Mkanganyiko baada ya roho kuachana na mwili

Mkanganyiko baada ya roho kuachana na mwili

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,840
Reaction score
861,350
Haya mambo bado yanachanganya wengi kwamba roho inaenda wapi baada ya kuachana na mwili
1.Je inaenda kuzimu?
2.Je inaenda peponi?
3.Je inazaliwa upya?
4.Je inawayawaya na kutangatanga huku na kule?

Maswali yote hapo juu yana majibu yanayofanana, kuwa roho zipo na zinakuwa kote huko kulikotajwa kutegemeana na kwenye uhai wake kidunia zilibeba/ zilifanya nini? Hebu twende moja baada ya jingine.

Kwanza, dini zote zinahimiza matendo mema na maisha baada ya kifo; hata wapagani pia. Hivyo basi, japokuwa maelezo yanatofautiana, lakini msingi unabaki kuwa ule ule wa roho kuwa sehemu husika.

1.Je, roho inaenda kuzimu? Jibu ni ndio

Kwamba bila kujali unaamini nini lakini jehanam iko hapahapa duniani , roho iliyotenda mabaya duniani baada ya kutoka katika mwili uharibikao huingia kwenye mwili mwingine uliojaa mateso tabu na mahangaiko mengi! Kumbuka ili roho iweze kubeba hisia za mateso na maumivu lazima zipate jumba/ mwili!! Hiyo ni jehanam au kuzimu.

2.Je, roho huenda peponi? Jibu ni ndio

Pepo iko hapahapa duniani, roho iliyoishi kwa kutenda mema hubaki mahali kwenye dunia hii ikiwa iko live lakini domant ikiwa haihisi wala kufanya chochote na kama ikibidi kupata mwili huingia kwenye mwili ambao haujui shida za dunia hii kila kitu kwake ni mteremko tu mpaka mwili husika unapochoka na kuharibika/ kufa!! Hii ni peponi.

3.Je, roho inazaliwa upya? Jibu ni ndio japo kimsingi sio kuzaliwa upya bali ni kupata makao/ makazi mapya hapa ndio penye dhana nzima ya reincarnation, ambapo sasa hutegemea matendo ya nyuma Kwahiyo yaweza kuwa kwenye mwili mzuri au mbaya refer pepo na kuzimu.

4.Je, roho zinatangatanga? Jibu ni ndio
kwanza roho huwa hazifi bali kuna wakati hukosa makao mapya/mwili baada ya zamani kwisha na kuharibika
Haijulikani hasa nini hutokea lakini hizi ni roho zenye matatizo makubwa na ndio hizi huwa mashetani majini vinyamkera na viumbe vya ajabu ajabu. Ni roho hizi hizi ambazo huweza kuingia kwenye familia kikundi au mkusanyiko wowote na kuleta mirafaruku mikubwa tu ambayo mingine huleta maafa makubwa.

Kwahiyo roho zipo na zipo sana na kamwe hazifi wala hazipotei jehanam, na pepo zao zipo hapahapa duniani na kwenye kila nyanja ya maisha yetu ikiwemo JF.
 
....mkuu mshana jr unataka kujibiwa kwa muktadha upi ? Wa kiroho ? au wa kisayansi..? anyway twende na kiroho. Swali lako ni rahisi sana kama utalitazama katika mtazamo Wa kiroho tena kama mkristo.

Sisi tunaamini Mara baada ya kufa kila roho inakwenda mahali pa kusubiri hukumu ya mwisho. Kama sikosei mahali hapo panaitwa toharani kwa wwale wakiokufa ktk dhambi. Wataendelea kupata mateso kama kiu n.k. na wale wakiokufa ktk bwana watakwenda mahali pazuri huku wakisubiri kuingia mji wa ahadi ambao Yesu anawaandalia.

Kumbuka habari ya Lazaro na yule tajiri. Tajiri Mara baada ya kufa dhambini alimuona Lazaro amabaye alikuwa masikini akiwa ubavuni mwa Yesu na yeye ukiwa kwenye mateso akamuomba angalau maji ya kunywa tone moja kupoza kiu yàke. ....
 
Last edited by a moderator:
Gefu ni sahihi kabisa kitu ni hichocho bali kwa maelezo mengine hasa kulingana na imani ya kikristo. Nenda pale Muhimbili wodi ya Sewa Haji wale wagonjwa wa kinywa na koo wanatamani kunywa lakini tone moja kupita kooni ni ishu! Unajua haya mambo tunaishi nayo ni kwa kuwa tu tumezingwa na changamoto za kidunia.
 
Tusilemazwe na hii tabia ya kutafuta chanzo cha habari wakati kuna wakati mtoa mada ndio chanzo baada ya kusoma na kufanya utafiti binafsi bila kuegemea mabandiko ya wazungu

hii mada inaongelewa wafu, ninavyojua mimi binadamu akipoteza uhai (mfu) basi hana uwezo wowote ule na kwa namna yoyote ile kuwasiliana na binadamu alie hai. Nachotaka kujua ni msingi wa utafiti wako uliota ndotoni au wewe ni yule tuliekuwa tunamtazamia na sasa umekuja 'kidigital'
 
Kwa kifupi mtoa mada unapotosha watu. Mtu akifa kinachofuata ni hukumu tu soma waebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja na baada ya kufa hukumu. Hapo unaona pia hakuna habari za toharani muda wa kutengeneza mambo ni hapa duniani ukiwa hai basi.

Ni vema ukaokoka hata ukifa uwe salama huko uendako.
 
jmoses Ambako ni wapi huko uendako? Sijapotosha mtu soma tena kwa makini na habari za kiama parapanda na ufufuko wa mwisho
 
Last edited by a moderator:
Mmmhh, aisee haya mafundisho yako yamebase katika nini? Ni uelewa wako binafsi au Biblia au Quran?
 
mtzmweusi Wee yalinganishe tu na uhalisia utagundua kitu.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom