ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Kuna wakati nilitembelea kiwanda cha sukari Mtibwa. Katika ofisi ya mkurugenzi. Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Yahya kuna picha kubwa ukutani Mkapa na Mkewe wakiwa na viongozi wakuu wa kampuni hiyo. Mkapa na Mama Anna wamevalia viatua aina ya raba wanaonekana walienda kuvinjari shamba lao la miwa. Kiwanda cha sukari cha Mtibwa ni moja ya viwanda vya umma ambavyo vilibinafsishwa kwa utata mkubwa. Mkapa na familia yake wamepewa shamba la bure ambalo linahudumiwa na kampuni ya Mtibwa yenyewe. Wamiliki wa Mtibwa na Kagera sugar ni kampuni moja ya Super doll.