Mkapa above the law?: Allegations

Hapa serikali ya CCM inatapatapa. Juhudi hizo ni kutafuta mahali pa kupumulia. Sijui kama patapatikana kwa mbinu rahisi namna hiyo.
 
Pinda hapa hajajibu hoja halisi aliyoulizwa. Kihistoria, maswali yote anayoulizwa ndugu Pinda huwa anayajibu kwa style ya kuzungusha maneno bila ya kusema specifically how is he going to tackle the issues... Simwamini kabisa Pinda kwamba ni mtu mwenye machungu na nchi yetu... Yeye ni Waziri Mkuu wa Nchi, na sio publicity Secretary wa serikali. Majibu yake inabidi yakae ki-uwaziri mkuu mwenye dhamana kwa wananchi. Wananchi wanamtegemea yeye kutenda kazi kama Waziri Mkuu na sio vinginevyo.

Tukiangalia mfano wa suala la leo bungeni; Issue ya Mkapa na wenzie iko wazi kabisa kwamba hawa jamaa wamehujumu uchumi wa nchi kwa kutumia vibaya madaraka waliyopewa na wananchi. Hapa kuna haja gani ya "Kufatilia kwa karibu" kama ndugu Pinda anavyotusanifu? Hivi anahitaji apate data gani zaidi ya alizopatiwa mpaka leo hii ili aweze kubaini kwamba Mkapa ana kesi ya kujibu kuhusiana na matendo yake ya kifisadi? Pinda, Are you really serious on this?

Na hao wabunge waliopewa majibu ya kusanii namna hiyo kwa nini hawakumpa kibano cha uhakika?

Nimeshachoshwa na kauli zake zisizo na mwelekeo. Kama ndugu Pinda anaona madaraka aliyopewa ni makubwa kuliko uwezo alio nao, tutamheshimu zaidi kama akiamua ku-step down NOW!!!!...
 
Mkuu nadhani hii niiweke kwa mtindo wa swali kwakuwa bado haijaeleza bayana kuwa anayechunguzwa ni Mkapa. Ila ukweli ni kuwa pamoja na zunguka yote Mkapa ni mmojawapo wa walengwa!
Umejuaje? Una uhakika?
 

Asanteni sana kwa kichekesho cha kufungia wiki. Katiba iliyopo sasa inasemaje kuhusu Raisi Mstaafu?. Mkapa ametumia mwanya wa katiba yetu mbovu kutuibia mabilioni na hana mpango wa kujibu tuhuma wala kurudisha mapesa yetu.

Tulilie katiba mpya kwani bila katiba mpya ukombozi ni kichekesho katika Tanzania yetu.
 

Maneno yako msumari kwa Mkapa ,maana anaweza hata akakuita pembeni akakuwekea hisa ya kukuletea gunia moja la mkaa kila siku.
 

Nani anayefuatilia taarifa hizo? Polisi, TAKUKURU, Ikulu au CCM? Tunataka aweke mambo yote bayana na siyo kuwaacha Watanzania na maswali chungu nzima kuhusu kali yake.
 
Tunapenda mabadiriko yaje huku yakisimamiwa na mafisadi wenyewe hiki ni kichekesho cha karne ya 21.

CCM na serikali yake hawawezi kujiosha hata ipite miaka 1000.

Wametuibia sasa wanapoteza muda ili tusahau aua hoja ikose mwmko.

Ili Viongozi wote wa juu wachukuliwe hatua zinazostahili CCM ni lazima ikae pembeni.

Hoja ya kuiweka CCM pembeni ni hoja inayopakwapakwa mafuta na walio wengi hapa JF na kuikwepa.

Ukweli unajidhihirisha wazi kwamba hakuna Kiongozi wa ngazi yeyote ndani ya CCM na serikali ya CCM mwenye Kende Kubwa za kuwabana Viongozi wote wa juu akiwemo Rais mtaafu na aliyeko madarakani.

Serikali ya CCM kwa vyovyote vile itaendelea kulinda maslahi yake, katika kufanya hivyo ni lazima ilinde Mafisadi wote amabo wengi kati yao ni Makada wa CCM.

Hukumu yeoyote ya haki kwa Majangiri ndani ya CCM haiwezi kutolewa na CCM wala serikali ya CCM. Huku ya haki itatolewa na wananchi kwa kupiga makelele na kufichua hila zao na kuwaabisha viongozi wa wote Mafisadi.

Ili kufanikisha Vita hii kuna haja ya kubadili namna ya kulitazama sakata zima la Viongozi kuiba fedha za umma.
 
Posted Date::4/24/2008
Serikali yachunguza tuhuma kuhusu Rais Mstaafu Benjamin Mkapa
* Ni kuhusu kutumia wadhifa wake kujinufaisha
* Pia yumo Daniel Yona
* Pinda asema ikibainika hatua zitachukuliwa


Na Muhibu Said, Dodoma
Mwananchi

SERIKALI imesema inachunguza tuhuma zilizoibuliwa bungeni wiki hii na Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM) dhidi ya Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona kwamba walitumia vibaya ofisi za umma walipokuwa madarakani, kuanzisha kampuni binafsi kinyume cha sheria.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliliambia Bunge mjini hapa jana, kuwa serikali ina taarifa za tuhuma hizo, ambazo alisema zimeibuka kwa nguvu katika siku za hivi karibuni.

Kutokana na hali hiyo, alisema serikali inazichunguza ili kufahamu ukweli wa kilichotokea na kwamba, ikidhihirika na ushahidi ukapatikana, hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya taifa.

“Suala hilo liliibuka kwa nguvu sana. Tunafuatilia kujua hali halisi ya kilichotokea. Taarifa za kutosha zikipatikana, tutafikia uamuzi utakaokuwa kwa maslahi ya nchi yetu,” alisema Pinda alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo kwa wabunge katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.

Kauli hiyo ya Pinda ambayo ni ya kwanza kutolewa na serikali tangu kuibuliwa kwa tuhuma hizo dhidi ya Mkapa na Yona, inafuatia maswali yaliyoulizwa jana na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed.

Katika swali lake la msingi, Hamad ambaye pia ni Mbunge wa Wawi (CUF), alisema Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Mwaka 1995 , inamzuia mtumishi yeyote wa serikali kutumia ofisi ya umma (serikali) kufanya shughuli binafsi.

“Sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu, kuna taarifa kwamba, Mheshimiwa Rais Mstaafu, Mkapa na kiongozi mwingine wa serikali ya awamu ya tatu, walitumia ofisi zao kuanzisha kampuni binafsi, je, serikali inasema nini juu ya hilo?” aliuliza.

Baada ya Pinda kujibu swali hilo, Hamad aliuliza swali la nyongeza akisema: "Kwa kuwa tuhuma dhidi ya watu hao, ni za muda mrefu, BRELA (Kitengo cha serikali cha Kusajili Makampuni), inalifahamu suala hilo na kuna watu wengine waliobainika kutenda kosa kama hilo walichukuliwa hatua. Kwa nini serikali imekuwa na kigugumizi kuwafikisha mahakamani watu hao?"

Waziri Mkuu alisisitiza kuwa kinachofanywa na serikali hivi sasa ni kuangalia iwapo kuna jinai katika tuhuma zinazowakabili watu hao na kwamba, itakapojiridhisha itachukua hatua zinazostahili kwa maslahi ya nchi.

“Unapelekwa mahakamani ushahidi unapothibiti, tunajaribu kuangalia kosa gani la jinai lililotendeka ndipo tuchukue hatua,” alisema Pinda.

Jumatatu wiki hii, Mbunge wa Vunjo (CCM), Kimaro, alimtuhumu bungeni Mkapa, mkewe,

Anna Mkapa pamoja na Yona, kwamba walinunua Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira (KCML), ulioko Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya kwa kificho.

