Mkakati wa Wazi: CHADEMA 2014/2015 kufanya mapinduzi ya mawasiliano na Ushirikishaji.

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,605
2,000
Wadau salaam!

Katika Taasisi yeyote ya kisiasa ya kidemokrasia,mawasiliano/taarifa zina nguvu isiyokuwa ya kawaida.Ushirikishwaji wa wananchi wa level zote huongeza nguvu hiyo mara dufu.Kwa sababu hiyo basi, kwa kadiri taasisi ya siasa inavyozidi kuwa na taarifa/ za kutosha na za kuaminika ndivyo taasisi husika inavyopata nguvu zaidi na kinyume chake.Kwa kadiri wananchi wanavyoweza kuwa na taarifa za kutosha na kuaminika juu ya taasisi husika, ndivyo taasisi inavyozidi kupata nguvu na kinyume chake.Kadhalika kwa jinsi taasisi inavyo washirikisha wadau zaidi na zaidi ndivyo inavyopata mawazo mengi zaidi na kadiri inavyopata mawazo mengi zaidi ndivyo inavyoimarika zaidi na kinyume chake.

CHADEMA kama taasisi ya kisiasa inaonekana kulitambua hilo na hivyo kubuni mbinu mbalimbali za mawasiliano kuhakikisha taarifa zinazotoka kwenye chama zinafikia umma na zinazotoka katika umma zinafikia chama n.k.Nitaeleza kwa kifupi mbinu zinazotumika zaidi kwa sasa faida zake na changamoto zake.

(A.)MIKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI.

FAIDA ZA MBINU HII.

1. Huwawezesha Viongozi wa chama kufikisha taarifa/ mawazo yao/msimamo wa chama kwa umma.
CHANGAMOTO
1.Wanahabari hufikisha taarifa kulingana na mitizamo yao juu ya taarifa yenyewe.
2. Mtizamo wa mmiliki wa chombo cha habari huweza kusababisha taarifa isitolewe.
3. Mfumo huu huwezesha taarifa/ maoni kwenda kwa upande mmoja tu; yaani kutoka juu (kwa viongozi kwenda chini)
4. Njia hii hufikisha taarifa kwa watu wachache tu katika umma ambao wanavifikia vyombo husika.
5. Mbinu hii haishirikishi umma kwa namna yeyote.

(B). KUTUMIA MIKUTANO YA HADHARA.

FAIDA YA MBINU HII.

1. Huwezesha kufikia kundi kubwa la watu kwa wakati mmoja.
2. Umma humuona msemaji/kiongozi na hivyo kupata hamasa zaidi.
3. Kunakuwa na mawasiliano kutoka kwa pande zote kutoka kwa kiongozi na kwa umma kupitia maswali.
CHANGAMOTO.

1.Muda wa mikutano unakuwa unabanwa mno hivyo kuleta ugumu kwa umma kuuliza maswali na kutoa ushauri.
2. Kwa kawaida umma huwajibika kuuliza ndani ya topic iliyozungumziwa tu!
3.Idadi ya wahudhuriaji wa mikutano ni ndogo kuliko wasiohudhuria.
4.Kuna aina ya watu hata kama wana maswali au ushauri hawawezi kutoa kwenye mikutano ya hadhara.
C. MAANDAMANO.
FAIDA.
1.Huibua hamasa kwa umma
2. Huonesha mshikamano miongoni mwa wadau.
3. Huonesha hisia za wadau.
CHANGAMOTO.

1. Watanzania wengi hawapendi mikikimiki hivyo wanaosalia majumbani ni wengi kuliko wanaoshiriki maandamano.
2.Mikimiki ya maandamano wakati fulani husababisha fujo na hivyo kuwa kero kwa baadhi ya watu.
3.Maandamano wakati fulani huingiliwa na kusababisha vifo na hasara.
4. Watanzania wengi bado wanatazama maandamano kama kitendo cha fujo kutofuata taratibu na kitu cha hatari kwa washiriki.

D. MITANDAO YA KIJAMII


FAIDA.
1.Ni mfumo wa haraka sana wa kufikishia watu taarifa.
2. Taarifa huuenda kwa pande zote mbili; yaani kutoka kwa chama kwenda kwa umma na kutoka kwa umma kwenda kwa chama.

CHANGAMOTO.
1. Watumiaji wa mtandao tanzania ni wachache mno.


Kama ambavyo tumeona mbinu zinazotumiaka hapo juu, pamoja na faida zake bado zina changamoto kubwa ambazo ni ngumu kuzikabili, hiyo basi ipo haja ya kutumia mbinu ya tano ambayo inaweza kuwa na mafanikio makubwa sana hasa katika kipindi hiki ambapo kuna maendeleo makubwa ya teknolojia.

"UTUMIAJI WA SIMU ZA MKONONI."
NAMNA YA KUTEKELEZA.

Unaweza kuundwa mfumo ambao utaweza kupata namba za simu za wanachama na wapenzi wote(ikibidi watu wote wazima), namba hizo zitatunzwa kwenye mfumo maalum.Inapotokea kuna jambo lolote la kutolea taarifa, ofisi yenye namba hizo iatuma taarifa kwa namba zote.Inapotokea mdau yeyote ana mawazo au taarifa yeyote anaweza kuituma kwenye ofisi inayo dhibiti mawasiliano_Ofisi hiyo itakuwa na wajibu wa kupokea kuchambua na kujibu maswali na ushauri utakaotolewa na yeyote.
FAIDA.
1.Mfumo huu utawafanya wanachama/umma ujisikie kuwa karibu sana na chama na hivyo kujihisi kama wao ndio chama chenyewe.
2. Mfumo huu utaufanya umma ujisikie unathaminiwa.
3. Mfumo huu utawezesha kukika kwa taarifa kwa watu wengi kwa wakati mmoja kuliko mfumo mwingine wowote ule.
4.Mfumo huu unawez kukiwezesha chama kuwa na taarifa/mawazo mengi zaidi kuliko mfumo wowote ule mwingine
5.Mfumo huu utakuwa unatumia gharama kidogo sana.
6.Mfumo huu utakuwa na ufanisi wa ajabu sana wakati wa uchaguzi.

CHANGAMOTO.


1. Zoezi la kupata namba za simu za watu wote ni gumu hivyo linahitaji watu waliojitoa kweli
2.Watu wengine watatumia mfumo huu kuleta usumbufu, kutuuma taarifa za kuudhi, kukatisha tamaa n.k

Kwa ujumla mfumo/mbinu hii ya tano ya mawasiliano na ushirikishaji itakuwa safi kabisa na ikitumika vizuri inaweza kuleta matunda zaidi ya inavyoweza kufikiriwa.Ni vyema mbinu hii ikatumika 2014/2015.Uzuri ni kwamba kwa sasa karibu nusu ya watanzania wana simu. Ikumbukwe kwamba chama mbadala ni lazima kioneshe ubunifu kila mara ili kuonesha umbadala wake kweli. Kuboresha kila mara ni muhimu.CHADEMA wasipoitumia fursa hii, wengine watachukua fursa na kwenda zao!.

 

Fenento

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
320
225
betlehem Well said! Nimatumaini yetu mawazo yako yatafanyiwa kazi na viongozi wa CDM kwa manufaa ya wanamabadiliko Tanzania.
 
Last edited by a moderator:

jebibay

JF-Expert Member
Nov 3, 2012
1,413
2,000
Ni muda sasa nimekuwa sikubaliani na maudhui ya posts zako nyingi (sio zote) ulizokuwa unazipost hapa JF siku za hivi karibuni. Baadhi ya posts nilikuwa nakubaliana na wewe partially....

Kwa mara ya kwanza nakubaliana na wewe kwa 100%.
 

Tumaini Makene

Verified Member
Jan 6, 2012
2,619
1,500

Asante Betlehem kwa mchango wako. Noted. Bila shaka nawe unajisikia vyema kuona kuwa mengi kama si yote uliyoyasema hapa yanatekelezwa kila siku. Mengine si lazima tuyaanike hapa. Tunashukuru sana kwamba wewe ni miongoni mwa Watanzania mamilioni, wanaamini, wana matumaini makubwa na wanaipenda CHADEMA.

Kila mtu aone kuwa ni jukumu lake na wajibu wake kuwa rasilimali (kwa njia mbalimbali) kwa ajili ya CHADEMA na mabadiliko.


 

Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,519
2,000
Mkuu betlehem umeacha risk moja kubwa ya kutumia njia hiyo uliyoipendekeza nayo ni hatari ya kuingiliwa mawasiliano. Ukuaji wa teknolojia unakwenda sambamba na wimbi kubwa la uhalifu wa kiteknolojia, maingiliano ya mawasiliano yanaweza kutumika kupotosha ujumbe au kukwamisha ujumbe usifike unapotakiwa. Tumeona njia hii ilipotumika kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 haikutoa matokeo mazuri sana. Na risk nyingine ni kwa chama chenu kinaweza kuhujumiwa na mashirika ya simu kwakuwa kwanza mashirika ya simu yote makubwa yana mkono wa serikali au CCM au makada wa CCM ( airtel, Voda), pili kwakuwa yanafanya kazi kiujanja ujanja (tigo) hayawezi kuikera serikali kuogopa kuchukuliwa hatua.
Nashauri jaribuni kutumia njia kama ile ya network marketing.
 
Last edited by a moderator:

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,605
2,000
Ni muda sasa nimekuwa sikubaliani na maudhui ya posts zako nyingi (sio zote) ulizokuwa unazipost hapa JF siku za hivi karibuni. Baadhi ya posts nilikuwa nakubaliana na wewe partially....

Kwa mara ya kwanza nakubaliana na wewe kwa 100%.
mkuu wanapokuwepo watu zaidi ya wawili wanaofikiri, hawawezi kukubaliana katika kila kitu na kila wakati.Ukiona wanakubaliana kwenye kila kitu na kila wakati basi ujue kuna mmoja anakuwa ameamua kutofikiri na kumuachia mwenzake kazi ya kufikiri kwa niaba yake lakini kama wote wanafikiri kuna wakati watakuwa wanaenda sawa na wakati fulani wanatofautiana.Hiyo ni kanuni ya kimaumbile.
 

j2chenga

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
201
0

Asante Betlehem kwa mchango wako. Noted. Bila shaka nawe unajisikia vyema kuona kuwa mengi kama si yote uliyoyasema hapa yanatekelezwa kila siku. Mengine si lazima tuyaanike hapa. Tunashukuru sana kwamba wewe ni miongoni mwa Watanzania mamilioni, wanaamini, wana matumaini makubwa na wanaipenda CHADEMA.

Kila mtu aone kuwa ni jukumu lake na wajibu wake kuwa rasilimali (kwa njia mbalimbali) kwa ajili ya CHADEMA na mabadiliko.Makene, pamoja na kwamba nakubaliana na mchango wa Betlehem, nadhani ipo haja ya CDM kuwa na Tv station yake na waandishi na wapiga picha wake. Tumekuwa tukiona picha za mikutano ya CDM ambazo upigaji wake Ni wa upotoshaji kabisa. Picha inakuwa "zoomed-in" na kuonesha sehemu ndogo Sana au mzungumzaji peke yake bila umati unaomsikiliza kuoneshwa kwa mapana yake!
Kwasababu chama Ni chombo cha wanachama na wananchi kwa ujumla, nadhani wanachama watakuwa tayari kuchanga ili kituo cha televisheni kipatikane maana watapata habari sahihi kwa wakati muafaka kuliko hizi propaganda za TBC na vituo vingine ambavyo vinamilikiwa na makada wa ccm.
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,605
2,000
Makene, pamoja na kwamba nakubaliana na mchango wa Betlehem, nadhani ipo haja ya CDM kuwa na Tv station yake na waandishi na wapiga picha wake.
Mkuu pamoja na uzuri wa wazo lako, lakini undeshaji wa TV gharama zake si mchezo. TV mara njingi hutegemea matangazo kuiendesha.TV inahitaji kujipanga kweli maana investment inayohitajika si mchezo.Si swala la kuibuka ndani ya siku chache bali mchakato na mipango ya muda mrefu labda.
 

j2chenga

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
201
0
Mkuu pamoja na uzuri wa wazo lako, lakini undeshaji wa TV gharama zake si mchezo. TV mara njingi hutegemea matangazo kuiendesha.TV inahitaji kujipanga kweli maana investment inayohitajika si mchezo.Si swala la kuibuka ndani ya siku chache bali mchakato na mipango ya muda mrefu labda.

Mkuu nashukuru Sana kwa jibu lako. Nadhani huu uwe Ni mpango mkakati wa muda mrefu. Suala la gharama halikwepeki kwani nadhani CDM inapoteza zaidi kwa kutokuwa na Tv kuliko gharama ambayo ingewekeza kuwa na Tv. Suala la matangazo nadhani siyo issue Sana kwasababu itategemea credibility ya kituo chako na jinsi gani kitajitangaza na kuwavutia watu na kuona Ni kituo cha kutegemewa na matangazo yatakuja tu. Huu Ni mtazamo wangu tu.....
 

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,225
1,195
Yani wewe siku unaniambia unaondoka ccm niliumia sana lakini nilipiga moyo konde kwa sababu wewe ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanaeleza ukweli na mikakati mizuri sana lakini kwa sbb tu ya baadhi ya viongozi Mamangimeza yakawa yanabeza!!

Anyway maisha popote wanasema waswahili,mimi ngoja niendelee kupelekeshana nao ingawa mkuu kwa sasa wameshaanza kuona hali ambayo tulikuwa tunaipigania na kuisema kila wakati!

Unajua baadhi ya viongozi wa ccm ni sawa na wale wawindaji ambao hata ukimuonya kwamba hapo kuna nyuki anabisha tu mpaka wamuume ndio anastuka.

Ila mkuu hongera sana kwa maoni yako ni kazi tu kwa viongozi wa chadema kufanyia kazi ingawa na wao kuna baadhi ya viongozi wao ambao ni Mamangimeza!

Ingawa chadema ni chama ambacho kilikuwa tayari miongoni mwa watu walio wengi wakiacha ubabe waliouanza hasa juu ya madaraka kama ma-ccm basi tunaweza kufanya kitu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom