Hili jambo mtu anaweza kulitazama ktk mitazamo mingi tu.
Kwanza inawezekana watanzania tulizoea na kuridhika na jinsi FAT ilivyokuwa inaendeshwa.Pengine ilikuwa inaendeshwa vizuri zaidi ndio maana ilipoingia TFF ikafanya kazi tofauti na FAT ndio maana tunaona kama sheria zinakiukwa na kuona kama kuna upendeleo na ubaguzi fulani.Na ndio maana watu wanalalamika kwa kuona baadhi ya wanachama wananyimwa haki kugombea nafasi wanazostahili.Maana imekuwa kinyume na mazoea tuliyokuwa nayo.
Lakini pia inawezekana TFF imekuwa bora zaidi ya FAT kwa kuweka taratibu/sheria nzuri zaidi kiasi kwamba zimeweza kuwabana wababaishaji ambao kama ingekuwa ni enzi za FAT wangeendelea kugombea na kuongoza hata kama hakuna mafanikio yoyote kisoka yanayoonekana.Maana sheria ni msumeno haitajali umaarufu wa mtu,bali itaangalia historia ya utendaji wa mhusika ktk nafasi mbalimbali huko nyuma.
Sasa hapa ndipo busara inahitajika zaidi.Tunahitaji kupambanua yote mawili,je ni TFF imekuwa dhaifu kulinganisha na FAT, au ni kwamba tumezoea na kuridhika na jinsi FAT ilivyokuwa ikiendesha soka letu?
Lakini pia ukiangalia upande mwingine wa shilingi.Je ni nani mdhibiti wa TFF hasa pale inaoonekana kutenda kinyume na utaratibu? Je tukae pembeni kuangalia na kulalamika tu? Ni kweli serikali kwa sheria za FIFA haina ruhusa ya kuingilia utendaji wa TFF,lakini je,ikiwa TFF itakiuka utaratibu,itawajibishwa kwa nani? Na pengine kutokana na utaratibu wa unaoongoza mashirikisho yetu ya michezo,inawezekana viongozi wakautumia kunajisi maendeleo ya michezo yetu.
Kituko kingine ni kwamba,inawezekana kweli Mama Mkandara alikuwa hajui utaratibu wa FIFA? Mshauri wake ni nani? OK,sasa ameishajua ameenda kinyume na huo utaratibu,na TFF ni wazi wameishatupilia mbali ile order ya waziri,what is next? Nashukuru nimemsikia Tenga akiomba kukutana na waziri ili kushauriana,fine;waziri kapata fundisho gani hapa?!
Mwisho,naamini Wambura ni mwanasheria,anashindwaje kuifikisha TFF kwenye ngazi ya maamuzi iliyo juu ya TFF kwa mujibu wa utaratibu wa FIFA? Inapotokea anachukua uamuzi wa kudai haki yake kwa kukiuka utaratibu uliowekwa na FIFA na wakati huo anataka kuiongoza TFF ambayo inaongozwa kwa mujibu wa sheria za FIFA,hapa inaleta picha gani? Na sisi bila kujua au kwa makusudi tunajifanya hatujui,tunamuunga mkono,hii nayo ikoje? Wambura inawezekana kweli ana haki ya kugombea,hatukatai,lakini hiyo haina maana kwamba turuhusu utaratibu tuliojiwekea kuvunjwa.