa tu ili kutuonyesha kuwa kuna utawala wa sheria na mahakam ziko huru wakati hakuna lolote.
 
Back
Top Bottom