Mkanganyiko katika kutumia herufi "L" na "R"

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
275
Wanajamvi naomba kuuliza haya yanayojitokeza siku hizi kwa wingi katika kuandika na hata kutamka maneno ya kiswahili na kingereza kwa kubadili l na r. Hii inasababisha kubadili maana hasa ya maneno yaliyokusudiwa. Utakuta mtu anatamka neno harufu anatamka halufu. Anataka kuandika Lema anandika Rema. Maana ya maneno huwa inabadilika na wakati mwingine inakuwa ni matusi. Kwa mfano ukienda Marangu utakuta kunaukoo unaitwa Mboro. Ukimwita mwanaukoo Mbolo, utakuwa umemtukana kwani ***** ni korodani kwa kichaga cha vunjo.

Ninajiuliza, Je hili ni tatizo la kuwa na walimu wa vodafasta au ni mabadiliko ya hali ya hewa?
 
L stand for left and R stands for right.
lafudhi huharibiwa na lugha ya asili, kutegemea anakotoka mtu na lugha ya sehemu hiyo. ila ni makosa kwa mtu kuendekeza makosa ya lafudhi tena hasa kwenye kuandika afadhali kutamka yawezekana ilamuwia ugumu mtu kutamka herufi fulani lakini sio kuandika.
tujitahidini kuandika maneno kwa usahihi wake.
 
Lafudhi ya kikabila sio tatizo. Kinachitakiwa mtu pale anapokosea kutamka asahihishwe mara moja. Inasikitisha kusikia mtangazaji anakosea kwa namna hiyo alitakiwa wakati wa "Interview" kiwe kitu cha kwanza kumfanya awe "disqualified", lakini kwa vile watangazaji wanaajiriwa kiundugu undugu ndio hivyo bora liende, halafu wanajiita kioo cha Jamii, huelemisha, kwa namna hii? mmmhh!
 
mimi hilo tatizo la L na R ninalo sana nimejaribu kujilekebisha nimeshindwa lakini kwasababu watu wananielewa hamana tatizo
 
mimi hilo tatizo la L na R ninalo sana nimejaribu kujilekebisha nimeshindwa lakini kwasababu watu wananielewa hamana tatizo
nikweli mkuu naona una hilo tatizo maana hata hapo kwenye red ilitakiwa iwe kujirekebisha!! pole jitahidi
 
Back
Top Bottom