Kimaro alisema mwaka 2004, Mkapa kwa kushirikiana na mkewe, pamoja na Yona walianzisha Kampuni ya TanPower Resources Ltd na mwaka mmoja baadaye wakauziwa mgodi huo kimya kimya.

Kimaro alisema hayo alipokuwa akichangia Muswada wa Sheria ya Umeme wa Mwaka 2007, bungeni.

Jana Yona alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nchini, akikiri kumiliki hisa katika machimbo hayo na kuwataka wanaohisi kuwa amekosea wamshtaki mahakamani.

Hadi sasa, Mkapa na mkewe Anna wamekaa kimya bila kujibu wala kuzitolea ufafanuzi tuhuma zinazowakabili.

Tuhuma za Rais Mkapa kutumia madaraka yake vibaya kutokana na kuanzisha kampuni zake binafsi akiwa Ikulu, zililipuka kwa nguvu mwaka jana ambapo alidaiwa kwamba, akiwa madarakani alisajiri kampuni yake binafsi ya Anbem Ltd na kukopa fedha benki za kuiwezesha kuanza kufanya kazi.

Pamoja na kwamba fedha hizo alizipata kupitia njia sahihi ya kukopa benki, lakini anatuhumiwa kutumia madaraka yake ya urais kuishawishi benki iliyomkopesha, kumpa fedha hizo.

Tuhuma za kununua Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira, zililipuka mwanzoni mwa mwaka huu pamoja na za Benki M ambayo ilidaiwa kuwa ni yake, ingwa baadaye zilikanushwa kuwa yeye ana hisa tu kwenye benki hiyo na kwamba imepangishwa kwenye nyumba yake.

Kufuatia tuhuma hizo, hadhi ya Mkapa ambaye aliingia madarakani akiwa safi na kujulikana kama 'Mr Clean' inazidi kuporomoka miongoni mwa wananchi mbalimbali, ambao wanaamini kuwa alitumia vibaya wadhifa wake kujipatia mali kinyume na maadili ya uongozi.

Viongozi wa vyama vya upinzani wamelaani kitendo hicho na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake, kwa kuanzia na kumchunguza, licha ya Mkapa kutokuwa tayari kujitokeza na kusema hadharani ukweli wake katika kuhusika kwenye tuhuma hizo, ambazo ni kashfa inayoondoa rekodi yake safi ya uongozi bora mbele ya macho ya jumuiya ya kimataifa.

Pamoja na suala hilo, jana Waziri Mkuu aliulizwa maswali tisa ya papo kwa papo, kuhusiana na masuala mbali mbali yakiwamo nane ya nyongeza.

Wakati huo huo, aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge jana alitinga bungeni, ikiwa ni siku chache tangu ajiuzulu uwaziri kwa tuhuma za kumiliki kifisadi dola za Marekani 1 milioni (Sh1.2 bilioni) alizozificha kwenye akaunti yake iliyoko katika Kisiwa cha Jersey.

Chenge ambaye jana hakukaa katika eneo la mawaziri, anachunguzwa na Taasisi ya Makosa Makubwa ya Jinai(SFO) ya nchini Uingereza, kubaini jinsi alivyopata fedha hizo ambazo anakisiwa kuzipata kwa njia ya rushwa, katika mkakati wa ununuzi wa rada, unaodaiwa kuinyonya serikali ya Tanzania kutokana na kuuzwa kwa bei kubwa zaidi ya ilivyotakiwa kuuzwa.

Zaidi ya Sh70 bilioni za umma zilitumika kununua rada hiyo, ambayo ilipigiwa kelele na wabunge nchini, na baadaye wabunge wa Uingereza walijadili suala hilo katika bunge lao na kumtaka Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair kulitolea ufafanuzi.
 
Time for Mr Clean to ’come clean’(Thisday)


-Ex-president said to be preparing long-awaited response to simmering corruption charges

 
Habari kama hii uliyo ipost MH Mtanzania ni uthibitisho mmoja kwamba Kesi za Mafisadi wote wa CCM akiwemo MH Mkapa ni kesi inayoweza kuhukumiwa kwa haki na wananchi au vyombo visivyo na hisa yeyote CCM.

Ukimya wa wananchi wa Tanzania hususani wale wishio Dar unanishangaza sana.

KWa nini wananchi katika umoja wao hawawezi kuamka kutoka huko waliko alala na kupinga Uovu huu unao watesa wao na mwingine kuja kuwatesa vilembwe wao?

Wako Busy wanafukuza shilingi?

Wote wamepata mgao wa Mafisadi?

Ni woga wa kusema wazi?

Ni upenzi wa kipenzi chao CCM?

Ni ukondoo?

Ni kudhani amambo yatajipiga fimbo na kujipa?

Kesi ya wizi wa mabilioni ya Fedha za Umma uliofanywa na viongozi wa CCM na sasa unalindwa na viongozi hao hao ni kesi inayotakiwa kushughulikiwa na sisi wananchi wenyewe.

Kama tumeshindwa kabisa kuwashughulikia Mafisadi, basi tutafute agent atutafutie watu wengine kutoka nchi nyingine walio tayari kudai haki kwa niaba yetu kwa mfano nchi kama USA, Poland, South Korea,Kenya,Fiji na Comoro.
 
Anayechunguzwa ni mkapa eti kwa maslahi ya taifa
Laini mkuu wa kaya alikataa kuwachunguza ili asijeogopa kuachia ngazi muda ukitimu kuoagopa kuchunguzwa ???? kama pinda anamaanisha aliyosema BIG UP Nampa laikini akumbuke wanainchi wanataka matokeo ya uchunguzi ili maamuzi ya busara yafikiwe kwa uwazi.....ikibidi kinga kwa RAIS mstaafu iondolewe......
 
Confirmed!

Serikali imeanza rasmi kuuchunguza mkataba wa Kiwira kama ulikuwa wa kifisadi na ikigundulika ulikuwa wa kifisadi basi hatua za kisheria zitafuata.

Invisible
 

Wakuu sometimes tujifunze ku-apreciate na kuelewa siasa, so far haya ni maneno mazito sana kutamkwa na kiongozi wa juu wa serikali yetu on this ishu, sasa kweli mtalinganisha haya maneno ya Pinda na ya "tumuache mzee wetu apumzike", wakuu siasa za taifa ni pamoja na uvumilivu,

Believe me mkapa na wenziwe hawawezi kulala usingizi mzuri na haya maneno, lazima saa hizi wanahangaika, this is very strong political statement so far on this ishu, sisi ni kusubiri you never know, watatokea wazungu wengine huko wananchunguza mambo yao halafu wanawakuta michirizi ya hela zinaenda kwa kina kina mkapa, wakisema tu Pinda mwenye atakula maneno yake,

maana sasa nasikia wafadhili wagundua njia mpya ya kuwaabisha viongozi wetu mafisadi, wao ni kujifanya wanchunguza mambo yao na in the process wanataja majina ya mafisadi na hela zao kama Chenge, patamu hapo mwanangu!

Mambo baado kabisa, ndio kwanza yameanza!
 


Mkuu nadahni umeoverlook hiyopost angalia vzr si mimi mkuu.. am very big fun of you you should know today, na kuogopa kwangu kuamini hakujakulenga wewe, nilikuwa na maana kwamba naogopa kuiaminihiyo serikali inayotaka kuchunguza halafu mwisho wa siku wanayeyusha, mfano halisi ni wamafisadi. Mkuu ondoa shaka kabisa lengo letu hapa ni moja tuu
 
Confirmed!

Serikali imeanza rasmi kuuchunguza mkataba wa Kiwira kama ulikuwa wa kifisadi na ikigundulika ulikuwa wa kifisadi basi hatua za kisheria zitafuata.

Invisible

Asante sana invisible, nimefarijika kusikia hii habari, tunaomba huu uchunguzi usichukue mwaka mzima (miezi sita uchunguzi na miezi sita mingine uchunguzi wa uchunguzi)maana kila kitu kiko wazi, wawajibishwe haraka iwezekanavyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…