Mkapa apanda kizimbani Kisutu

Mkapa apanda kizimbani Kisutu

mh mkapa ni mkweli kwan yeye ndo aliye mbariki mahalu.hivyo amemkaanga mr president waziwaz ,hawakukagua mafail,mh presdent alikua wazir wa mambo ya nje hakushirikishwa?
the fourm and new leader hawana ushirikiana viongozi jifunzen kwa ya jana mahakamani
 
Kikwete alikuwa na mgogoro binafsi Mahalu tangu Kikwewte akiwa waziri wa mambo ya nje

uchunguzi wa kesi yake ulifanyika wakati mkapa akiwa madarakani na yeye akakataa kuidhinisha afunguliwe kesi. jk alipoingia hilo lilikuwa moja ya mambo yake ya kwanza kuyaulizia
 
Source Tanzania Daima

RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, jana aliikaanga serikali ya Jakaya Kikwete mahakamani akidai kuwa hakuna ubadhirifu wowote uliofanywa na aliyekuwa Balozi wa Italia, Prof. Costa Mahalu, katika ununuzi wa jengo la ubalozi nchini humo.

Akiongozwa na wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa, baada ya kuapa alieleza kuwa kati ya mwaka 1995-2005 akiwa Rais alifahamu ununuzi wa jengo la ubalozi nchini Italia kwa euro 3,098,741.40, na kuwa hata aliyekuwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye ni Rais wa sasa, Jakaya Kikwete alikubaliana na ununuzi huo.

Mkapa ambaye ni shahidi wa Mahalu katika kesi hiyo alisema mwaka 2003 yeye ndiye aliyekwenda mjini Rome-Italia kulizindua jengo hilo la kisasa, Profesa Mahalu akiwa balozi.

“Serikali yangu iliarifiwa bei na taratibu za kulinunua na mimi kama Rais wa nchi nilitaarifiwa kuwa muuzaji alitaka malipo yafanywe mara mbili tofauti katika akanti zake …na mimi kwa niaba ya serikali yangu nikatoa idhini linunuliwe kwa mtindo huo nilioutaja hapo juu,” alidai Rais Mkapa.

Mahalu anatuhumiwa kuidhinisha kwa niaba ya serikali ununua wa jengo la ubalozi kwa thamani ya euro milioni 3 kwa njia ya mikataba miwili na kwa akaunti mbili.

Mawakili: Wewe au serikali ya awamu ya tatu iliwahi kupokea malalamiko toka serikali ya Italia kuwa ubalozi wetu nchini humo ulivunja sheria kuhusu mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo?

Mkapa: Hapana, sijawahi kupokea malalamiko.

Mawakili: Ukiwa Rais hujawahi kupokea malalamiko kuwa fedha za serikali yetu zilizotumwa kwa ajili ya kumlipa muuzaji wa jengo hilo kuwa hazijamfikia?

Mkapa: Hadi leo hii natoa ushahidi hapa mahakamani sijawahi kupokea malalamiko ya aina hiyo.

Mawakili: Uliwahi kupata malalamiko toka kwa CAG, Wizara ya Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi, Waziri wa Mambo ya Nje, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wala Ofisi ya DPP kuhusu ubadhirifu wa ununuzi wa jengo hilo?

Mkapa: Sijawahi kupata.

Mawakili: Nini ufahamu wako kuhusu utumishi wa Profesa Mahalu?

Mkapa: Namfahamu kama msomi mzuri, mchapakazi, muadilifu na kiongozi anayetenda haki.

Mawakili: Mawasiliano kati ya serikali na balozi yanafanyika kwa njia zipi?

Mkapa: Balozi anaweza kuwasiliana na serikali yake kwa njia ya barua kwa Wizara ya Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi, Rais au kwa njia ya mdomo. Na mawasiliano siyo lazima yafanyike kwa njia ya maandishi tu kwa sababu maelekezo mengine ambayo anapewa balozi na serikali yake ni ya siri kwa maslahi ya taifa hivyo anaweza kuitwa nyumbani na kupatiwa maagizo hayo kwa njia ya mdomo.

Mawakili: Kwa wadhifa wako ule wa urais, kabla ya kwenda kuzindua jengo hilo Januari 23, 2003, hukuwahi kupokea taarifa toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na DPP za kukukataza usiende kuzindua jengo hilo kwa sababu kulikuwa na harufu za ubadhirifu wa fedha za umma?

Mkapa: Ofisi hizo hazikuwahi kunipatia taarifa hizo.

