Mkanda wa Soweto: Aliyenao anipe niupeleke ICC

Mkanda wa Soweto: Aliyenao anipe niupeleke ICC

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Nauhitaji sana mkanda wa mabomu ya Soweto,Arusha. Natamani kuiona nchi na wahusika wakitubu na kuwajibika kabla ya kuingia awamu ya tano. Mauaji ya Arusha yalisikitisha na kuhuzunisha.

Bahati njema,nitakuwa safarini katika nchi mbalimbali za Ulaya hivi karibuni. Mojawapo ni Uholanzi ilipo Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC). Nitaupeleka mkanda wa Soweto bila woga wala mawaa.

Nitoe rai kwa aliyenao. Nauomba niufanyie kazi. Mhusika ashughulikiwe kimataifa. Marehemu wa Soweto,Arusha wanasubiri hatua dhidi ya wauaji wao. Tuwatendee haki watanzania wenzetu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba ( sasa Dodoma)
 
Utapewaje na wewe uko CCM ambao ndo watuhumiwa kwa kutumia jeshi la polisi! Mkanda utatolewa kwa tume ya kijaji ikiundwa!
 
Mkanda utatoka muda mwafaka ukiwadia lakini kabla au wakati wa kampeni uchaguzi mkuu.
 
ICC inashughulikia makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, Crimes against humanity, genocide na atrocities, na war crimes kama kutumia watoto vitani, hayo ya soweto hayaqualify kwenda the ICC, jurisdiction za ndani zina uwezo wa kushughulikia, kama tume ya haki za binadamu na utawala bora,
 
angalia tu usijepewa mkanda wa katuni za madagascar maana chadema hawaishi vituko.
 
Utapewaje na wewe uko CCM ambao ndo watuhumiwa kwa kutumia jeshi la polisi! Mkanda utatolewa kwa tume ya kijaji ikiundwa!

Atakachopewa ni copy ya DVD na original si itabaki. Jee hata mahakama ya Hague ni ccm. Mbona wa kenya wamepeleka ushahidi na mashahidi bila kusubiri Uhuru kenyata kuunda tune yake. ni lazima marehemu wapate haki yao na wahusika wakamatwe. Hata kama ni Raisi
 
Mzee Tupatupa tangaza rasmi kuwa unajitoa sasa hivi huko Lumumba na utapewa huo mkanda mara moja. Hata hivyo matukio ya Soweto ni ya kijinai na kosa la jinai halichachi hata likikaa miaka 10. Ushahidi ule kuna siku utatumika mahakamani pale tuu ambapo wahusika watakapo kosa back up ya serikali ndio watakapojua kuwa kumtumikia shetani hakulipi kwani kuna wakati huwa hapatikani kukubeba.
 
Kwa mbwembwe hujambo mara nilikuwa safarini ulaya,uholanzi n.k ni ashomile wa kule bukoba nini?
Mkanda utatoka muda mwafaka ukiwadia lakini kabla au wakati wa kampeni uchaguzi mkuu.
CHADEMA walisema wanao.walipokomaliwa wautoe wakabidhi vyombo vya dola. Wakatokomea mitini na uwongo wao kama kawaida yao.
 
Kuna documentary moja ipo mtaani kuhusu vurugu mbalimbali ktk mikutano ya cdm, ya arusha ni mojawapo...AU KUNA NYINGINE?
 
sina imani kwamba huo mkanda upo, unless uwepo na wameupanga kuutoa siku chache kabla ya uchaguzi mkuu ili kuwapunguzia ccm wapiga kura...yaleyale za zitto na mabilioni ya uswisi.
 
Hama Kwanza Hapo Lumumba Maana Mwanzo Wa Jina Unapoish Ndo Hayo Tunayo Yachukia,,,
 
Wenye nao (kama upo) wanajua na ICC ilipo. Kama wanataka uende huko wanaweza kuupeleka bila ya kutafuta mtu wa kati kama Mzee tupatupa wa Lumumba...
 
Kwa mbwembwe hujambo mara nilikuwa safarini ulaya,uholanzi n.k ni ashomile wa kule bukoba nini?
Mkanda utatoka muda mwafaka ukiwadia lakini kabla au wakati wa kampeni uchaguzi mkuu.
CHADEMA walisema wanao.walipokomaliwa wautoe wakabidhi vyombo vya dola. Wakatokomea mitini na uwongo wao kama kawaida yao.

Aliyetaka kupewa ni Kamanda Chagonja, yule ni ccm kindakindaki, wao cdm ninavyojua walitaka tume ya kijaji iundwe ili ushahidi upelekwe mpaka leo haijaundwa. Wala msijali kwani ule mkanda hauzi ni lazima ukweli utadhihiri tu. Muda upo wa kutosha na wengi walioshirini ni vijana watakuwepo tu kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
 
aliyetaka kupewa ni kamanda chagonja, yule ni ccm kindakindaki, wao cdm ninavyojua walitaka tume ya kijaji iundwe ili ushahidi upelekwe mpaka leo haijaundwa. Wala msijali kwani ule mkanda hauzi ni lazima ukweli utadhihiri tu. Muda upo wa kutosha na wengi walioshirini ni vijana watakuwepo tu kufikishwa kwenye mkono wa sheria.

onyesha ushahidi kuwa chagonja ni ccm
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom