Mkakati wa Wazi: CHADEMA 2014/2015 kufanya mapinduzi ya mawasiliano na Ushirikishaji.

Asante Betlehem kwa mchango wako. Noted. Bila shaka nawe unajisikia vyema kuona kuwa mengi kama si yote uliyoyasema hapa yanatekelezwa kila siku. Mengine si lazima tuyaanike hapa. Tunashukuru sana kwamba wewe ni miongoni mwa Watanzania mamilioni, wanaamini, wana matumaini makubwa na wanaipenda CHADEMA.

Kila mtu aone kuwa ni jukumu lake na wajibu wake kuwa rasilimali (kwa njia mbalimbali) kwa ajili ya CHADEMA na mabadiliko.

Mkuu safi sana nimefurahi kwa kujitokeza leo na hasa kwenye hoja ya maana na yenye kujenga kama hii na ku-comment!

Unajua wewe ni miongoni mwa viongozi wakubwa tu ndani ya chadema na ambao mnapaswa kuaminika,lakini sometimes cheo chako kinachezewa tu na watoto watoto flani hivi ambao wamejifunza siasa za maji taka eti nao wanakuja hapa na kujifanya ni wasemaji wa chadema!!

Safi kaka!
 
Yani wewe siku unaniambia unaondoka ccm niliumia sana lakini nilipiga moyo konde kwa sababu wewe ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanaeleza ukweli na mikakati mizuri sana lakini kwa sbb tu ya baadhi ya viongozi Mamangimeza yakawa yanabeza!!

Anyway maisha popote wanasema waswahili,mimi ngoja niendelee kupelekeshana nao ingawa mkuu kwa sasa wameshaanza kuona hali ambayo tulikuwa tunaipigania na kuisema kila wakati!

Unajua baadhi ya viongozi wa ccm ni sawa na wale wawindaji ambao hata ukimuonya kwamba hapo kuna nyuki anabisha tu mpaka wamuume ndio anastuka.

Ila mkuu hongera sana kwa maoni yako ni kazi tu kwa viongozi wa chadema kufanyia kazi ingawa na wao kuna baadhi ya viongozi wao ambao ni Mamangimeza!

Ingawa chadema ni chama ambacho kilikuwa tayari miongoni mwa watu walio wengi wakiacha ubabe waliouanza hasa juu ya madaraka kama ma-ccm basi tunaweza kufanya kitu.
Mkuu WABHEJASANA wakati fulani unanipa raha sana kwa comment zako. Nawe unaanza kubadilika kidogo kidogo! Tehe! haya mambo bwana!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu WABHEJASANA wakati fulani unanipa raha sana kwa comment zako. Nawe unaanza kubadilika kidogo kidogo! Tehe! haya mambo bwana!

Kaka unajua kuna watu humu huwa wanajifanya kwamba wao wanajua sana kusema mambo,lakini bahati mbaya sana huwa hawajui kwa sbb wanafanya siasa chafu na zaidi ya yote ni ushabiki tu!

Kuna maeneo ambayo ushabikia hauna nafasi hata kidogo!

Kama ni suala la kubadilika mimi nilishabadilika siku nyingi sana na fuatilia lile kundi la umoja wa vijana la miaka minane iliyopita ulilokuwa unasikia linadaiwa ni wasaliti kama anavyodaiwa zitto hivi sasa,nami nilikumo kwenye kundi hilo!

Lakini nataka nikwambie hatukuwahi kufanya uasi hata siku moja isipokuwa tulikuwa na slogan ya kuwapinga baadhi ya viongozi ambao kwanza wanang'ang'ania madaraka,lakini pili hizi nafasi wanazifanya ni za ukoo,wanapeanapeana tu kama karanga!

Wenzetu walau wamepata nafasi ndani yq bunge na hata U-DC na U-RC pamoja n sekta mbalimbali,lakini bado tunasonga mbele kinachotakiwa ni haki kwa sbb kila mtanzania wa nchi hii ana haki ya kuongoza na kuka mema ya nchi mahali popoteaipo!

Mimi kiukweli mpaka sas sina imani na ccm kwa asilimia 100,na vivyo hivyo hata kwa vyama vingine tofauti na ccm kwa sbb ukivichunguza kwa umakini sana,utagundua kwamba vinafananafanana sana,kimfumo,kiutendaji,kimatukio!
 
Last edited by a moderator:
Kuna limitations kadhaa pia ilikupasa kuzizingatia kabla ya kufikia hitimisho, nitazitaja hapa na kuzitolea maelezo kiasi.

1/ Tamaduni au mazoea
Japo ni kweli matumizi ya simu yameenea sana Tanzani lakini bado mazoea ya kutuumia kifaa hiki kama njia ya kujielimisha hayajasambaa kabisa. Bado watanzania wengi wanatumia simu zao strictly kwa mawasiliano ya kijamii na si kujielimisha. Ujumbe kwenye simu bado haupewi uzito sawa na ule utolewao ana kwa ana.

2/ Idadi ya maneno katika ujumbe

Kuchagua kutumia ujumbe wa simu maana yake ni kwamba unakuwa umejiwekea kizingiti cha idadi ya maneno utakayotumia kufikisha ujumbe. Kwa siasa hii ni hasara kubwa kwakuwa mtaji wa siasa ni maneno, ujumbe wa siasa hufika ipasavyo kwa kutumia maneno mengi, fursa hii haipo kwenye simu labda utume sms nyingi kitu ambacho kinaweza kuwakera wateja( rejea yale malalamiko ya wateja wa Tigo kwenye zile sms za bahati nasibu)

3/ Hakuna fursa ya kujitetea

Iwapo kutakuwa na kasoro katika ujumbe uliotumwa au tafsiri zaidi ya moja basi mtoa mjumbe atakosa fursa ya kujitetea hapo kwa hapo. Ujumbe ukitumwa utafika hivyo hivyo na inampa mpokea ujumbe nafasi kutafsiri anavyotaka hadi hapo tafsiri nyingine itakapomfikia. Uharibu ukitokea ni kazi sana kuuziba hasa kwa kutumia njia ile ile iliyousababisha.

4/ Hakuna fursa ya kuonesha hisia

Pengine hili ni kubwa kuliko yote kwakuwa mtaji mkubwa wa siasa ni zile hisia mbalimbali unazozibeba kwenye kila ujumbe. Kutumia ujumbe wa simu kunamkosesha mwanasiasa kuonesha hasira, huzuni, masikitiko,furaha au majonzi kwenye sura yake. Hisia ni muhimu sana kumfanya mtu akuamini wewe mtoa ujumbe na pia auamini ujumbe wako.

5/ Muda mwingi utatumika kuandaa ujumbe

Kutokana na uchache wa maneno yanayotakiwa kwenye ujumbe, huchukua muda mrefu kuandaa ujumbe mmoja tu. Kama hiyo haitoshi ujumbe utakaoandaliwa pia hupitia milolongo mingi ya majaribio (pretesting) kabla ya kukubaliwa. Hii inapoteza sana muda hasa ukizingatia muda wa wanasiasa ni mali sana.
betlehem angalia hizo na kisha niambie iwapo ukiongeza kwenye mizani yako bado njia hii inakuja juu ya hizo nyingine.
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na hayo Mkuu, Kitu rahisi zaidi kwa mawasiliano ya watu wengi kwa muda mfupi,
Ni Chadema Taifa Kutafuta namba maalum, Mfano zile za Radio One ili kila mtu anaetaka kupata taarifa zote Chadema atume neno CHADEMA kwenda 15... hapo hapo chama kitakua kinajipatia mapato kupitia huo mtandao wa Push Mobile kwa Mujibu wa TCRA
 
mkuu sehemu nyingine ya mchango wako sitajibu kitu kwa sababu nikijibu muelekeo wa mada hii utapotea.Mimi nimevutiwa na mchango wako hapo chini.

Mkuu umejikuta ukiwa "Wakushuku" Tehe! tehe! tehe! Katika vitu ambavyo vinanipa raha na kunikumbusha mbali sana ni pale ninapomuona mtu akiwa anashukushuku mambo.Licha ya wakati fulani watu kushuku mambo bila sababu, wakati fulani wanashuku mambo kwa sababu za msingi kabisa. Nakumbuka hoja ya "Ndoto" ja jaama mmoja mwanafalsa descartrs ambaye alibobea sana kwenye kushuku mambo. Jamaa anakuambia "Unapokuwa kwenye ndoto unakuwa unaona mambo ukidhani ni sahihi na ya ukweli na unapokuja kugundua kwamba hayakuwa ya ukweli ni pale unapotoka usingizini, kisha anahoji ni kivipi tunaweza kuwa na uhakika na kuthibitisha mambo tunayoyaona kwamba ni halisia na ukweli bila ya shaka" Mkuu utashuku sana CCM , na baadae unaweza kuhamia chama kingine ukawa unashuku vile vile.Duniani kuna binadamu wa kila aina na binadamu hawatabiriki sana.Mifumo yote duniani huundwa na wanadamu. Chamsingi ni kutekeleza wajibu wako na kutumia akili yako uwezavyo.
 
Mkuu huo utaratibu sio rafiki kwa watanzania wengi kwa kuwa watakuwa wanakatwa hela wao na hawatapata taarifa wanayoitaka kwa wakati.Na niyule tu atakayeomba taarifa ndiye atakayepata.Utaratibu huo si rafiki sana.Hata hivyo kupitia utaratibu huo, mwananchi hawezi kutoa taarifa au ushauri bali yeye hupokea tu halafu si lazima apokee anachokitaka kwa wakati.
 
Kuna limitations kadhaa pia ilikupasa kuzizingatia kabla ya kufikia hitimisho, nitazitaja hapa na kuzitolea maelezo kiasi.

1/ Tamaduni au mazoea
Japo ni kweli matumizi ya simu yameenea sana Tanzani lakini bado mazoea ya kutuumia kifaa hiki kama njia ya kujielimisha hayajasambaa kabisa. Bado watanzania wengi wanatumia simu zao strictly kwa mawasiliano ya kijamii na si kujielimisha. Ujumbe kwenye simu bado haupewi uzito sawa na ule utolewao ana kwa ana.

2/ Idadi ya maneno katika ujumbe

Kuchagua kutumia ujumbe wa simu maana yake ni kwamba unakuwa umejiwekea kizingiti cha idadi ya maneno utakayotumia kufikisha ujumbe. Kwa siasa hii ni hasara kubwa kwakuwa mtaji wa siasa ni maneno, ujumbe wa siasa hufika ipasavyo kwa kutumia maneno mengi, fursa hii haipo kwenye simu labda utume sms nyingi kitu ambacho kinaweza kuwakera wateja( rejea yale malalamiko ya wateja wa Tigo kwenye zile sms za bahati nasibu)

3/ Hakuna fursa ya kujitetea

Iwapo kutakuwa na kasoro katika ujumbe uliotumwa au tafsiri zaidi ya moja basi mtoa mjumbe atakosa fursa ya kujitetea hapo kwa hapo. Ujumbe ukitumwa utafika hivyo hivyo na inampa mpokea ujumbe nafasi kutafsiri anavyotaka hadi hapo tafsiri nyingine itakapomfikia. Uharibu ukitokea ni kazi sana kuuziba hasa kwa kutumia njia ile ile iliyousababisha.

4/ Hakuna fursa ya kuonesha hisia

Pengine hili ni kubwa kuliko yote kwakuwa mtaji mkubwa wa siasa ni zile hisia mbalimbali unazozibeba kwenye kila ujumbe. Kutumia ujumbe wa simu kunamkosesha mwanasiasa kuonesha hasira, huzuni, masikitiko,furaha au majonzi kwenye sura yake. Hisia ni muhimu sana kumfanya mtu akuamini wewe mtoa ujumbe na pia auamini ujumbe wako.

5/ Muda mwingi utatumika kuandaa ujumbe

Kutokana na uchache wa maneno yanayotakiwa kwenye ujumbe, huchukua muda mrefu kuandaa ujumbe mmoja tu. Kama hiyo haitoshi ujumbe utakaoandaliwa pia hupitia milolongo mingi ya majaribio (pretesting) kabla ya kukubaliwa. Hii inapoteza sana muda hasa ukizingatia muda wa wanasiasa ni mali sana.
betlehem angalia hizo na kisha niambie iwapo ukiongeza kwenye mizani yako bado njia hii inakuja juu ya hizo nyingine.

Yale ni mawazo yake na haya ni yako mkuu,yote ni mema ahsante kwa kuongezea nyama taarifa ha betlehem
 
Last edited by a moderator:
Kuna limitations kadhaa pia ilikupasa kuzizingatia kabla ya kufikia hitimisho, nitazitaja hapa na kuzitolea maelezo kiasi.

1/ Tamaduni au mazoea
Japo ni kweli matumizi ya simu yameenea sana Tanzani lakini bado mazoea ya kutuumia kifaa hiki kama njia ya kujielimisha hayajasambaa kabisa. Bado watanzania wengi wanatumia simu zao strictly kwa mawasiliano ya kijamii na si kujielimisha. Ujumbe kwenye simu bado haupewi uzito sawa na ule utolewao ana kwa ana.
Mkuu ni kweli ila walau hakuna mtu anayefuta sms bila kusoma.TCRA wanajua hii kitu na wanajua nguvu ya sms Tanzania katika kujenga au kubomoa jamii na ndio maana wakaja ya kampeni ya "Delete" kwa hiyo sms zina nguvu ya ajabu sana!.

2/ Idadi ya maneno katika ujumbe

Ni kweli ila utafiti unaonesha watanzania wengi hawapendi kusoma mambo mengi. Kwa mfano mimi mwenyene niliandika kitabu chenye kurasa chini ya 100 lakini wengi walilalamika kikubwa mno.Wanzania wanapenda kusoma summary ya vitu.

3/ Hakuna fursa ya kujitetea

fursa ipo kwenye eneo hili kwa kuwa mtu anaweza kujibu ujumbge au hata akapiga simu kuhoji aeleweshwe zaidi.Hii nhi tofauti kabisa na mbinu nyingine kama magazeti na tv.
4/ Hakuna fursa ya kuonesha hisia

Ni kweli ila haja JF na kwenye magazeti hakuna fursa hiyo sana.Hata hivyo si kila taarifa inayohitaji hisia.Taarifa nyingine ni objective zaidi.

5/ Muda mwingi utatumika kuandaa ujumbe

sio kweli. Kuandika ujumbe mmoja unacommand kwenye system uende kwa watu wengi ni kazi rahisi tu.
 
Ni muda sasa nimekuwa sikubaliani na maudhui ya posts zako nyingi (sio zote) ulizokuwa unazipost hapa JF siku za hivi karibuni. Baadhi ya posts nilikuwa nakubaliana na wewe partially....

Kwa mara ya kwanza nakubaliana na wewe kwa 100%.

Mimi bado kwani anapo niambia Watanzania wengi wanaona Maandamano ni Fujo, nashindwa kumuelewa wengi wa wapi? Amefanya wapi hiyo sensa?

Kizazi cha sasa ni kizazi cha Vijana na kimekulia kwenye maandamano tokea Primary, sasa unaponiambia Mandamano ni fujo Simuelewi.

Kama yupo tayari anialike Mtaani kwao nije tufanye sensa ya wapenda maanda$ano na wasio penda. Nipo Tayari kwa gharama zangu.
 
mkuu sehemu nyingine ya mchango wako sitajibu kitu kwa sababu nikijibu muelekeo wa mada hii utapotea.Mimi nimevutiwa na mchango wako hapo chini.

Mkuu umejikuta ukiwa "Wakushuku" Tehe! tehe! tehe! Katika vitu ambavyo vinanipa raha na kunikumbusha mbali sana ni pale ninapomuona mtu akiwa anashukushuku mambo.Licha ya wakati fulani watu kushuku mambo bila sababu, wakati fulani wanashuku mambo kwa sababu za msingi kabisa. Nakumbuka hoja ya "Ndoto" ja jaama mmoja mwanafalsa descartrs ambaye alibobea sana kwenye kushuku mambo. Jamaa anakuambia "Unapokuwa kwenye ndoto unakuwa unaona mambo ukidhani ni sahihi na ya ukweli na unapokuja kugundua kwamba hayakuwa ya ukweli ni pale unapotoka usingizini, kisha anahoji ni kivipi tunaweza kuwa na uhakika na kuthibitisha mambo tunayoyaona kwamba ni halisia na ukweli bila ya shaka" Mkuu utashuku sana CCM , na baadae unaweza kuhamia chama kingine ukawa unashuku vile vile.Duniani kuna binadamu wa kila aina na binadamu hawatabiriki sana.Mifumo yote duniani huundwa na wanadamu. Chamsingi ni kutekeleza wajibu wako na kutumia akili yako uwezavyo.

Mkuu samahani kama nitakuwa sijakuelewa vizuri pengine!

Unajua suala la kushuku ni moja ya mafanikio ama ya kujua jambo,huwezi kujua tu jambo bila kushuku

Ninachoamini mimi kwa mtu makini lazima ni kwamba ili taarifa ikamilike ama upate ukweli wa jambo flani ni lazima haya hapa chini yapate majibu!

1: News worth(issues,Agenda)
2: Source & Sourcing
3: Attribution
4: Assumption
5: Specificity
6:Accountability
7: Balance & sense if Judgement
8: Quots & Data
9:Language pamoja na
10: Background.

