Zawadini
JF-Expert Member
- Feb 2, 2012
- 2,213
- 1,638
Unapaswa kufahamu kwamba utendaji wote kwa Serikali upo chini ya Rais. Mawaziri, kwa mujibu wa katiba,wanafanya kazi kwa niaba ya Rais, hivyo Rais anaweza, kama alivyofanya, kuelekezaWakati wa kusainiwa mkataba wa Muungano, yalikuwa mambo 17. Baadaye yakaongezwa mpaka kufikia 24.
Misaada na mikopo ya nje, ni kweli ni jambo la Muungano. Zanzibar inastahili kupewa asilimia fulani (sina uhakika, lakini nadhani ni asilimia 4). Lakini pesa hiyo hukabidhiwa kwa Serikali ya Zanzibar kwaajili ya kugharamia mambo yasiyo ya Muungano, afya ni mojawapo. Pesa hiyo ikipelekwa Zanzibar, inatumika kwa kadiri ya maamuzi ya Serikali ya Zanzibar na Baraza la wawakilishi. Kwenye hilo msemaji haiwezi kuwa serikali ya JMT wala Rais wa serikali ya JMT. Hili la CT scan, kwa nini maamuzi na msemaji awe serikali ya JMT?