Yafuatayo ni mahojiano baina ya mawakili wa serikali

Mawakili: Hebu ieleze mahakama ni kwa nini bei za jengo zinatofautiana maana risiti za manunuzi zinaonyesha lilinuliwa kwa euro milioni 3 na hansard ya Bunge iliyosomwa na Kikwete bungeni mwaka 2004 inasema ilinuliwa kwa shilingi bilioni 2.9?

Mkapa: Kazi yangu siyo kufanya uthamini wa fedha za kigeni kwamba wakati huo hizo euro milioni 3 zilikuwa na thamani gani kwa fedha Tanzania (kicheka).

Mawakili: Nani aliagiza upelelezi wa manunuzi ya jengo la Italia ufanyike?

Mkapa: Sijui.

Mawakili: Uchunguzi wa jengo hilo ulifanyika wakati wewe ukiwa madarakani?

Mkapa: Sijui, nilikuja kuona Balozi Mahalu kashtakiwa mwaka 2007 nikiwa tayari nimestaafu. Nilithibitisha taarifa hizo kupitia vyombo vya habari kuwa ameshtakiwa.

Mawakili: Nani alikupa taarifa za muuzaji wa jengo hilo anataka kulipwa kwa mtindo huo wa akaunti mbili?

Mkapa: Ni Mahalu na alinipa taarifa kwa mdomo na alikuwa ameandaa ripoti juu ya ununuzi na akawa anaomba ridhaa ya serikali kabla ya kulinunua.

Mawakili: Ulisema hukuweza kuzuia ununuzi wa jengo, je ulikuwa na madaraka ya kuweza kuzuia lisinunuliwe?

Mkapa: Eh! Mimi ndiye nilikuwa Rais wa nchi; nilikuwa na madaraka hayo na badala yake fedha hizo zingeelekezwa kwenye mahitaji mengine ila kwa sababu nilikuwa ninajua umuhimu na faida ya nchi kununua jengo lile ndiyo maana nikaridhia kwa mdomo linunuliwe.

Wakili: Ulitoa maelekezo kwa nani?

Mkapa: Nilitoa maelekezo kwa njia ya mdomo kwa watendaji na maagizo hayo yalipaswa yatekelezwe na Wizara ya Mambo ya Nje na ilikuwa jukumu la Mahalu kuieleza wizara hiyo na ubalozi utekeleze maagizo yangu.

Wakili: Kwa hiyo unaieleza mahakama kuwa Wizara ya Mambo ya Nje, ilituma malipo kwa mtindo wa akaunti mbili tofauti?

Mkapa: Inahusu nini sasa? Mimi nilitoa maagizo, hivyo lilikuwa ni jukumu la Balozi Mahalu kuieleza wizara yake. Sasa suala la hayo makaratasi ya kufanya mchakato wa kulinunua, mimi kama Rais siwezi kuingilia. Watendaji walipaswa watekeleze.

Mawakili: Utajisikiaje tukikwambia kuwa yule muuzaji aliyetuuzia jengo kwa mtindo wa akaunti mbili alikuwa akikwepa kodi kwa serikali ya Italia?

Mkapa: Aaah! Mi’ sioni tatizo; kikubwa hapa Tanzania tumepata jengo, Alhamdulilah (kicheko).

Mawakili: Utajisikiaje ukisikia Mahalu alitumia zile euro milioni 3 kwa matumizi yake binafsi?

Mkapa: Nitashangaa sana. Pia wewe wakili wa serikali ndiyo nitakushangaa zaidi kwani hansard ya Bunge iliyosomwa na Kikwete bungeni imetamka bayana kuwa serikali ilimlipa muuzaji wa jengo na kwamba taratibu na sheria ya manunuzi ya umma zilifuatwa na hadi sasa huyo muuzaji hajawahi kulalamika kuwa hajalipwa fedha zake.

Rais Mkapa aliingia mahakamani hapo saa 3:45 asubuhi akiwa katika gari aina VX lenye namba T 745 BQE akiongozwa na walinzi wake.

Maafisa toka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) walionekana kuingia katika viwanja vya mahakama hiyo kabla ya kiongozi huyo kuwasili.

Hakimu Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ilvin Mugeta, aliahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo mshtakiwa wa pili aliyekuwa Meneja Utumishi na Utawala wa Ubalozi huo, Grace Martin, ataanza kujitetea.
 
Mkapa sio msafi, ameliibia taifa hili sana, Kiwila itamsuta mpaka anaingia kaburini. Hivyo watanzania hatutashangaa akimtetea Prof Mahalu kuwa hajawahi kuliibia taifa. Mkapa sio msafi- amelihujumu taifa hili kwa kiasi kikubwa. He is an accomplice of Mahalu. It is shame anaitwa kutoa ushahidi wa kumkingia kifua "mwizi". Haturuhusiwi kusema sana kama kesi ipo mahakamani
 
Baada ya Mkapa kutoa ushahidi dhidi ya kesi ya Mahalu nimekuwa najiuliza, DPP alifungua kesi bila kuwasiliana na serikali? Mkapa kasema serikali ililidhia... Kesi ilikuwa ya nini basi? au serikali ilishauriwa vibaya?
Tutafakari pamoja.
 
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Benjamin William Mkapa amejitolea kumtetea Prof. Costa Mahalu,Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Italia na Mkuu wa zamani wa Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dare s Salaam.Prof.Mahalu kwasasa ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo.Anashtakiwa kwa uhujumu uchumi-kununua isivyo halali nyumba ya ubalozi huko Italia.

Ikumbukwe kuwa,wakati Prof. Costa Mahalu alipokuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia,Mkapa alikuwa ndiye Rais wa nchi hii na Rais Jakaya Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Mwaka jana,Mkapa aliandikishwa Kiapo cha Utetezi na Mawakili wa Mahalu wakioongozwa na Wakili Msomi Mabere Nyaucho Marando.Kama hiyo haitoshi,Mkapa jana ameamua kupanda kizimbani kumtetea Mahalu Mhakama ya Hkimu Mkazi-Kisutu,Dar es Salaam.Hoja ya Mkapa ni moja: Mahalu ni msafi,muaminifu na manunuzi yalifuata taratibu zote za kisheria.

Mkapa anatetea maslahi ya nani hasa? Usafi wa Serikali yake?
 
Mkapa anahalalisha wizi/ufisadi wa mali ya umma wa Tanzania.
 
Pengine kweli serikali iliridhia hayo matumizi ya fedha hizo kutokana na report ya uongo ya mheshimiwa.
 
Mi nadhani ni usanii mtupu. Inawezekana kabisa labda Mzee Mkapa anahusika katika hii ishu. Haiwezekani kabisa Katibu Mkuu Kiongozi Mr Lumbanga asiwe anafahamu kuhusiana ununzi huo, na pia haiwezekani waziri wa mambo ya nje wa wakati huo mhe kikwete asiwe hajui kama kina faulo imefanyika. Naamini kwenye hii kesi ya Prof mahalu kuna siri nzito imejificha hapo labda na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje kwa kipindi hicho asaidie kutoa maelezo yake ili ukweli uweze kujulikana .
 
Jk alimuumbua Mkapa kule arumeru.Mkapa alitaka mgombea wa CCM atangazwe hata kama kashindwa. Kilichotea kundi la bab Riz likiongozwa na Napee wakashabikia ushindi wa CDM kama anguko na kumuumbua El.CCM kwa mchezo huu ni bora wajiingize kaburini wenyewe wasisubiri kuzikwa 2015 kwa lazima.
 
Ninaiangalia hii kesi kwa pande hizi
  1. Balozi alitumia mwanya wa kuaminiwa na Mkapa kujinufaisha, tumeona haya katika serikali yetu. Maana Mkapa anasema alipewa taarifa na taratibu za manunuzi zilifuatwa.(Hili ni la kufikirika maana mpaka sasa hata upande wa mashtaka hawajatoa feasible evidence ya kuonesha balozi alidanganya).
  2. 10% lazima ilikuwepo: Hivyo balozi hakugawa hiyo 10% kwa JK na Katibu mkuu kiongozi. Ndio maana JK alimvua ubalozi ghafla (alikuwa na kinyongo naye).
 
Kwenye hii kesi,kama ilivo kwa ile ya akina Mramba pesambili na Yona kuna kujikanganya kwingi mno! Serikali inashtaki watu kisha hiyohiyo inawatetea,acha tumsubirie jk mwenyewe atasemaje naamini atatoa ushahidi wake

Utashangaa Jk haendi kama Batilda na lowasa kwenye Kesi ya Lema A town na bado Mahalu akafungwa Jela...

Tanzania ya JK bana Mungu atusaidie.
 
Ni kweli kuwa hakuna rafu inawezafanyika bila ya aliyekuwa waziri wa mambo ya nje asijue, kama ndivo basi Mh. kikwete atoe ushahidi wa jinsi hiyo nyumba ilivyo nunuliwa maana ni lazima ana some details kuhusu huo mjengo wa Italy.
 
Ni kweli kuwa hakuna rafu inawezafanyika bila ya aliyekuwa waziri wa mambo ya nje asijue, kama ndivo basi Mh. kikwete atoe ushahidi wa jinsi hiyo nyumba ilivyo nunuliwa maana ni lazima ana some details kuhusu huo mjengo wa Italy.
 
Ni kweli kuwa hakuna rafu inawezafanyika bila ya aliyekuwa waziri wa mambo ya nje asijue, kama ndivo basi Mh. kikwete atoe ushahidi wa jinsi hiyo nyumba ilivyo nunuliwa maana ni lazima ana some details kuhusu huo mjengo wa Italy.
kuna HAJA ya kupata mwendelezo wa Kesi hii....
 
Nikijaribu kukumbuka kisa hiki cha nyumba ya ubalozi italia:
Nyumba ilikuwa ni muhimu kununuliwa na kweli ilinunuliwa. Taratibu kiasi fulani zilitumika lakini hapakuwepo na suala la tenda, labda kwa vile nyumba ya ubalozi ni nyeti na inapaswa kuwa katika eneo lenye vigezo maalum ambavyo kwa tenda si rahisi kuvifikia. Hii ndiyo sababu nchi huamua kujenga na si kununua.
Serikali ya TZ iliambiwa na balozi wetu kuwa mwenye nyumba anaiuza kwa dola say 3m,; kutokana na umuhimu wake serikali iliridhia. Sakata lilikuja pale ambapo mwenye nyumba alitoa stakabadhi ya dola say 1.8m ikiwa ni mauzo ya nyumba hiyo. Pakajitikeza tofauti ta say dola 1.2m (vocha ya malipo na receipt ya muuzaji vikatofautiana). Inasemekana kuwa yalikuwepo makubaliano yasiyo rasmi kati ya balozi wetu na muuzaji kuwa bei halisi ya nyumba haikuwa hizo dola say 3m bali zaidi lakini kwa kuwa serikali haikuwa na fedha hizo, walikubaliana kupunguziana kwa masharti kwa muuzaji atoe receipt ya bei ndogo ili alipe kodi kidogo kwa serikali ya italia.
Ni suala hili la kukwepa kodi ya italy lililozusha sakata lote hili. Baada ya serikali ya italia kugundua kuwa serikali ya tz inasema ilinunua nyumba kwa bei iliyo tofauti na bei muuzaji aliyotaja wakati wa kulipa kodi, iliamua kuibana tz na kutishia kuondoa misaada na kutishia kuihamasisha european union kupunguza misaada kwa tz hadi hapo itakapolipwa kodi halali. Muuzaji wa nyumba aling'ang'ania kuwa nyumba aliiuza kwa bei iliyo kwenye receipt, na ndipo ikabidi balozi wetu abanwe ili aeleza hiyo tofauti ilikwenda wapi! Kwa hiyo:
Hatujui bei halisi ya nyumba ilikuwa kiasi gani na kama ilikuwa inflated kuweka cha juu.
Serikali ya italia inasema ni kosa la jinai kukwepa kodi na mtu yeyote anayemsaidia mwingine kukwepa kodi anakuwa ametenda kosa, katika sakata hili ikaelekea kuwa serikali ya tz ilihusika kusaidia ukwepaji kodi. Ili serikali ijivue tuhuma hizi ilibidi Balozi wetu ashtakiwe kama yeye binafsi.

Kama si serikali ya italia kusimama kidete, sakata hili lingeisha kimya kimya.
NB: Mwenye exact figures anaweza kusahihisha, lakini mlolongo wa sakata hilo ndivyo ulivyokuwa.
soma hapahttp://www.zoominfo.com/CachedPage/?archive_id=0&page_id=-1932555383&page_url=//www.ippmedia.com/ipp/guardian/2008/03/15/110417.html&page_last_updated=2008-03-15T17:52:05&firstName=Ricky&lastName=Mahalu
kuwa bei ilkuwa euro 1,032,000 wao wakasema ni euro 3,098,000 wakachakachua euro 2,065,000
 
Ninaiangalia hii kesi kwa pande hizi
  1. Balozi alitumia mwanya wa kuaminiwa na Mkapa kujinufaisha, tumeona haya katika serikali yetu. Maana Mkapa anasema alipewa taarifa na taratibu za manunuzi zilifuatwa.(Hili ni la kufikirika maana mpaka sasa hata upande wa mashtaka hawajatoa feasible evidence ya kuonesha balozi alidanganya).
  2. 10% lazima ilikuwepo: Hivyo balozi hakugawa hiyo 10% kwa JK na Katibu mkuu kiongozi. Ndio maana JK alimvua ubalozi ghafla (alikuwa na kinyongo naye).
Sio hivyo tu hata, JK wakati akiwa waziri wa mambo ya nje alitetea ununuzi wa jengo hilo akisema ulifata taratibu zote za manunuzi na hata hansard za bunge zinaonyesha hivyo

Bila shaka hicho ndo kilichotokea na ndo kinachosababisha yote hayo
 
Back
Top Bottom