Ndiyo maana nikasema kwamba kiukweli kutoka moyoni mwangu sina Imani na vyama vyote vya siasa hapa nchini kwa asilimia 100 kama kweli vipo kwa ajili ya maslahi ya jamii na hasa kama utafiti wako utajikita kwa mambo hayo 10 hapo juu!!

Vyama vingi hapa nchini ni migogoro,majungu,fitina na unafiki usiokiwa na maendeleo,wenzetu pia wana vyama vingi lakini wakati wote hawana majungu,fitina wala umafia wa ajabu ajabu kama wa wanasiasa wetu wa huku!,wako serious na siasa na wanaifanya kweli na ndiyo maana wanapata mafanikio!

Kwetu hapa chukua hivyo vigezo kumi vifanyie kazi utakubaliana na mm kwamba hakuna chama ambacho kina dhamira ya dhati kwa asilimia 100 kutumika kwa wananchi,vingi vinaongozwa na watu maslahi!

Ingawa kidoogo vinatofautiana hasa pale unapotafuta unafuu,na hakuna ubishi kwamba walau CHADEMA ni nafuu more than CCM!!!

Tatizo tu ni kwamba bado watu maslahi wanakikodolea macho!
 
Kwa hapa tulipo useme tu ukweli TV station ni ishu isiyokwepeka kwa CDM, hayo yote kayaongea Bethlehemu ni sahihi lakini ukiwaza kwa undani ni lazima kuangalia mitandao hii iko safi kiasi gani ukizingatia wamiliki ndo hao hao wapinzani wenu,hapa pia tuwe tayari kuhujumiwa na kitakachofuata mtadespair na kurudi nyuma

TV ni bora zaidi na ishu za matangazo si tatizo sana kama mna watu makini wa fani husika eventually kituo kinaweza kujiendesha hata kwa 70% ni nzuri sana,chako chako bwana.
 
Kuna limitations kadhaa pia ilikupasa kuzizingatia kabla ya kufikia hitimisho, nitazitaja hapa na kuzitolea maelezo kiasi.

Mkuu ni kweli ila walau hakuna mtu anayefuta sms bila kusoma.TCRA wanajua hii kitu na wanajua nguvu ya sms Tanzania katika kujenga au kubomoa jamii na ndio maana wakaja ya kampeni ya "Delete" kwa hiyo sms zina nguvu ya ajabu sana!.

Ni kweli ila utafiti unaonesha watanzania wengi hawapendi kusoma mambo mengi. Kwa mfano mimi mwenyene niliandika kitabu chenye kurasa chini ya 100 lakini wengi walilalamika kikubwa mno.Wanzania wanapenda kusoma summary ya vitu.

fursa ipo kwenye eneo hili kwa kuwa mtu anaweza kujibu ujumbge au hata akapiga simu kuhoji aeleweshwe zaidi.Hii nhi tofauti kabisa na mbinu nyingine kama magazeti na tv.
Ni kweli ila haja JF na kwenye magazeti hakuna fursa hiyo sana.Hata hivyo si kila taarifa inayohitaji hisia.Taarifa nyingine ni objective zaidi.

sio kweli. Kuandika ujumbe mmoja unacommand kwenye system uende kwa watu wengi ni kazi rahisi tu.

Nahisi hujanielewa kwenye kuandika ujumbe, wacha nitoke gym ntakuelewesha.
 
mkuu bado tu uko Gym? salama lakini au kuna opereshen unaenda kuifanya maana gym toka jana mpaka sahizi unanitisha ujue!

Nilikuwa nimebanwa na jukumu la kupitia rasimu ya pili ya katiba mkuu betlehem. Kuhusu kuandika ujumbe sikuwa na maana ya ku type la hasha, nilikuwa na maana ya ku construct/ au kutunga ujumbe utakao tumika. Zoezi hili likifanywa ipasavyo sio kazi ya siku moja maana linahusisha kupitia malengo ya ujumbe, walengwa wa ujumbe na uchambuzi wa lugha ya ujumbe. Baada ya kukubaliana juu ya ujumbe, kuna kazi ya kuufanyia majaribio huo ujumbe( pretesting) ambapo inaweza kukurudisha kwenye ubao wa kuchorea tena. Mkuu japo mimi sio mtaalamu wa mawasiliano ila katika ujasiriamali wangu nimewahi kushiriki kwenye kampeni kubwa za kitaifa zilizotumia ujumbe wa maandishi, nakuapia ni kazi kubwa kuunda ujumbe mzuri.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom